Afungwa jela kwa kosa la kumlawiti mkewe kama adhabu anapokosea

Afungwa jela kwa kosa la kumlawiti mkewe kama adhabu anapokosea

Pole shosti
Unajua maana ya kujipendekeza ww hili ni jukwaa huru yoyote anayezingua anapigwa za uso kama ww anasemwa raisi wa nchi halafu ww unawaambia watu wanajipendekeza kwa lipi sasa tumia akili yako vizuri.
 
Vizuri sana
Mahakama ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imemtia hatiani Dickson Mbwilo (42), mkazi wa Kitelewasi na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumlawiti mke wake.

Kulingana na maelezo ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka (32), mumewe alikuwa akimfanyia kitendo hicho pale anapokuwa amekosea ili iwe ndiyo adhabu yake hali ambayo ilimsababishia sehemu zake za siri kuharibika vibaya.

Hata hivyo, mpaka kufikia hatua ya Mbwilo kutiwa hatiani na kufungwa, mlalamikaji hakuwahi kufika kortini kutoa ushahidi wake, isipokuwa Mahakama iliamua kuegemea maelezo yake aliyokuwa ameyaandika Polisi.

Hukumu hiyo ilitolewa Machi 6, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, Benedict Nkomola na nakala yake kupatikana Machi 12, ikisema ushahidi uliotolewa umethibitisha mashtaka dhidi ya Mbwilo.

Hakimu amesema katika kesi ya jinai, maelezo ya malalamikaji yanaweza yakatumika kama sehemu ya ushahidi kwa kuwa sheria ya ushahidi inatoa utaratibu wa kushughulika na kesi ambazo mlalamikaji atakuwa hapatikani kutoa ushahidi.
 
Utakuta mke ni michezo yake na michepuko ila ameamua kumwangushia jumba bovu mume wake hii kesi imekaa kiwizi sana sana
 
Pamoja na adhabu iliyotolewa, nadhani kulikuwa na haja Mahakama ikajiridhisha zaidi Kwa kupata ripoti ya Daktari.

Lakini pia, isije kuwa hii ni mbinu inayotumika kutuumiza Wanaume.

Unaweza ukawa unapewa hayo mambo kama sehemu ya Starehe na mapenzi yenu na Mkeo alafu baadaye akaja kuitumia kukufunga jela.

Mtafanya Wanaume tuombe talaka Kwa Wake zetu sasa kuogopa hayo yasije kutokea.

Mungu atunusuru Wanandoa, naona Taasisi ya Ndoa inaendelea kupigwa Vita Kila Leo [emoji24]
Mtaalam naona umejikuta unaandika
 
Mtaalam naona umejikuta unaandika
Nimeogopa hiyo case Mkuu, isije kuwa ile agenda yao ya kupoteza Kizazi cha Kiume inaendelea.

Kama wanasapoti Ushoga na mambo ya haki sawa ina maana Wanaume tupo hatarini kupotezwa.
 
Nikikuta umechelewa kupika kifiro
Nikikuta unachat na wanaume wengine kifiro
Nikiacha hela ya nyama nikakuta maharagwe kifiro.
Ukichelewa kujib txt kifiro
Daaaaah!!! Kwa hawa dada zetu wa mjini, atajitahidi kila siku akoseee
🤣 🤣we jamaa shenzi sana
😀
 
Mwanaume Mkazi wa Kitelewasi Mkoani Iringa aitwae Dickson Mbwilo (42), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti Mke wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi amesema Mtuhumiwa huyo alikuwa akimfanyia Mke wake kitendo hicho kama sehemu ya adhabu pale anapomkosea.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye jina lake limehifadhiwa, alikiri ni kweli Mumewe alikuwa akimfanyia kitendo hicho kila alipokuwa amekosea hali ambayo ilimpelekea kusababisha sehemu za siri kuharibika vibaya.

Katika hukumu nyingine, Watu wengine wawili Kheri Lutumo (25) wa Malangali Wilayani Mufindi na Mathayo Kitosi (34) wa Isele Wilayani Kilolo Mkoani Iringa, wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka Watoto wenye umri wa miaka 8 ambao walikuwa wakisoma darasa la pili.
 
Kwanini Huyo Mwanamke hajawahi kushitaki siku zote hizo mpaka ikawa mara kwa mara
 
Back
Top Bottom