Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Afue tu. Hamna kitu kirahis kama huna pa kuanzia wala source ya kukianzisha.
Mkuu Hawa wasomi wana laptops za laki 7 mpk milioni 1, wengine wana simu janja za laki 3 mpk milioni. Yote hii ni mitaji tosha kabisa kwa kilimo. Sema Kuna kasumba miongoni mwa wasomi kwamba kilimo ni kwa ajili ya wasiosoma.

Watapata tabu Sana wasipobadilika.
 
Issue sio kazi..., issue ni kama kazi zilizopo / zinazofanyika zinampatia mtu kipato.....

Huwezi kutegemea mtu mmoja awe producer, marketing, human resource na market researcher, hilo halipo..., wakulima wamelima zao mahindi kule alafu utegemee wao wao ndio waingie kitaa kufatufa masoko (wakati kuna walanguzi wanawatazama na serikali inawakataza wasiuze nje mazao yakiwa machache na kuwasahau yakiwa mengi)...

Kujiajiri na kuwa street smart sio elimu ya shule ni they way mtu alivyo (attitude) na inahitahi uvumilivu na discipline, aina ya watu hao ni wachache kama 10% katika population na ni hao ndio wanaweza kufungua fursa za wengi ambao wanaishi pay-check to pay-check so long as wanapata malazi, mavazi na chakula (middle income) hilo sio tatizo...

Ofcourse kuna tatizo na elimu yetu pia its not fit for purpose....

Hapo sasa. Kwanza mbolea inavyopanda kila siku wakulima wengi watashindwa kulima tena. Na ili upate mazao mazuri mbolea muhimu. Labda wakulima wakipungua demand itakua kubwa supply kidogo bei za vyakula zitapanda mkulima atafaidi ila consumer atakoma.
Nendeni mikoa kama Katavi huko mpunga unalimwa bila mbolea. Mahindi unaweza kulima kwa kutumia samadi peke yake. Mwanzo mgumu. Jifunzeni kuanzia chini
 
Hivi wewe ambaye unajiita umesoma halafu inalalamika kuwa huna kazi, unafahamu kwamba unajidhalilisha?

Acha wakose kazi vijana wa Ulaya na Marekani huko lkn siyo hapa Tanzania. Ardhi yenye rutuba isiyohitaji mbolea imejaa tele kwann usijiajiri kwenye kilimo?

Ardhi ya bure ipo tele katika mikoa ya Tabora, Katavi, Tanga, Ruvuma, n.k.
Kwani lazima ukae mjini? Mbona watanzania zaidi ya 80 wamejiajiri ktk kilimo tena wengi wao hawana madigrii kama ninyi lkn maisha yanasonga na ni watulivu wala hawapigi kelel za kukosa ajira.

Wengi wenu mmesomeshwa na wazazi wenu ambao ni wakulima wasiokuwa na elimu. Hawajawahi kuajiriwa na yeyote maisha yao yote.

Mmerogwa na nani ninyi mnaoenda shule? Kama hizi shule na vyuo mnavyoenda ndiyo vinawapeni huu ujinga mm nashauri zifutwe.

Kuna vijana chungu nzima walioishia darasa la saba wanaendeleza maisha kwa kilimo na shughuli nyingine hatusikii wakililia ajira. Wewe msomi umesoma halafu unalia. Usingesoma je? Jinga kabisa!

View attachment 1974112
usilolijua ni usiku wa giza kama umefanikiwa kwenye chochote kila shukuru sana mungu alafu mwambie muumba tafadhali usije nipitisha kwenye kikombe cha mateso..
 
usilolijua ni usiku wa giza kama umefanikiwa kwenye chochote kila shukuru sana mungu alafu mwambie muumba tafadhali usije nipitisha kwenye kikombe cha mateso..
Nakupitisha kwenye lango kuu la fursa nchini Tanzania mkuu. Sifanyi mzaha hapa. Nakasirika sana kuona maomi anaosha vyombo kwa shemeji yake mwaka mzima eti kisa hajapata kazi. Kwann ??
 
