Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Hapa deni langu lmebaki sh.ngapi maana sielewiiiiiii
Screenshot_2021-06-26-16-56-58-94.jpg

Sent from my CPH2083 using JamiiForums mobile app
 
Kama tunavyojua, kwa mujiba wa katiba yetu Mheshimiwa Rais halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote yule.

Hivyo basi tunapokuwa na rais msikivu tena anayefanyia kazi maoni na malalamiko ya watu wake ni baraka kubwa kwa taifa

Kwa sasa ukiangalia statement ya deni lako kwenye mfumo wa bodi ya mikopo (olas.heslb.go.tz ) utaona kuwa wameondoa tozo zote za VRF, yaani hata zile walizotoza zamani (kabla ya agizo la rais) wameziondoa

Wanufaika wa mikopo tunamshukuru sana Mheshimiwa rais kwa kusikia na kuyafanyia kazi maombi yetu. Tulilalamika sana wakati wa mwendazake lakini tukajibiwa kuwa 'hapangiwi'.

Sasa ni muda wa kila mnufaika mwenye uwezo wa kulipa na alipe, tena wamerahisisha unaweza kulipa hata kwa M-pesa na malipo yako yanaonekana hapohapo kwenye mfumo.

Pia niwakumbushe wadau, twendeni vizuri na mama, naiona katiba mpya hususani wakati wa ungwe yake ya pili Mungu akimjaalia na wananchi wakampa ridhaa.

---- update----
Wadau wengi wameuliza namna ya kuangalia, naamini bodi watatoa maelekezo zaidi lakini kwa hapo ngoja nieleze kwa ufupi.

Ingia kwenye website

View attachment 1830801

Kwenye dashboard (juu kushoto) chagua loan repayment
View attachment 1830804

Kisha baada ya apo, chagua beneficiary/lonee/ employee login

View attachment 1830805

Baada ya hapo ingiza namba yako ya form four kwa format inayo onekana

View attachment 1830806

System itaiangalia namba hiyo kwenye database ya bodi na kukuketea jina lako mnufaika.

Baada ya hapo utathibitisha kuwa ni jina lako kweli kwa ku click hilo jina.

Baada ya hapo utajaza taarifa muhimu kama namba ya simu, email na taarifa za mwajiri pamoja na kutengeneza password.

Ukikamilisha utakua umeshatengeneza account kwenye mfumo wao

Baada ya hapo uta log in as registered user na utaona taarifa zako zote za deni lako. Pia utaona control namba unayoweza kuitumia kulipa mwenyewe.

Natumaini inaeleweka.
NB sijaweka picha za hatua za mwisho kwakua zinaonesha taarifa binafsi za mnufaika.
Asante mkuu. Umesomeka.
 
Hapa deni langu lmebaki sh.ngapi maana sielewiiiiiiiView attachment 1830840

Sent from my CPH2083 using JamiiForums mobile app
Jinsi nilivyo elewa hapo kwako ni kama kwangu hapa.
Disbursed amount ni deni lote toka chuoni. Sasa zile zilizoongezeka juu hazionekani.
Inawezekana wanaoanza kulipa sasa watalipa tu deni kamili bila retention fee.
 
Hapa deni langu lmebaki sh.ngapi maana sielewiiiiiiiView attachment 1830840

Sent from my CPH2083 using JamiiForums mobile app
Ni hiyo milioni tatu laki tatu na kitu.

Disbursed amount ni pesa uliyokopeshwa.

Total amount repayed ni hela uliyo lipa mpaka sasa

Total charges ni tozo zao, na hapo ndio palikua na uchawi, ulikua unakuta mamilioni hapo.

Deni lako = (Disbursed amount + total charges) - repayed
 
Shukran mkuu..nmeona..there is a big difference
Wakayi was mwendazake nilienda ofisini kwao wakaniprintia deni la milioni tisa..sasa hv nmecheki deni limepungua hadi milioni mbili.
Ni kweli kabisa, mimi nilipoliona langu kipindi cha mwendazake nilipagawa, nikatamani hata kwenda benki kukopa nimalizane nao.
 
Ni hiyo milioni tatu laki tatu na kitu.

Disbursed amount ni pesa uliyokopeshwa.

Total amount repayed ni hela uliyo lipa mpaka sasa

Total charges ni tozo zao, na hapo ndio palikua na uchawi, ulikua unakuta mamilioni hapo.

Deni lako = (Disbursed amount + total charges) - repayed
Ok asantee asa kule kwenye salary slip inasomeka milioni 6 na kitu

Sent from my CPH2083 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona mi niki log in, naambiwa 'acces denied,' na security code ni kitu gani
Security code ni hayo maandishi yenye herufi na namba za ajabu ajabu, unapaswa kuyajaza kwenye sehemu ya secury code kama yanavyo onekana, herufi kubwa kwa kubwa, ndogo kwa ndogo na namba vilevile. Ni mifumo ya kiusalama ili kuzuia automated bots
 
Mungu ambariki Sana mhe.Rais...nlivoangalia tangazo la watu walioitwa kazini ualimu na afya..plus hi kitu..Nmeamini kweli Mungu amejibu..Nchi yetu sote..Tunaipenda Tanzania Tunaipenda Samia Suluhu
 
Ni hiyo milioni tatu laki tatu na kitu.

Disbursed amount ni pesa uliyokopeshwa.

Total amount repayed ni hela uliyo lipa mpaka sasa

Total charges ni tozo zao, na hapo ndio palikua na uchawi, ulikua unakuta mamilioni hapo.

Deni lako = (Disbursed amount + total charges) - repayed
Kwa ufafanuzi huu ni kama vile hakuna kipya unless kuwe kuna maelezo ya tofauti...how come ujumlishe total charges na disbursed amount (tofauti hapo iko wapi sasa i.e. total chares & disbursed???)
 
Kwa ufafanuzi huu ni kama vile hakuna kipya unless kuwe kuna maelezo ya tofauti...how come ujumlishe total charges na disbursed amount (tofauti hapo iko wapi sasa i.e. total chares & disbursed???)
Uliziona hizo total charges kabla ya VRF kuondolewa zilikua kiasi gani??

Mimi binafsi zilikua zaidi ya milioni 7, zimeondolewa za VRF imebaki laki tatu na kitu ya loan processing fee na administratio fee.
 
Back
Top Bottom