Kama kilimo kingekuwa kinalipa,basi mikoa ya Kanda ya ziwa,nyanda za juu kusini ingeongoza kwa kipato kimkoa na mchango kwenye pato la Taifa,lakini unajua mkoa unaoongoza?ni Dar es salaam,mkoa ambao hauna shughuri kubwa za kilimo lakini unachangia asilimia 80 ya pato la Taifa!!
Kwa kila shilingi 100 inayoingizwa kwenye mfuko wa Taifa,asilimia 80 inatoka Dar!!hiyo mikoa inayolima ipo wapi??
Hoja zako kwamba vijana wakiomaliza vyuo waende mikoani,wakamate ardhi(ambayo ipo bwelele)walime,zimekaa kinadhalia tu na ni story za kwenye makaratasi hazina uhusiano na Hari halisi iliyopo kwenye mazingira yao.
Huwezi kutoka hapa ukaenda Katavi,ukachukua ardhi,ukaanza kulima mahindi,ukavuna!na ukapiga pesa ndeefu!?
Mfuko wa mbolea unauzwa 100000Tsh,gunia la mahindi linauzwa 20000Tsh!