Hapo sasa. Kwanza mbolea inavyopanda kila siku wakulima wengi watashindwa kulima tena. Na ili upate mazao mazuri mbolea muhimu. Labda wakulima wakipungua demand itakua kubwa supply kidogo bei za vyakula zitapanda mkulima atafaidi ila consumer atakoma.
Yeah mkuu wew unaelewa unajuwa Kama unafanya kilimo cha biashara s kirahis kihivo tuko Weng sasa Hiv mpaka matajir wakubwa wanafanya biashara ya kilimo
 
Naoma una mashamba yako ya urithi huko katavi unatafuta wa kukodi[emoji28]
Hapana. Nimetaja mikoa 5 kwenye uzi wangu ambako mashamba hupatikana bure kabisa. Nenda hata Leo utapewa ardhi bure
 
Hapo sasa. Kwanza mbolea inavyopanda kila siku wakulima wengi watashindwa kulima tena. Na ili upate mazao mazuri mbolea muhimu. Labda wakulima wakipungua demand itakua kubwa supply kidogo bei za vyakula zitapanda mkulima atafaidi ila consumer atakoma.
Mimi msimu huu sijalima mahindi maana ya mwaka jana bado yako stoo na mbolea imepanda sana. Nilikwenda duka la pembejeo nikaabiwa DAP mfuko wa kilo 50 shs 130,000!
 
Yeah mkuu wew unaelewa unajuwa Kama unafanya kilimo cha biashara s kirahis kihivo tuko Weng sasa Hiv mpaka matajir wakubwa wanafanya biashara ya kilimo
Suluhu ya tatizo hili Ni kuishinikiza serikali kufungua mipaka ili mazao yauzwe hadi Somali huko
 
Mkuu Unafikir hatulimi sasa mtu unalima na mahindi unapata ya kutosha ila sasa changamoto n nying kuliko faida mkuu mm n mwenyej wa mbeya ukiacha mbali madawa na mbolea ukija kupiga usafir ukija kupiga vibarua ukija kupiga tozo kod haya unataka kuuza Unakuta gunia ef 30 soko market n tatizo pia
Kilimo cha mdomo rahis kweli sio cha shambani. Ukodishe shamba kama huna, utafute vibarua, ununue mbegu, mbolea hii inayopanda kila siku, madawa, sumu za wadudu, booster. Hapo bado hujaibiwa
Tunaofanya miradi ya kilimo tuna cheeka tukiona asiyejua mambo ya shambani anavyo ongea kirahi rahisi tu.
Nililima mahindi kisha akaja myonyaji mmoja anasema nimuuzie mabichi 150/- kwa indi moja nikamtimua sasa nakula ugali mweyewe na kulisha kuku.
 
Walau unapata faida kupitia kuku, kuliko aliyekaa bure.
 
Hivi wewe ambaye unajiita umesoma halafu inalalamika kuwa huna kazi, unafahamu kwamba unajidhalilisha?

Acha wakose kazi vijana wa Ulaya na Marekani huko lkn siyo hapa Tanzania. Ardhi yenye rutuba isiyohitaji mbolea imejaa tele kwann usijiajiri kwenye kilimo?

Ardhi ya bure ipo tele katika mikoa ya Tabora, Katavi, Tanga, Ruvuma, n.k.
Kwani lazima ukae mjini? Mbona watanzania zaidi ya 80 wamejiajiri ktk kilimo tena wengi wao hawana madigrii kama ninyi lkn maisha yanasonga na ni watulivu wala hawapigi kelel za kukosa ajira.

Wengi wenu mmesomeshwa na wazazi wenu ambao ni wakulima wasiokuwa na elimu. Hawajawahi kuajiriwa na yeyote maisha yao yote.

Mmerogwa na nani ninyi mnaoenda shule? Kama hizi shule na vyuo mnavyoenda ndiyo vinawapeni huu ujinga mm nashauri zifutwe.

Kuna vijana chungu nzima walioishia darasa la saba wanaendeleza maisha kwa kilimo na shughuli nyingine hatusikii wakililia ajira. Wewe msomi umesoma halafu unalia. Usingesoma je? Jinga kabisa!

View attachment 1974112
We kulima unafikiri mchezo!!!
 
Haya madigrii tuyafungie stoo! Tupambane na mtaa. Huwa nashangaa matajiri wako bize kupita maelezo lakini wasio na kitu wanalala tu wakiamka wanajilizaliza tu! Mtu kasoma BVM (udaktari wa mifugo) anang'ang'ania mjini kulilia ajira njoo Bush uwasaidie wafugaji ambao mifugo yao inatibiwa na la Saba failure wenye uzoefu tu.
 
Njoo Iringa nikupe shamba heka 5 ulime mwaka mzima halafu uje ulete mrejesho hapa.

Kilimo kinahitaji uvumilivu, mtaji na ukishavuna bei ya mazao yako anapanga dalali au serikali.

Njoo ulime. Ni rahisi sana kuongea ukiwa umeshiba umekaa sebuleni kwako nakuona watu wengine wote wavivu.

Kama Kilimo kinalipa Mbeya, Iringa, Ruvuma na Njombe zisingekuwa na maskini.

NB: bei ya mfuko mmoja wa mbolea ni 120,000.
 
Back
Top Bottom