Tuangalie sehemu moja tu, kujitambua.
Wahindi wana maandishi yao, wana dini yao, wana falme zao, wana kalenda yao, kabla ya wahindi dhana ya 0 ilikuwa haitumiki katika hesabu, wao ndio wameiongeza, wameanza haya kwa maelfu na maelfu ya miaka.
Ukoloni umekuja kuwaingilia kidogo tu katika mambo yao hayo, sasa umewaacha, wamerudia walipoishia wakajiongeza na mambo ya dunia ya leo.
Chukua Waafrika walio Tanzania ya leo.
Dini yao ya asili imeandikwa katika kitabu gani? Maandishi yao ya asili ni yapi? Kalenda yao ya asili ni ipi? Falme zao kubwa za miaka maelfu na maelfu ziko wapi? Wamechangia nini kipya katika literature ya dunia, sayansi, falsafa?