Hero
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 3,932
- 2,839
Kwani lazima umtaje mwenda zake kwenye kila kibaya! Aliyeweka hayo makato si ilikuwa kipindi cha JK na yy alijua kula tu bila kununua ndege, kulipia ada watoto up to form 4, bila kujenga bwawa la umeme la mwl Nyerere dam, wala std gauge railway, na bila ubungo interchange, wala Mameli na mahospitali kujenga 😡! Mnamsakama aliyekuwa anawajengea nchi bila hata yy kufaidika🤔!Kama tunavyojua, kwa mujiba wa katiba yetu Mheshimiwa Rais halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote yule.
Hivyo basi tunapokuwa na rais msikivu tena anayefanyia kazi maoni na malalamiko ya watu wake ni baraka kubwa kwa taifa
Kwa sasa ukiangalia statement ya deni lako kwenye mfumo wa bodi ya mikopo (olas.heslb.go.tz ) utaona kuwa wameondoa tozo zote za VRF, yaani hata zile walizotoza zamani (kabla ya agizo la rais) wameziondoa
Wanufaika wa mikopo tunamshukuru sana Mheshimiwa rais kwa kusikia na kuyafanyia kazi maombi yetu. Tulilalamika sana wakati wa mwendazake lakini tukajibiwa kuwa 'hapangiwi'.
Sasa ni muda wa kila mnufaika mwenye uwezo wa kulipa na alipe, tena wamerahisisha unaweza kulipa hata kwa M-pesa na malipo yako yanaonekana hapohapo kwenye mfumo.
Pia niwakumbushe wadau, twendeni vizuri na mama, naiona katiba mpya hususani wakati wa ungwe yake ya pili Mungu akimjaalia na wananchi wakampa ridhaa.
---- update----
Wadau wengi wameuliza namna ya kuangalia, naamini bodi watatoa maelekezo zaidi lakini kwa hapo ngoja nieleze kwa ufupi.
Ingia kwenye website
View attachment 1830801
Kwenye dashboard (juu kushoto) chagua loan repayment
View attachment 1830804
Kisha baada ya apo, chagua beneficiary/lonee/ employee login
View attachment 1830805
Baada ya hapo ingiza namba yako ya form four kwa format inayo onekana
View attachment 1830806
System itaiangalia namba hiyo kwenye database ya bodi na kukuketea jina lako mnufaika.
Baada ya hapo utathibitisha kuwa ni jina lako kweli kwa ku click hilo jina.
Baada ya hapo utajaza taarifa muhimu kama namba ya simu, email na taarifa za mwajiri pamoja na kutengeneza password.
Ukikamilisha utakua umeshatengeneza account kwenye mfumo wao
Baada ya hapo uta log in as registered user na utaona taarifa zako zote za deni lako. Pia utaona control namba unayoweza kuitumia kulipa mwenyewe.
Natumaini inaeleweka.
NB sijaweka picha za hatua za mwisho kwakua zinaonesha taarifa binafsi za mnufaika.
Kuna watu mnaboa sana! May the merciful God rest the precious soul of our great African hero 💔 Hon Dr JPM in eternal peace and power amen🙏!