Mungu atusamehe wote wenye pumzi tunaojifanya ni watakatifu na kuhukumu vile tunavyopenda..
Agness hakuwa malaika, kama sisi tuu kila mtu ana makosa yake, nashangaa wengi mnajifanya humu kama ni wasafi mno na kumsema marehemu kwa mabaya, Mungu atusamehe sana maana najua sote tuna mapungufu makubwa tuu ila tuna jeuri maana bado tuna pumzi ya bure bure aliyotupa Muumba aliyemuumba na agness..
Tukumbuke pia agness ana ndugu, ni dada,mdogo,shangazi n.k , tusiwaumize wenzetu katika kipindi hiki kigumu, licha ya umaarufu wa agness tutambue ana haki zake ikiwemo ya kuheshimu faragha yake.Tujaribu kuheshimu maana njia hiyo ni yetu sote na haikwepeki, zaidi tuombe tubadilike matendo pamoja na kuiombea familia yake katika nyakati hizi ngumu... ni hayo tuu wakuu Please dont judge her...