Issue sio kazi..., issue ni kama kazi zilizopo / zinazofanyika zinampatia mtu kipato.....
Huwezi kutegemea mtu mmoja awe producer, marketing, human resource na market researcher, hilo halipo..., wakulima wamelima zao mahindi kule alafu utegemee wao wao ndio waingie kitaa kufatufa masoko (wakati kuna walanguzi wanawatazama na serikali inawakataza wasiuze nje mazao yakiwa machache na kuwasahau yakiwa mengi)...
Kujiajiri na kuwa street smart sio elimu ya shule ni they way mtu alivyo (attitude) na inahitahi uvumilivu na discipline, aina ya watu hao ni wachache kama 10% katika population na ni hao ndio wanaweza kufungua fursa za wengi ambao wanaishi pay-check to pay-check so long as wanapata malazi, mavazi na chakula (middle income) hilo sio tatizo...
Ofcourse kuna tatizo na elimu yetu pia its not fit for purpose....
Imebidi niangalie tupo Jukwaa gani mara mbili...., Mkuu tukiongelea Mbinu za Tanzania kuchukua Kombe la dunia haimaanishi tutachukua kombe lijalo au kama tutachukua maishani mwetu..., ni kuongelea mbinu theoretically... baada ya hapo watu wanaweza kuboresha, kubadilisha au kupuuzia ila haikatazi...