Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Kama tunavyojua, kwa mujiba wa katiba yetu Mheshimiwa Rais halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote yule.

Hivyo basi tunapokuwa na rais msikivu tena anayefanyia kazi maoni na malalamiko ya watu wake ni baraka kubwa kwa taifa

Kwa sasa ukiangalia statement ya deni lako kwenye mfumo wa bodi ya mikopo (olas.heslb.go.tz ) utaona kuwa wameondoa tozo zote za VRF, yaani hata zile walizotoza zamani (kabla ya agizo la rais) wameziondoa

Wanufaika wa mikopo tunamshukuru sana Mheshimiwa rais kwa kusikia na kuyafanyia kazi maombi yetu. Tulilalamika sana wakati wa mwendazake lakini tukajibiwa kuwa 'hapangiwi'.

Sasa ni muda wa kila mnufaika mwenye uwezo wa kulipa na alipe, tena wamerahisisha unaweza kulipa hata kwa M-pesa na malipo yako yanaonekana hapohapo kwenye mfumo.

Pia niwakumbushe wadau, twendeni vizuri na mama, naiona katiba mpya hususani wakati wa ungwe yake ya pili Mungu akimjaalia na wananchi wakampa ridhaa.

---- update----
Wadau wengi wameuliza namna ya kuangalia, naamini bodi watatoa maelekezo zaidi lakini kwa hapo ngoja nieleze kwa ufupi.

Ingia kwenye website

View attachment 1830801


Kwenye dashboard (juu kushoto) chagua loan repayment
View attachment 1830804

Kisha baada ya apo, chagua beneficiary/lonee/ employee login

View attachment 1830805

Baada ya hapo ingiza namba yako ya form four kwa format inayo onekana

View attachment 1830806

System itaiangalia namba hiyo kwenye database ya bodi na kukuketea jina lako mnufaika.

Baada ya hapo utathibitisha kuwa ni jina lako kweli kwa ku click hilo jina.

Baada ya hapo utajaza taarifa muhimu kama namba ya simu, email na taarifa za mwajiri pamoja na kutengeneza password.

Ukikamilisha utakua umeshatengeneza account kwenye mfumo wao

Baada ya hapo uta log in as registered user na utaona taarifa zako zote za deni lako. Pia utaona control namba unayoweza kuitumia kulipa mwenyewe.

Natumaini inaeleweka.
NB sijaweka picha za hatua za mwisho kwakua zinaonesha taarifa binafsi za mnufaika.
Huhuhuuu "You have liquidate your loan" thank u Mama Samia,Fu^k Loan board!!
 
Haki ya mungu mwendazake angefufuka angejua hajui kitu aisee si kwa kupuuzwa huku!??
1) Akina mbowe wameshinda kesi warudushiwe 350milion zao
2)Kufundisha uzalendo kwa kiswahili.....NO
3)Mkopo ya HESLB imerudi kama mwanzo
4)Madaraja ya utumushi yamepanda
5)Hasara ATCL
6)mipaka ya Kenya open
7) Barakoa zinavaliwa mpaka ikulu
8)Ajira elimu na afya
9)vikao vya vyama vya upinzani vinaendelea
10) waliomwabudu akina saaabaya jela!??kukosoa srikali ruksa!
11) Ujenzi wa bandari ya bagamoyo mwekezaji na serikali wapo katika mazungumzo
12) wawekezeji wanakuja
13) Manji karudi!!!
Hahaaahaaaa aiseeeee duuu
 
Sio kweli, kila mtu angekuwa anapandisha tozo ya 6% or less kila mwaka kwa kisingizio cha 'kulinda thamani ya fedha' maisha yangekuwa magumu sana.

Wakati nasoma chuo ada ilikua 1,500,000 kwa mwaka. Leo hii miaka karibu kumi mbele ada ni ileile 1,500,000 na ndiyo mnufaika mpya analipiwa hiyo na bodi.

Sasa kwanini bodi itake mimi nirudishe 1,700,000 wakati kiasi anachopewa mwanafunzi mpya ni kilekile nilichopewa mimi miaka kumi iliyopita?

Plus, HESLB haikuanzishwa kufanya biashara.
Majibu haya yanaonesha kweli shule ipo sio ya ujanja ujanja...
 
Shida sio kulipa, shida ni kunikopesha halafu kila mwaka deni linajiongeza tu maana yake ni kwamba halitakaa liishe....

Ahsante sana kwa mama, sasa tutalipa deni meno nje, deni lilikua mzigo hili.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dea na wee muhanga wa hilo vanga? Acheni kulia lia bhana, lipeni madeni tena kwa riba kubwa, ili wanufaika wawe wengi,
Wanafunzi wahitaji wa mikopo ni wengi msisahau hilo pia.
 
Sio kweli, kila mtu angekuwa anapandisha tozo ya 6% or less kila mwaka kwa kisingizio cha 'kulinda thamani ya fedha' maisha yangekuwa magumu sana.

Wakati nasoma chuo ada ilikua 1,500,000 kwa mwaka. Leo hii miaka karibu kumi mbele ada ni ileile 1,500,000 na ndiyo mnufaika mpya analipiwa hiyo na bodi.

Sasa kwanini bodi itake mimi nirudishe 1,700,000 wakati kiasi anachopewa mwanafunzi mpya ni kilekile nilichopewa mimi miaka kumi iliyopita?

Plus, HESLB haikuanzishwa kufanya biashara.
Kijisentensi cha mwisho kidogo sana ila ndicho chenye majibu (hoja) ya msingi

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Swala la kulinda thamani ya pesa lilitakiwa kuachwa na cha msingi ingepunguzwa asilimia........ yani ukope leo laki halafu baada ya miaka kumi ulipe laki hiyo hiyo? aiseee
Kwani serikali ipo inatengeneza faida?.ama inatoa huduma..
Mishahara inaongezeka 6% nayo sio?!

Heri kuacha 15% rejesho ili deni liwahi kuisha
 
Swali kama wameondoa hiyo tozo tafsiri yake ni kwamba haikuwa halali, je Yale Makato uliyokatwa kinyume na makubaliano utarudishiwa au yanaingia kwenye kupunguza deni? Au ndo unafunika kombe mwanaharamu apite.
Ni kwenda mbele sio retrospectively

sheria ikitungwa leo hatutahukumu kwa matukio ya nyuma
 
Binafsi nimeshindwa kuangalia. Nikianza kuandika namba ya form four kama wanavyotaka tena kwa herufi kubwa, unatokea ujumbe kama unavyoonekana kwenye picha hapa chini. Natamani niangalie deni langu
Screenshot_20210626-230500.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20210626-230411.jpg
    Screenshot_20210626-230411.jpg
    31.6 KB · Views: 1
Sasa nikitengeneza account online ili nione deni langu si ndio wataniona na kunigundua coz kwa sasa siko tayar kuanza kulipa na sitaki niingize details zangu
Dawa ya deni ni kulipa

kidogo kidogo tu

unless kama una uhakika hautakuja kuingia sekta rasmi maisha yako yote ever!
 
Nmeshindwa kuingia,inataka password walau 6,lkn kila nikiwrka inagoms na kuleta ujumbe ule ule
 
kwa hiyo waliolipa hiyo VRF ndo wamepigwa au watarudishiwa
Jmn sheria huwa ni restrospectively...now onwards sio kurudi nyuma

mana makato ya nyuma yalikuwepo kisheria vile vile..

shuleni huwa mnasomea nini jmn
 
Back
Top Bottom