Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Kama tunavyojua, kwa mujiba wa katiba yetu Mheshimiwa Rais halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote yule.

Hivyo basi tunapokuwa na rais msikivu tena anayefanyia kazi maoni na malalamiko ya watu wake ni baraka kubwa kwa taifa

Kwa sasa ukiangalia statement ya deni lako kwenye mfumo wa bodi ya mikopo (olas.heslb.go.tz ) utaona kuwa wameondoa tozo zote za VRF, yaani hata zile walizotoza zamani (kabla ya agizo la rais) wameziondoa

Wanufaika wa mikopo tunamshukuru sana Mheshimiwa rais kwa kusikia na kuyafanyia kazi maombi yetu. Tulilalamika sana wakati wa mwendazake lakini tukajibiwa kuwa 'hapangiwi'.

Sasa ni muda wa kila mnufaika mwenye uwezo wa kulipa na alipe, tena wamerahisisha unaweza kulipa hata kwa M-pesa na malipo yako yanaonekana hapohapo kwenye mfumo.

Pia niwakumbushe wadau, twendeni vizuri na mama, naiona katiba mpya hususani wakati wa ungwe yake ya pili Mungu akimjaalia na wananchi wakampa ridhaa.

---- update----
Wadau wengi wameuliza namna ya kuangalia, naamini bodi watatoa maelekezo zaidi lakini kwa hapo ngoja nieleze kwa ufupi.

Ingia kwenye website

View attachment 1830801

Kwenye dashboard (juu kushoto) chagua loan repayment
View attachment 1830804

Kisha baada ya apo, chagua beneficiary/lonee/ employee login

View attachment 1830805

Baada ya hapo ingiza namba yako ya form four kwa format inayo onekana

View attachment 1830806

System itaiangalia namba hiyo kwenye database ya bodi na kukuketea jina lako mnufaika.

Baada ya hapo utathibitisha kuwa ni jina lako kweli kwa ku click hilo jina.

Baada ya hapo utajaza taarifa muhimu kama namba ya simu, email na taarifa za mwajiri pamoja na kutengeneza password.

Ukikamilisha utakua umeshatengeneza account kwenye mfumo wao

Baada ya hapo uta log in as registered user na utaona taarifa zako zote za deni lako. Pia utaona control namba unayoweza kuitumia kulipa mwenyewe.

Natumaini inaeleweka.
NB sijaweka picha za hatua za mwisho kwakua zinaonesha taarifa binafsi za mnufaika.
Kwani lazima umtaje mwenda zake kwenye kila kibaya! Aliyeweka hayo makato si ilikuwa kipindi cha JK na yy alijua kula tu bila kununua ndege, kulipia ada watoto up to form 4, bila kujenga bwawa la umeme la mwl Nyerere dam, wala std gauge railway, na bila ubungo interchange, wala Mameli na mahospitali kujenga 😡! Mnamsakama aliyekuwa anawajengea nchi bila hata yy kufaidika🤔!
Kuna watu mnaboa sana! May the merciful God rest the precious soul of our great African hero 💔 Hon Dr JPM in eternal peace and power amen🙏!
 
Wewe umeboa zaidi. Kwani usingeweza kumsifia Mwendazake bila kumponda JK?Wewe na hao unaowasema mnatofauti gani sasa?Acha hizo wewe
 
Taarifa:

Ni kwamba bodi wameifunga website yao baada ya watu wengi kuingia frequently kufuatilia madeni yao yamebaki kiasi gani au kama wamemaliza.

Mie pia nimeshindwa kuangalia,wamesema tarehe 1 ndo wataifungua.

Nahisi mie nimemaliza ghafla,maana deni lao lilibaki M 2 tu.
Umeenda bodi wakakuambia watafungua website yao tarehe moja?

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Wanasema VRF imefutwa kuanzia 1st May.
Yaani kuna kasiasa Fulani pale bodi
Sasa wameanza ubabaishaji kama ndiyo hivyo tena.

Waliokopa kabla ya 2013, kulikuwa hakuna VRF katika mkataba. VRF ikapitishwa na bunge mwaka 2013, lakini baadae hata waliokuwa na mkataba na hodi kabla ya 2013 waliwekewa VRF.

