Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Naanza kuli jumatatu sasa. Hapo tumekuwa lugha moja na serikali yangu pendwa
 
Mama tumpe mitano Tena, Mimi ngoja nilipe Deni langu kabla miaka yake haijaisha asije kuja mwingine akaridisha hyo VAR
😀😀😀😀 nilisema wasipo ondoa huo utopolo sitolipa kamwe. Hapa jumatatu naenda kifua mbele kabisa kuangaza wapa mzigo wao
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] nilisema wasipo ondoa huo utopolo sitolipa kamwe. Hapa jumatatu naenda kifua mbele kabisa kuangaza wapa mzigo wao
Mwenyewe nilikuwa silipi huo Utopolo Yani elimu ni huduma na sio biashara why watupandishie gharama ya 6 kila mwaka regardless mtu una kazi au hauna. Sasa ni kulipa tu mapema maana akija Rais mwingine kichwa ngumu ni mwendo wa kuumizwa tu.
 
Mlivokua mnapokea mkopo na boom, mlikua mnaona raha san, ila kulipa mnapiga mayowe,
Acheni ujinga, mlipe madeni ya HELSB.
Shida sio kulipa, shida ni kunikopesha halafu kila mwaka deni linajiongeza tu maana yake ni kwamba halitakaa liishe....

Ahsante sana kwa mama, sasa tutalipa deni meno nje, deni lilikua mzigo hili.
 
Swala la kulinda thamani ya pesa lilitakiwa kuachwa na cha msingi ingepunguzwa asilimia........ yani ukope leo laki halafu baada ya miaka kumi ulipe laki hiyo hiyo? aiseee
Elimu ni sehemu ya huduma za jamii. Ni wajibu wa serikali kuwapa wananchi wake huduma zote za kijamii, mfano elimu, afya, barabara nk.

Hivyo, mikopo ya elimu ya juu si biashara ya serikali bali ni huduma ya jamii.
 

Aise! Mama abarikiwe sana sana..tunaomba na katiba mpya aipitishe.

Mungu awabariki, MH RAIS SSH na MWINYI
 
Sasa nikitengeneza account online ili nione deni langu si ndio wataniona na kunigundua coz kwa sasa siko tayar kuanza kulipa na sitaki niingize details zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…