Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Hapana hajasema kuwa hataki kulipa, ila mie nilichosema ni kuwa walipe bila kuwa na kelele.
Au ngoja nkuulize swali, wakati wa kuomba mkopo si kunakuwa na kanuni na tararibu zake, vipi kuhusu utaratibu was marejesho? Huenda watu walikua wana sign mambo ambayi hawayajui.
Sorry naomba nieleweshe. Samahan lakini.
Teh teh teh
 
Baada ya index number weka mwaka ulomaliza kdt cha nne then inarespond automatic. Kabla hujaweka index number kuna maelekezo ndani ya hicho kibox, iandike kwa kadri maelekezo yanavyokutaka.
Maelezo gani nisaidie sijayaona zaidi ya mfano wa index no
 
Inatakiwa uambatanishe nini ili unufaike na mkopo ikiwa mzazi amefilisika ingawa huko nyuma Hali ya kifedha ilikuwa poa?
 
T
Swala la kulinda thamani ya pesa lilitakiwa kuachwa na cha msingi ingepunguzwa asilimia........ yani ukope leo laki halafu baada ya miaka kumi ulipe laki hiyo hiyo? aiseee
Takataka kabisa
 
Mwendazake yule mtu sijui katokea wapi

Nahisi Hana vinasaba vya utanzania.

Hakuwa binadamu wa kawaida aisee.

Kuna mwamba mfano Mimi namjua Yuko juu ya mawe(Hana kazi) tangu atoke chuo 2012 Hadi leo .

Hiyo VRF yake so ingekuwa maradufu na alisoma engineering.

Duuh aisee his death was good riddance.
 
Swala la kulinda thamani ya pesa lilitakiwa kuachwa na cha msingi ingepunguzwa asilimia........ yani ukope leo laki halafu baada ya miaka kumi ulipe laki hiyo hiyo? aiseee

Huna elimu ya juu kaa kimya
 
Ukiwaambia hivyo wanakwambia kuna watu wamejiajiri wanauza karanga na kuendesha bodaboda wanalipa 10% deni la bodi tens wanakupa na takwimu watu elfu 13.333333333888822222.
 
Swala la kulinda thamani ya pesa lilitakiwa kuachwa na cha msingi ingepunguzwa asilimia........ yani ukope leo laki halafu baada ya miaka kumi ulipe laki hiyo hiyo? aiseee
Una roho mbaya Sana...Kama ni hivyo mbona huwa serikali haiongezi mshahara kucover inflation rate?
 
Kama tunavyojua, kwa mujiba wa katiba yetu Mheshimiwa Rais halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote yule.

Hivyo basi tunapokuwa na rais msikivu tena anayefanyia kazi maoni na malalamiko ya watu wake ni baraka kubwa kwa taifa

Kwa sasa ukiangalia statement ya deni lako kwenye mfumo wa bodi ya mikopo (olas.heslb.go.tz ) utaona kuwa wameondoa tozo zote za VRF, yaani hata zile walizotoza zamani (kabla ya agizo la rais) wameziondoa

Wanufaika wa mikopo tunamshukuru sana Mheshimiwa rais kwa kusikia na kuyafanyia kazi maombi yetu. Tulilalamika sana wakati wa mwendazake lakini tukajibiwa kuwa 'hapangiwi'.

Sasa ni muda wa kila mnufaika mwenye uwezo wa kulipa na alipe, tena wamerahisisha unaweza kulipa hata kwa M-pesa na malipo yako yanaonekana hapohapo kwenye mfumo.

Pia niwakumbushe wadau, twendeni vizuri na mama, naiona katiba mpya hususani wakati wa ungwe yake ya pili Mungu akimjaalia na wananchi wakampa ridhaa.

---- update----
Wadau wengi wameuliza namna ya kuangalia, naamini bodi watatoa maelekezo zaidi lakini kwa hapo ngoja nieleze kwa ufupi.

Ingia kwenye website

View attachment 1830801

Kwenye dashboard (juu kushoto) chagua loan repayment
View attachment 1830804

Kisha baada ya apo, chagua beneficiary/lonee/ employee login

View attachment 1830805

Baada ya hapo ingiza namba yako ya form four kwa format inayo onekana

View attachment 1830806

System itaiangalia namba hiyo kwenye database ya bodi na kukuketea jina lako mnufaika.

Baada ya hapo utathibitisha kuwa ni jina lako kweli kwa ku click hilo jina.

Baada ya hapo utajaza taarifa muhimu kama namba ya simu, email na taarifa za mwajiri pamoja na kutengeneza password.

Ukikamilisha utakua umeshatengeneza account kwenye mfumo wao

Baada ya hapo uta log in as registered user na utaona taarifa zako zote za deni lako. Pia utaona control namba unayoweza kuitumia kulipa mwenyewe.

Natumaini inaeleweka.
NB sijaweka picha za hatua za mwisho kwakua zinaonesha taarifa binafsi za mnufaika.
Nilichogundua baada ya kuingia kwenye hyo portal ni kwamba Deni limeisha na ninawadai Kama laki mbili na pointi. Kitu kingine ninachokiona yani chuo na course niliyosoma ni tofauti kabisa na walichoandika kwenye hiyo statement, Sasa najiuliza hata Hilo Deni nililolipa ni langu kweli? Mi nilikuwa miongoni mwa wanafunzi waliopata multiple admission lakini wao kwenye statement yao wameandika chuo ambacho nilikiacha badala ya chuo nilichosoma. Heslb sidhani Kama wapo serious na kazi yao nahisi Kuna ubambikizwaji mkubwa Sana wa madeni
 
Kweli asee wameondoa manake mi hadi sasa ningekua nadaiwa milioni 20 na ushehe ila imerudi milioni 10 kama na laki 5 ,halafu mpaka sasa mi mpiga Dili ,nlilipaga kaka laki 4 na point kadhaa
 
Sijui nakosea wapi?
Niliomba statement tangia jana wakanijibu watanitumia within 72 hours nyinyi mnawezaje kuona ndani ya muda mfupi?

Back
Top Bottom