Sasa, iweje mama afute VRF mei mosi halafu wenyewe washindwe kufuta VRF ya miaka ya nyuma?

Bodi, rejeeni mikataba ya wahitimu kabla ya 2013 mtaona hakukuwa na VRF, mbona rahisi tu!
 
Wanachokifanya wanachukua kiasi cha hela uliyolipa wanaiweka kwenye VRF before 30th April. Kiasi kingine kinawekwa kwenye deni lako halisi.
Waafrika tuna roho mbaya sana.
 
Hebu fafanua tena hii inaongeza au inaounguza deni!?
 
Iko hivi:
Deni lililoko kwenye salary slip siyo deni lililopo bodi.
Kadri unavyolipa kwenye salary slip linapungua lakini kwenye hayo marejesho kwenye computer za bodi hilo rejesho LA kila mwezi wanapeleka kwenye VRF before 1May na nyingine inalipa deni halisi. Huku wewe utaona kwenye slip imebaki milioni 1 kumbe kwao imebaki milioni 2.
Kuna VRF before 1 May.
Chukua statement mkuu, mimi laki 5 imeongezeka
 
Huu ubabaishaji sasa
 
Mkuu, katika watu waliotoa ushuhuda wa kupata statement zao (either mtandaoni au physically kwenye ofisi za bodi) niliowasikia mimi, ni wewe pekee mwenye statement ya aina hii. Wote wanasema tozo za VRF zimeondolewa zote. Sijui kipi ni kipi maana hawajanitumia statement yangu japo niliona mtandaoni

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile app
 
Taarifa:

Ni kwamba bodi wameifunga website yao baada ya watu wengi kuingia frequently kufuatilia madeni yao yamebaki kiasi gani au kama wamemaliza.

Mie pia nimeshindwa kuangalia,wamesema tarehe 1 ndo wataifungua.

Nahisi mie nimemaliza ghafla,maana deni lao lilibaki M 2 tu.
Mimi pia nimeshindwa kuangalia. System haitambui index namba yangu wala chochote kinachonihusu miongoni mwa zile details wanazohitaji. Nimewasiliana nao kwa njia zote walizoweka, hawaja-reply. Akaunti yao ya Whataspp 0736665533 imefutwa.
 
Mkuu, katika watu waliotoa ushuhuda wa kupata statement zao (either mtandaoni au physically kwenye ofisi za bodi) niliowasikia mimi, ni wewe pekee mwenye statement ya aina hii. Wote wanasema tozo za VRF zimeondolewa zote. Sijui kipi ni kipi maana hawajanitumia statement yangu japo niliona mtandaoni

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile app
Ukichukua statement utaona kitu kinaitwa charges
1. Penalty = 0.0
2. VRF = 0.0
3. VRF repaid before 30 April = Hii IPO.
Kwahiyo wanapunguza marejesho yako kidogo wanaweka kwenye hiyo VRF before 30th April
 
Hapo nimekupata vizuri.Mimi jana nilienda ofisi zao hapa Arusha hawatoi statement kabisa.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ukichukua statement utaona kitu kinaitwa charges
1. Penalty = 0.0
2. VRF = 0.0
3. VRF repaid before 30 April = Hii IPO.
Kwahiyo wanapunguza marejesho yako kidogo wanaweka kwenye hiyo VRF before 30th April
Za wenzako (mliochukua pamoja) zina hiyo VRF before 30 April??

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile app
 
Sawa mkuu

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile app
Unajua hao jamaa ni waajabu,wadau hapo juu walioenda Bod wanasema VRF kabla ya tamko la mama bado ipo,Sasa jiulize mbona wao walituingizia 15% hata sisi ambao tulikuwa tushaanza kulipa na sheria ikatukuta tena kwa mkataba wa zamani?Nionavyo mimi HESLB pale bila Raisi kuwapiga chini baadhi ya watendaji akili zao hazitawakaa sawa.Walishaambiwa waondoe VRF kwakuwa ni mzigo mzito hawaelewi.

Sent from my Nokia 2.4 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom