Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumlawiti mke wake

Mahakama ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Boniface Mtweve(28) mkazi wa kata ya Lugarawa kwa kosa la kumlawiti mke wake (27) ambaye jina lake limehifadhiwa.

Akisomewa shitaka hilo na mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Isaac Ayeng'o ilielezwa kuwa mwanamke huyo alienda kwenye harusi na kuchelewa kurudi nyumbani kwake ambapo aliporejea majira ya usiku alimkuta mumewe nje akimsubiri huku akiwa amekasirika.

Amesema mtuhumiwa alimuamuru mkewe kuingia ndani na alipoingia akaanza kumfokea kuwa ametoka kwa wanaume na hakuwa kwenye harusi hivyo anataka amuoneshe kuwa yeye ni ndiye mwanaume ndani ya nyumba ambapo akachukua mafuta na kumfanyia kitendo hicho kitu ambacho ni kinyume cha sheria kifungu namba 154(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Amesema kulipokucha mkewe alitoa taarifa kituo cha polisi na kisha mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo alikana shitaka hilo lakini baada ya kufanyika uchunguzi na kutolewa ushahidi wa pande zote mbili mtuhumiwa alikutwa na hatia na katika utetezi wake aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwani ana watoto wadogo wanao mtegemea.

Kutokana na utetezi huo hakimu huyo aliyapokea maombolezo yake kisha kumhukumu kifungo hicho cha miaka 30 jela huku mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile akisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa wale wote wenye tabia hizo kwani kitendo hicho ni cha kikatili na udhalilishaji.
 
Watoto watakua tu,Kuna watu wanafariki na watoto wanalelewa na mama,huwezi kuvunjiwa utu uendelee kumvumilia kisa watoto,,,,Sasa kichaa kama huyo anaweza hata kulea watoto?
Tofauti jamaa aliatumia nguvu na mwanamke alishajichokea hiyo ndoa mwanaume anahisi mke wake anacheat kila mmoja ana hasira zake.. Ilaa watu huko ndoani kiutaratibu wanajipakuliaa kama kawaaa
 
Asimgeoa hayo yote yasingemkita kiherehere tu kujikuta lijali.
 
Mwanamke akifanyiwa ni kosa la jinai, Ila akifanyiwa mwanaume kwake Haina shida

Cc.Aliyekuwa Waziri Wa KATIBA .. ALIMWINGIZIWA MWANAUME CHUPA Na DPP kaona Hana hatia (Gekul)
Kama umefanyiwa kitendo hicho cha kikatili basi usisite kutoa taarifa katika kituo cha polisi kilicho karibu utahudumiwa asante
 
Watoto watakua tu,Kuna watu wanafariki na watoto wanalelewa na mama,huwezi kuvunjiwa utu uendelee kumvumilia kisa watoto,,,,Sasa kichaa kama huyo anaweza hata kulea watoto?
Huyo mke kadanganywa na hawala wamfunge jamaa ili wawe huru.

Kitakachotokea, hawala nae ataingia mitini.

Kwa kumfunga jela mumewe, huyu mwanamke atajuta sana, maana hata watoto watamtenga. maisha yake yote
 
Hizi baridi mkiendekea kutembea usiku na kuchelewa kurud kwa kisingizio chochote tutawamaliza. Hamwez kutuacha ndani na upwiru wakati tumewabadirisha na Ng'ombe.
Subirini joto lichanganye mtazurura tu kwa amani.
 
Wanaacha kuyafunga mashoga wanahangaika na ndoa za watu [emoji706][emoji706]
 
Duh! Kwahiyo Mume alitegemea baada ya hapo iweje, waongeeje?

Kwanini aliona hiyo ndio yaweza kutumika kama adhabu? Hajui kuna watu wanafanya kwa starehe? Mke angefurahia ingekuwaje? Kama wana watoto sijui itakuwaje? Wataambiwa baba yao alifungwa kwa kosa gani? Watoto wataamua kumsamehe baba yao siku moja??

Aisee nina maswali ambayo siwezi pata majibu maana mhusika yuko nyuma ya nondo.
 
Lipoti ya dakitari hiko wapi?ushahidi wa dakitari ndio wa muhimu kwenye swala hili hakimu hakutenda haki bhana
 
Mbona awakusema kuwa dakitari kathibitisha?
 
Hivi hakuna jinsi mama anaweza kurudi mahakamani kumwombea mkewe msamaha
Kosa likiitwa Jinai unaenda kupambana na mtu anayeitwa Jamhuri. Hakuna wa kukuombea msamaha hata huyo aliyekushtaki, Labda upunguziwe adhabu au ukate rufaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…