Okay asa kusema hivi...u talking abt history...hatuwezi badilisha. So wat can we do now...ili tuendelee
Kwanza kabisa mnatakiwa kuacha kuamini miungu ya watu.
Huwezi kuendelea kama unapangiwa dini na Roma, Uyahudi au unasoma dini kwa Kiarabu na kuhiji Mecca na kuelekea Al-Qabr unaposali. Mpaka hapo tu ushahsindwa kwa sababu saikolojia yako ishashikwa umejiweka chini ya Mzungu, Myahudi au Muarabu.
Pili, tunatakiwa kutaka kweli kuendelea kama jamii. Waafrika wengi tunaridhika kirahisi, tunasema hewala hewla, tunaishi kwa kudura za Mungu (ambaye tumepachikiwa tu). Hatuna ari ya kweli ya kutaka maendeleo, tumekubali umasikini wetu na hivyo hatuwezi kuupita.
Inatakiwa tuukatae umasikini, tukubali kwenda kwa mazoea na utamaduni tu, tukubali kukataa tamaduni mbovu, mifumo mibovu na viongozi wabovu, au angalau tujue jinsi ya ku phase out vizuri vitu vibovu. Sasa hivi tunaheshimu sana tamaduni hata kama mbovu, tunaheshimu sana wakubwa na historia.
Umeuliza haya matatizo ya historia tunayapita vipi?
Huwezi kupita tatizo la historia mbaya kama bado unaiheshimu hiyo historia mbaya.
Mfano.
Afrika mpaka leo inatumia US dola kufanya intra-African trade. Biashara kati ya nchi za Africa inafanyikankwa US dollars. Mmarekani anapata nguvu ya ku control hii biashara kupitia US Federal Reserve (tawi la Benki Kuu ya US la New York). Hiki kitu kinaipa nguvi US dollar bila sababu. Kwa nini Waafrika wasifanye biashara zao kwa kutumia hela zao na kuiondoa US katika biashara za Africa? Hakuna sababu nzuri.
Rais William Ruto wa Kenya kaanza kulipigia mbiu hili. Settlement system tayari ipo Addis Ababa Ethiopia.
Lakini sioni Waafrika wakilichangamkia jambo hili. Wanalalamika tu hawana dola. Kwani kufanya biashara kati ya Waafrika ni lazima kuwa na US dollar?
Unaona ujinga wa akili tegemezi zinazoangalia historia tu bila kutaka kui challenge hapo?