Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Mleta uzi ntakuunga mkono kama wewe umejiajiri, ila kama unaleta hizi dhihaka kwa vijana wetu wakati na ww ni muajiriwa tu utakua na matatizo sio bure.!
Sio Tu muajiriwa ata watoto zao wanawapa connection ndani ya taasisi majina yanajirudia tu!!!![emoji30][emoji30][emoji30][emoji30]
 
Kilimo cha mdomo rahis kweli sio cha shambani. Ukodishe shamba kama huna, utafute vibarua, ununue mbegu, mbolea hii inayopanda kila siku, madawa, sumu za wadudu, booster. Hapo bado hujaibiwa
Wao wanaweza izo gharama lakini hawawapi mitaji ya kilimo watoto wao,ni connection tu kwenye mataasisi ,NIMETUKANA TUSI KUBWA ATA HALIANDIKIKI
 
wasomi wa Tanzania na Africa kwa ujumla ni wasomi makanjanja.
hawajawai kuwa na msaada wowote ule isipokuwa wizi pale wanapoaminiwa katika position yoyote.
ukiondoa kundi la waasia na waarabu uchumi wa Tanzania unajengwa na ngumbalu.
ngumbalu ndiyo wazawa pekee waliojitwika jukumu la kujenga uchumi uku wasomi makanjanja wakibakia kulialia tu na kujiingiza kwenye siasa ili kupata teuzi..
 
Njoo Iringa nikupe shamba heka 5 ulime mwaka mzima halafu uje ulete mrejesho hapa.

Kilimo kinahitaji uvumilivu, mtaji na ukishavuna bei ya mazao yako anapanga dalali au serikali.

Njoo ulime. Ni rahisi sana kuongea ukiwa umeshiba umekaa sebuleni kwako nakuona watu wengine wote wavivu.

Kama Kilimo kinalipa Mbeya, Iringa, Ruvuma na Njombe zisingekuwa na maskini.

NB: bei ya mfuko mmoja wa mbolea ni 120,000.
Tena wewe wa Iringa unahitaju kuchapwa viboko kabisa. Huko kuna utajiri ambao uko wazi wazi kabisa. .
1. Maparachichi yanahitaji mbolea?
2. Miti inahitaji mbolea?
3. Viazi vya chips vinahitaji mbolea?

Vyote hivi vinastawi Iringa lkn wasomi wanabakia kulalama tu.
 
Mkuu Hawa wasomi wana laptops za laki 7 mpk milioni 1, wengine wana simu janja za laki 3 mpk milioni. Yote hii ni mitaji tosha kabisa kwa kilimo. Sema Kuna kasumba miongoni mwa wasomi kwamba kilimo ni kwa ajili ya wasiosoma.

Watapata tabu Sana wasipobadilika.
Hujui kilimo mkuu kaa kimya nayo ni busara
 
Tunaofanya miradi ya kilimo tuna cheeka tukiona asiyejua mambo ya shambani anavyo ongea kirahi rahisi tu.
Nililima mahindi kisha akaja myonyaji mmoja anasema nimuuzie mabichi 150/- kwa indi moja nikamtimua sasa nakula ugali mweyewe na kulisha kuku.
acha tu mkuu Unakuta unaona kaz rahis tu lakn ingia uone mzik wake
 
Tena wewe wa Iringa unahitaju kuchapwa viboko kabisa. Huko kuna utajiri ambao uko wazi wazi kabisa. .
1. Maparachichi yanahitaji mbolea?
2. Miti inahitaji mbolea?
3. Viazi vya chips vinahitaji mbolea?

Vyote hivi vinastawi Iringa lkn wasomi wanabakia kulalama tu.
Parachichi halihitaji mbolea?
Unajua bei ya shamba la miti na hadi uje uvune inachukua miaka kumi a ngapi?
Be serious tajiri.
Yaani mtu huna hata hela ya kula unaenda kununua shamba la miti? Bora hata parachichi kuna hii ya miaka 3. Na uwe na mtaji sio mtu katoka chuo na laki mbili ya boom unamwambia nunua shamba la miti wakati hiyo hata akilima mahindi itaishia kwenye mbolea tu.
 
