Age-mates wangu waliojiingiza kwenye ndoa wamechoka, wanatia huruma. Mimi ambaye bado "napuyanga" naponda raha tu

Yana mwisho hayo, ngoja viungo vianze kuchoka na magonjwa ya uzeeni yaanze kugonga hodi, Mungu aliona mbali kumfanya Binadamu awe na Mwenza.
Sio kama I support watu wasioe au wasizae, lakini kuoa au kupata watoto Kwa sababu ya kufikiria utapata usaidizi ukizeeka ni upuuzi wa hali ya juu, wazee wengi tumeona na watoto wao zaidi ya 10, lakini mwishoni wakizeeka na wakiugua wanaishia kupelekwa hospital na kuletewa chakula na majirani, huku watoto wao wakisubiri afe waje kuzika na kugawana mali kama anayo, wewe oa na zaa lakini usisahau kujiwekea pensheni yako itakayokutunza uzeeni
 
kuoa mapema kuna raha yake kama pesa ipo. kama huna pesa wala usioe kabisa, kataa ndoa
 
Endelea kupuyanga finally uzeeni.
 
usijedanganyika mtu akaja kukuambia ndoa ni kitu kibaya. ndoa ni kitu kizuri mno mno, hasa ukimpata mnayeendana. mnakuwa mnapendana, mnapeana kwa uhuru na furaha, mnajaliana, mnakuwa na watoto pamoja, watoto wanawaita baba na mama, pesa unayopata unanunulia watoto vitu mbalimbali mnafurahi nao, mna umoja, mna furaha, mna amani, mnapika na kupakua anytime you wish tena bila kupigwa mizinga, ni kitu cha furaha mno.
 
umejieleza vizuri sana. Unahaki ya kuchanua na kupendeza.
Kumwagiwa za moto kila siku si jambo dogo.
Subiri uzeeni ukiwa single unaharisha na huna mke wala mtoto kukusaidia. Wakati huo hakuna wa kukupumlia tena. Utaelewa show.
 
Subiri uzeeni ukiwa single unaharisha na huna mke wala mtoto kukusaidia.
Kwahiyo unajidanganya kuwa huyo mkeo/mumeo ndiyo atakusaidia uzeeni? Ugonjwa wa figo unaujua? Kansa na kisukari je ? Vipi mwenzi wako akiwa na ugonjwa mmojawapo, utasaidiwa? Temea mate chini mkuu.

Na kuhusu watoto, wao watajitegemea na kuishi mbali na wazazi au pengine ikawa bahati mbaya wakafa wote au wakawa mateja, wadangaji, n k. Narudia tena, temea mate chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