Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umetengeneza hoja yako vizuri sana 👍 tunahitaji cross sectoral approach ie mtu kasoma HR apewe basi idea ya kilimo na ufugaji au ujasiliamali hivyo kwa wahandisi na fani zingine lakini serikali haiwezi kukwepa jukumu la kuweka mazingira wezeshiI agree kuna fursa kwenye kilimo, kina potential sababu kuna ardhi kubwa nzuri tu, ila wasomi wajengewe msingi itakayo watayarisha both mind and body kukabiliana na kilimo, tatizo sio upatikanaji wa ardhi peke yake, Utampa graduate wa engineering piece of land afanyie nini? Kuna kujua wapi ni pa nini,nitapigana vipi na madalali wa mazao etc hapo unaona umuhimu wa kuwa na basic knowledge ya kilimo, mzigo wote unarudi kwa serikali. Serikali inapoteza rasilimali watu kwa kutotomia fani za watu vyema. Engineering hakupaswa kwenda kilimo,na kama ulikua unataka akimaliza Huyu engineering graduate afanye kilimo basi ungemuandaa kwa ku incorporate agriculture kwenye syllabus aliyokua anasomea. Kumsomesha mtu miaka 3 halafu usimpe ajira ni wastage of resources! Things can be improved ila ni jukumu la serikali kujenga good infrastructure
Hivi wewe ambaye unajiita umesoma halafu inalalamika kuwa huna kazi, unafahamu kwamba unajidhalilisha?
Acha wakose kazi vijana wa Ulaya na Marekani huko lkn siyo hapa Tanzania. Ardhi yenye rutuba isiyohitaji mbolea imejaa tele kwann usijiajiri kwenye kilimo?
Ardhi ya bure ipo tele katika mikoa ya Tabora, Katavi, Tanga, Ruvuma, n.k.
Kwani lazima ukae mjini? Mbona watanzania zaidi ya 80% wamejiajiri ktk kilimo tena wengi wao hawana madigrii kama ninyi lkn maisha yanasonga na ni watulivu wala hawapigi kelel za kukosa ajira.
Wengi wenu mmesomeshwa na wazazi wenu ambao ni wakulima wasiokuwa na elimu. Hawajawahi kuajiriwa na yeyote maisha yao yote.
Mmerogwa na nani ninyi mnaoenda shule? Kama hizi shule na vyuo mnavyoenda ndiyo vinawapeni huu ujinga mm nashauri zifutwe.
Kuna vijana chungu nzima walioishia darasa la saba wanaendeleza maisha kwa kilimo na shughuli nyingine hatusikii wakililia ajira. Wewe msomi umesoma halafu unalia. Usingesoma je? Jinga kabisa!
View attachment 1974112
Umeandika madini kweli kweli shida simu unayotumia inaonyesha kabisa haupo serious na maisha!!!!???Mtu ambaye huwa anawaponda wasomi kwa nini hawalimi nabaki namshangaa.
Gharama za kilimo ni kubwa na bei ya mazao ni ndogo. Soko la mazao la ndani si zuri kwa sababu nguvu ya manunuzi kwa Watanzania wengi ni dhaifu.
Mtoa mada unafahamu bei ya mbolea na bei ya mahindi kwa sasa?
Ili kilimo kistawi, ni lazima watu wenye mitaji yao wajenge viwanda ili kupata soko la kimataifa. mfano, vya nguo-(pamba), kusindika mboga mboga (nyanya nk).
Huku nilipo, kuna vijana wanapiga kazi za kulima matikiti kwa gharama kubwa, lakini wanakuja kuuza bei ndogo.
Kule kijijini wazee wanakomaa na kilimo cha kujikimu, na wanafanya hivyo kwa kuwa hawana namna. lakini kiukweli, ni wakulima wachache sana wa Tanzania wanaofurahia kazi ya kilimo kwa kuwapatia faida.
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Uliingia mkataba na nani kwamba ukisoma lazima uajiriwe?7 years (Primary)+4 years (O level)+2 years (A level)+4 years (Bachelor)=17years (Assuming hujafanya masters and PhD), nimepoteza miaka 17 shuleni, nikiamini kwamba hiyo miaka na jasho langu nililoliweka kwenye hiyo miaka ndiyo uwe mtaji wangu kupitia ajira rasmi, then uniambie futa hiyo miaka 17, ukaanze upya kwa kilimo!! Kuwa serious!! Je hiyo miaka 17 ningefocus kwenye kilimo bila kushurutishwa na serikali na wazazi kwenda shuleni unadhani ningemsumbua mtu kutaka ajira zenu? Ajira tunazidai sababu tumetumia jasho letu kwa miaka 17 ili kuipata hiyo ajira, ambayo since day 1 tunaingia shule tuliulizwa unataka kuwa nani, na tukajichagulia tu like Banker, Engineer, Rubani n.k.., then namaliza unaniambia nikalime?
[emoji3581]Mleta uzi umeongea kinadhalia bila kujenga hoja za msingi ie kilimo ni biashara Kama zilivyo biashara nyingine, umesema ardhi ipo tele lakini usichojua hiyo ardhi sio bure je huyu kijana pesa anapata wapi kununua hiyo ardhi?
