Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Tumia akili yako kulima kwa mtaji mdogo unapata mazao.mengi. kwa mfano unaweza usitumie mbole za viwandani badla yake ukakusanya samadi toka kwa wafugaji kwa kuwapati pesa kidogo sana. Ukamwaga samadi hekari tano. Ukavuna mpk dunia ikakushangaa
Mkuu umelewa nini mbna kama idea zako ziko kinadharia sana we mtaji wa kumudu ekari tano unauonaje

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Sexless emb ntajie kijijini kimoja huko Tanga mie niende nkajitwalie ardhi bure nianze mdogomdogo kwenye kilimo, then ntaleta mrejesho.
 
Mfano WA kilimo cha biashara ni kilimo cha maua huko Kaskazini, kilimo cha chai na Pareto huko kusini.
Kilimo cha biashara siyo aina ya mazao yanayolimwa bali ni malengo uliyojiwekea. Unaweza kulima maharagwe, mahindi, mpunga ama viazi kwa lengo la kuuza ili kupata pesa. Tayari hicho kinakuwa kilimo cha biashara.
 
sasa maana ya wao kusoma mpaka vyuo vikuu iko wapi?.... huko huko shule ya msingi si tungewafundisha tu skills za maisha + hicho kilimo then tuwaache waje mtaani...
Kuwa na vyuo vikuu vingi katika nchi ni kuongeza idadi ya masikini nchini.ilitakiwa vyuo vya ujuzi ndo viwe vingi watu wajifunze ujuzi wakazalishe
 
Mkuu Sexless emb ntajie kijijini kimoja huko Tanga mie niende nkajitwalie ardhi bure nianze mdogomdogo kwenye kilimo, then ntaleta mrejesho.
Nenda Gairo Morogoro kisha elekea Chakware Kijiji cha Ngiloli. Hiki kimepakana na mkoa wa Tanga. Huko uliza wenyeji watakupeleka. Utapata ardhi virgin kabisa. Ila kunahitaji ulinzi mkali wa wanyama waharibifu wa mazao
 
Ukiwa na mtaji wa kuanzia na kujaribu tena unakuwa na kiburi cha kusema haya unayosema.
Fresh graduate atatoa wapi pesa ya majaribio yote hayo?
Anaishi vipi muda wote wa majaribio? Yaani anakuka nini, anapataje matibabu na anavaa nini?

Pia ukiwa na watu wa kukubeba inawezekana usemayo.
Umesema vema sana, yaani ukiangalia comments za watu unagundua kwamba huyu anaelewa anachokisema, lakini mwingine labda kwa sababu ya hali nzuri aliyonayo kiuchumi( kwa kubebwa ) anaona ni rahisi sana hiyo shughuli.

Nawambieni vijana wengi ideas zipo, lakini unaanzaje ndiyo kasheshe hususani financial means
 
Kichekesho cha mwaka.
Yaani mtu alieajiriwa anaita wasio na ajira akawashauri namna ya kujiajiri ,
Aaache kwanza hiyo kazi ,aingie kwenye kilimo cha mboga mboga ndio aitishe huo mkutano .

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
Nenda Gairo Morogoro kosha elekea Chakware Kijiji cha Ngiloli. Hiki kimepakana na mkoa wa Tanga. Huko uliza wenyeji watakupeleka. Utapata ardhi virgin kabisa. Ila kunahitaji ulinzi mkali wa wanyama waharibifu wa mazao
Shukran sana mkuu Sexless , Gairo napaelewa. Chakwale na Iyogwe nadhani ndio zipo ukanda mmoja.

Ngoja tukalime viazi vitamu, huwa vinakubali sana maeneo hayo na wala huwa hawatumii mbolea, ni kulima matuta, kupanda mbegu, kupalilia na kusubiri mavuno tu.
 
Tumia akili yako kulima kwa mtaji mdogo unapata mazao.mengi. kwa mfano unaweza usitumie mbole za viwandani badla yake ukakusanya samadi toka kwa wafugaji kwa kuwapati pesa kidogo sana. Ukamwaga samadi hekari tano. Ukavuna mpk dunia ikakushangaa
Mim kama msomi nisiye na ajira ,uzi huu umeniuma..ila najifunza.
Ndugu yangu hapa pa kukusanya mbolea ya kuenea heka tano utatumia kichwa,au nguvu kazi watu au chombo cha moto cha kukodi.
Kutumia kichwa hutamaliza kwa haraka peke yako,kama utahitaj kukod nguvu kaz ,ni bora kununua ya viwabdan mana gharama hazikwepeki.

Hii comment imekaa kinadharia,
 
jamaa yangu mbona sasa unazungumzia hela hela mara hela kidogo....hakuna kilimo rahisi duniani cha kutumia nguvu zako tu bila hela karne hii... jaribu kutoa mbinu nyingine....Dunia ya sasa inahitaji kianzio kwa maana ya hela uweze kutafuta uelekeo....hata udalali tu wa vyumba nao unahitaji mtaji....
 
Back
Top Bottom