TANZIA Aga Khan Afariki dunia akiwa na Miaka 88

TANZIA Aga Khan Afariki dunia akiwa na Miaka 88

Tutafute hela jamaa anang'aa sana kipesa pesa
 
Kuwa na farasi kwahitaji fedha za kumhudumia, eneo kubwa na matunzo. Ni lazima uwe na uwezo mkubwa wa kifedha. Kuhusu tafiti nikifanya kautafiti kadogo sana. Moja ya mambo ambayo nilibaini ni kwamba kuna kitu chaitwa lineage kwamba hakuna kuchanganya damu na mtu ambae hajapitishwa kwani kufanya hivyo kutatoa siri.

Dodi alisababisha madhara makubwa sana na sasa Megan kabanana lakini kashindwa kwani Harry kajitambua na ndo maana wamekimbia mbali na watoto wao kuepusha matatizo.

Hiyo ni kitu adimu chaitwa lineage.
Ni kweli Farasi ni gharama sana nabakia na Mbuzi na kuku na Bata na Mbwa tu nao wamudu kwakweli.
Hilo swala la kuchanganya Damu wenzetu wako makini sana hasa kulinda himya zao nakubaliana na wewe kabisa. Aksante sana kwa Elimu hii
 
Eleweni pia kuwa Aga Khan siyo jina lake bali ni cheo chake kama kiongozi mkuu wa dini ya ismailia; anatambulika kama His Highness The Aga Khan au kwa kifupi HH The Aga Khan. Jina halisi la marehemu ni Prince Shah Karim al-Husseini. Alikuwa Aga Khan kuanzia mwaka 1957 hadi kifo kilipomkuta jana.
 
RIP
Ni wengi ulitufikia, Nilisoma Agha Khan Nursery School huko mikoani hebu fikiria…
 
Dah... Kuna WATU mna taarifa za watu kushinda wahusika wenyewe
Hadi nimeshangaaa mtu ana taarifa kama kaulizwa mwana malundi dah big up ila hujasema kama huyu ndie chanzo cha ugomvi wa bibi titi na nyerere mpk bibi titi akawekwa ndani naishia hapaaaa
 
Shida moja ya ile Hospital ya Agakan ni kutokua na mabingwa wazuri wana vijana pale junior Doctors hawana utalamu wa kutosha. Usafi wako vizuri sana ila huduma zao sio kivile.
Kwa hiyo hata wao pia wananyanganyana na Mhimbiri wale Senior Doctors wa Mhimbiri wanakua pale pia kutoa huduma.
Unajuaje taaluma ya afya ilihali executive officer wote wanatibiwa pale lakini the way ulivyoandika mhimbiri na kurudia nilithibitisha utakuwa dalali wa kupeleka nyama pale hospitali
 
Ukoo wake wa asili ni wa kutokea Iran (siyo Uturuki kama nilivyokuwa nimeandika mwazo), lakini walisambaa sana dunia nzima kuanzia Pakistani hadi ulaya huko Italy na Switzerland na hata Marekani na kanada.
inaonekana walizaliana wengi sana..
 
Aga khan ndo muanzilishi wa
Diamond.Trust Bank
Agha khan hospital
Jubilee insurance

Pia ana magazeti yake, media na biashara nyingi sana, huyu jamaa ni legend kabisa,

Ukienda Bank zote za DTB utaona picha yake ukutani
magazeti ya new habari,citizen TV vp
Jangwani ilijengwa na wakoloni, Azania ilijengwa na serikali ya Mwalimu.

Shule za Aga Khan hapo ni Tambaza (Aga khan Boys) na Zanaki (Aga khan girls). Mzizima sec ilijengwa 1967 baada ya serikali kuzitaifisha shule hizo mbili (A.K boys na girls).
AZANIA ILIJENGWA NA MKOLONI IKIITWA MYENDENI BOYS
 
Ny
Eleweni pia kuwa Aga Khan siyo jina lake bali ni cheo chake kama kiongozi mkuu wa dini ya ismailia; anatambulika kama His Highness The Aga Khan au kwa kifupi HH The Aga Khan. Jina halisi la marehemu ni Prince Shah Karim al-Husseini. Alikuwa Aga Khan kuanzia mwaka 1957 hadi kifo kilipomkuta jana.
Nyerere akimuogopa sana.Muiteni mzee Mohamed Said walau atudondoshee Taazia ya Kiongozi huyu.
 
Ny

Nyerere akimuogopa sana.Muiteni mzee Mohamed Said walau atudondoshee Taazia ya Kiongozi huyu.
Amuogope kwa nini; kwani alikuwa na jeshi lake binafsi kubwa kuliko JWTZ? Watu wanowaza dini muda wote huwa na fikra finyu sana
 
Hii familia hakika wanao mawe, ukiavhana na hospital na Chio cha afya hawa jamaa wana uwekezsji mkubwa sana hasa hoteli zao za Serena Hotel ambazo ni moja ya Brand kubwa sana Eee East Africa.
 
Back
Top Bottom