Umeongea kujiajiri kwenye kilimo kama kwenda kunya yaani unaenda chooni unakata gogo unatoka, Dada kilimo hakiko hivyo labda unaongea kwa kuwananga vijana wasio na ajira lakini sio kuwasaidia, kilimo ni mchakato sio kama unavyowaza wewe mfano Mimi nilipata pesa kidogo kwa kusikiliza watu kama wewe nikasema ngoja nilime nikatumia kama 2m kulima alizeti nje ya muda nikambulia 7k nikawa nimekula loss ya 1.3 hivyo ukiwa unawananga vijana uwe practical sio umekaa kwenye key board unaandika tu na hapo nimetoa uzoefu wangu Mimi nilikua na mtaji je wale wasiokua na mtaji hali ni mbaya
Wewe hauna tofauti na ma inspirational speaker wengine unahifanye ku inspire kumbe ni mbinu yenu ya kuwageuza vijana mtaji
Iyo hasara kwa mtu ambaye unasema auze laptop yake na simu,mtaji wa kuchoma Moto mara tatu utampa wewe, dada tulia ujue tunakutukana kimyakimya usije tufanya tukayaweka kwenye keyboardTatizo mnataka mkiwnzq tu mtoke na hela ndefu. Kubali kupata hasara hata miaka 3 wakati unajifunza
Acha uongo wewe , Takwimu zako za kijinga umezitoa wapi?Kama kilimo kingekuwa kinalipa,basi mikoa ya Kanda ya ziwa,nyanda za juu kusini ingeongoza kwa kipato kimkoa na mchango kwenye pato la Taifa,lakini unajua mkoa unaoongoza?ni Dar es salaam,mkoa ambao hauna shughuri kubwa za kilimo lakini unachangia asilimia 80 ya pato la Taifa!!
Kwa kila shilingi 100 inayoingizwa kwenye mfuko wa Taifa,asilimia 80 inatoka Dar!!hiyo mikoa inayolima ipo wapi??
Hoja zako kwamba vijana wakiomaliza vyuo waende mikoani,wakamate ardhi(ambayo ipo bwelele)walime,zimekaa kinadhalia tu na ni story za kwenye makaratasi hazina uhusiano na Hari halisi iliyopo kwenye mazingira yao.
Huwezi kutoka hapa ukaenda Katavi,ukachukua ardhi,ukaanza kulima mahindi,ukavuna!na ukapiga pesa ndeefu!?
Mfuko wa mbolea unauzwa 100000Tsh,gunia la mahindi linauzwa 20000Tsh!
Achana nae, hao ndio wanakuwaga na masponsor kazi Yao kuona wenzao wezembe tu, kumbe anatuletea Mambo ya majaribio mtu akiwa anavumilia hasara mara 3 .DU!!Ukiwa na mtaji wa kuanzia na kujaribu tena unakuwa na kiburi cha kusema haya unayosema.
Fresh graduate atatoa wapi pesa ya majaribio yote hayo?
Anaishi vipi muda wote wa majaribio? Yaani anakuka nini, anapataje matibabu na anavaa nini?
Pia ukiwa na watu wa kukubeba inawezekana usemayo.
Achana nae huyo ajitambuiNimelima nikiwa hapohapo na ni mashamba ya nyumbani sikukodi hizo hela nilitumia kwenye mbegu,vibarua usafiri na vitu vingine inshort nilitamani nifanye kilimo ful time job bila kuadhiriwa lakini niliangukia pua Sasa kuna vijana wangapi wamekata tamaa katika mazingira Kama hayo
Ajitambui huyo achana naeHasara miaka 3 unakula nini ndani ya hio miaka 3? Nina uhakika umeajiriwa au una shughuli nyingine ya kukuingizia kipato,kilimo unakifanya kama shughuli ya ziada tu, mkuu ungekua tu ndio umetoka chuo, huna kazi ,wazazi wanakutegemea afu mtu anakuambia hasara ya miaka 3, utamuelewa? [emoji848][emoji848][emoji848][emoji4]
Nipo sirias na maisha ndiyo maana nina simu hii. Sina uwezo wa kununua sumsung mana yatakuwa yale yale, ukiomba mtaji unaambiwa, "Uza simu yako ndiyo mtaji. Unamiliki simu ghali halafu huna hela?"Umeandika madini kweli kweli shida simu unayotumia inaonyesha kabisa haupo serious na maisha!!!!???
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Hajitambui huyo achana nae7 years (Primary)+4 years (O level)+2 years (A level)+4 years (Bachelor)=17years (Assuming hujafanya masters and PhD), nimepoteza miaka 17 shuleni, nikiamini kwamba hiyo miaka na jasho langu nililoliweka kwenye hiyo miaka ndiyo uwe mtaji wangu kupitia ajira rasmi, then uniambie futa hiyo miaka 17, ukaanze upya kwa kilimo!! Kuwa serious!! Je hiyo miaka 17 ningefocus kwenye kilimo bila kushurutishwa na serikali na wazazi kwenda shuleni unadhani ningemsumbua mtu kutaka ajira zenu? Ajira tunazidai sababu tumetumia jasho letu kwa miaka 17 ili kuipata hiyo ajira, ambayo since day 1 tunaingia shule tuliulizwa unataka kuwa nani, na tukajichagulia tu like Banker, Engineer, Rubani n.k.., then namaliza unaniambia nikalime?
Hajitambui huyo achana naeHiyo hasara ya miaka mitatu ni shillingi ngapi?