Afrika tutapata maendeleo endapo tutawapa wazungu nafasi ya Urais na Mawaziri

Mi nafikiri mchakato wa upigaji kura maamuzi ya mwisho kura ya watu wote isiamue ushindi wa kiongozi. kwa sababu hawa wanasiasa wanatumia jamii kubwa ambayo haijaelimika kuingia madarakani kwa njia za rushwa na ulaghai.
 
Inahitajika watu wenye hofu ya Mungu kushika madaraka tuone jinsi nchi itakavyonyooka.
 
Mkuu ina maana tangu uhuru hatujapata hao wenye akili? Mfano nchi yetu tu miaka 60 ya uhuru ni kipindi kirefu sana lakini hatuna uelekeo wowote kama taifa
Kwa hiyo tangu 1961 hakuna kilichofanyika.unaijua hii nchi ilivyokuwa mwaka 1961?narudia tena ardhi tunayo,watu tunao,tunahitaji siada Safi na uongozi bora.tuweke na ubinafsi pembeni.
 
Kwa hiyo tangu 1961 hakuna kilichofanyika.unaijua hii nchi ilivyokuwa mwaka 1961?narudia tena ardhi tunayo,watu tunao,tunahitaji siada Safi na uongozi bora.tuweke na ubinafsi pembeni.
Image ngozi nyeusi miaka 50 imeshindwa kupata siasa safi na uongozi bora..sasa inaweza nini?
 
Nimechk kimbwa .hasa hii inayfndsh chuo ni mishirkina kweli. Kaz kuandk vijarida tu kuvmbua ndo haiwez . Hodar wa makongamano
 
Nimechk kimbwa .hasa hii inayfndsh chuo ni mishirkina kweli. Kaz kuandk vijarida tu kuvmbua ndo haiwez . Hodar wa makongamano
Sasa yule jamaa wa Iramba amewahi kuifanyia nini hii nchi kinachoonekana na amekuwa waziri maranyingi..zaidi ya ule mdomo wa kinyeremba na majungu.
 
Wajerumani walitawala hapa 1885-1919 miaka 34
Waingereza wakashika hatamu kwa miaka 42 (jumla miaka 76)
Tokea tumepata uhuru mpaka sasa tuna miaka 63.

Tulinganishe wakati wa mkoloni mzungu huduma za kijamii afya, elimu, barabara, reli, meli vs watawala weusi (JKN, AHM, BWM, JMK, JPM & SSH) hali ikoje?

Ninakumbuka mpaka 2007 tulikuwa tukitoka Dar kwenda Mwanza tunapitia Arusha/Namanga/Nairobi/Sirari/Mwanza waenda Bukoba walilazimika mpaka kupitia Kampala then Mutukula to BK.

Mzungu sio mwema kiviiilee. Hata bondeni, kuna neema miji wanayoishi watasha, ila kule kwenye makazi ya weusi wamechoka tu.

Wazungu sio wema sana kama inavyodhaniwa! Nenda hata Kahama, Nyamongo au Geita kwenye uwekezaji wa migodi mikubwa ya kukwapua dhahabu, hali sio ya "neema" kama inavyodhaniwa!
 
Kwa kweli lipelekwe Ombi sijui tamko kuwa kutokana na tatizo la kiuongozi tangu nyakati za Ukombozi wa Afrika na Uhuru hadi imeonekana kushindwa kuleta maendeleo kabisa kama ilivyotarajiea,

Maendeleo interms of democracy hakuna bali ni ghiliba na hila tu

Maendeleo ya kiuchumi hali ni mbaya hairidhishi hata kidogo.

Hakuna eneo lenye afadhali.

Waje watuongoze kwa muongo kadhaa hata mitano tu Kisha waturejeshee wenyewe tutakuwa tumejifunza kutoka kwao na watanzania watakuwa wameamka kwenye usingizi wa pono walolala sababu ya ujinga na kutojitambua.
 
Kama rasilimali żazinakabidhiwa wageni Basi uongozi waje wazungu watuongoze kwa miaka 50 tu kwanza na watubadilishie mifumo kama vile ya elimu ili wananchi wajue kujitambua na kuepuka ujinga na unafiki.
 
Wapo watu ambao ni wazuri sana katika nchi hii lakini wanakatishwa tamaa
 
Kina Lisu waandike hiyo hoja waipeleke UN ikajadiliwe Kisha upatikane mrejesho kwa wananchi.

Sababu failures ni kubwa na dhahiri.
 
Maneno ya trump yanaishi[emoji17][emoji17][emoji3]
 
Hata hivyo Hiyo mikopo wanayokopa hayo matrilioni baada ya muda masharti yake ya kuifuta itamgharimu Taifa , na nchi nyingi za Africa zikikutwa hivyo azimio litakuwa la kuja kuwaongoza.

Kwa hiyo this time tunakuwa radhi wenyewe waje kutuongoza haitakuwa kututawala bali itakuwa kutuongoza.
 
Unajua hata maana ya Maendeleo kwanza kabla ya kuandika upumbavu?
 
Elimu bora kwa kila MTANZANIA, Watanzania wote wakielimika hatutoona upuuzi tena Mkuu.

TUNAPELEKESHWA KWASABABU ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA HAWANA ELIMU WALA UFAHAMU WA HAKI ZAO.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Kwa mtaala huu au mtaala mwingne
 
Muafrica awez kusimamia na kusimamia wengine

Boss anakula ganji na watu wa chini sasa apo kitaeleweka kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…