Sio Tu muajiriwa ata watoto zao wanawapa connection ndani ya taasisi majina yanajirudia tu!!!![emoji30][emoji30][emoji30][emoji30]
Mimi nalima mkuu. Nina shamba la maparachichi ekari 2 kule KK Tukuyu
Nina shamba la michikichi ekari 4 Tabora (siyo Kigoma). Nilisikia kwenye redio nikazitumia hizi fursa.

Muda mwingi napiga mishe yangu Katavi. Nalima mpunga na ninauza pia.

Jamani jitumeni. Ajira hakuna.
Siyo lazima ulime ulipo zaliwa.
 
Mleta uzi umeongea kinadhalia bila kujenga hoja za msingi ie kilimo ni biashara Kama zilivyo biashara nyingine, umesema ardhi ipo tele lakini usichojua hiyo ardhi sio bure je huyu kijana pesa anapata wapi kununua hiyo ardhi?
Umeongea kujiajiri kwenye kilimo kama kwenda kunya yaani unaenda chooni unakata gogo unatoka, Dada kilimo hakiko hivyo labda unaongea kwa kuwananga vijana wasio na ajira lakini sio kuwasaidia, kilimo ni mchakato sio kama unavyowaza wewe mfano Mimi nilipata pesa kidogo kwa kusikiliza watu kama wewe nikasema ngoja nilime nikatumia kama 2m kulima alizeti nje ya muda nikambulia 7k nikawa nimekula loss ya 1.3 hivyo ukiwa unawananga vijana uwe practical sio umekaa kwenye key board unaandika tu na hapo nimetoa uzoefu wangu Mimi nilikua na mtaji je wale wasiokua na mtaji hali ni mbaya
Wewe hauna tofauti na ma inspirational speaker wengine unahifanye ku inspire kumbe ni mbinu yenu ya kuwageuza vijana mtaji
 
Mimi nilipata pesa kidogo kwa kusikiliza watu kama wewe nikasema ngoja nilime nikatumia kama 2m kulima alizeti nje ya muda nikambulia 7k nikawa nimekula loss ya 1.3
Itakuwa hukuwa na muda wa kukisimamia kilimo. Ulilima kwa remote (maagizo mengi).

Nakubaliana nawe. Hata hivyo Kuna watu kibao wanaendesha maisha yao kwa kilimo. Wewe ulienda kubeep, na kilimo ukikibeep kinakupigia
 
Parachichi halihitaji mbolea?
Unajua bei ya shamba la miti na hadi uje uvune inachukua miaka kumi a ngapi?
Be serious tajiri.
Yaani mtu huna hata hela ya kula unaenda kununua shamba la miti? Bora hata parachichi kuna hii ya miaka 3. Na uwe na mtaji sio mtu katoka chuo na laki mbili ya boom unamwambia nunua shamba la miti wakati hiyo hata akilima mahindi itaishia kwenye mbolea tu.
Mkuu kwenye miti siyo lazima upate hela kwenye kuuza mti. Kuna biashara ya vitaku vyw miti mkuu inalipa kinyama. Tatizo mnapambana kunishinda kwa kuonesha kwamba kilimo hakifai. Kinafaa wakubwa changamkieni kilimo ila mkipende
 
Mimi nalima mkuu. Nina shamba la maparachichi ekari 2 kule KK Tukuyu
Nina shamba la michikichi ekari 4 Tabora (siyo Kigoma). Nilisikia kwenye redio nikazitumia hizi fursa.

Muda mwingi napiga mishe yangu Katavi. Nalima mpunga na ninauza pia.

Jamani jitumeni. Ajira hakuna.
Siyo lazima ulime ulipo zaliwa.
Hilo shamba la parachichi umeridhi au umeanzisha wewe, Kama umeanzisha wewe umetumia mtaji kiasi gani the same to michikichi na mpunga halafu angalia ni vijana wangapi wanaweza ku afford hizo gharama
Ninachotaka kusema inawezekana vijana wanatamani au wanaweza kufanya hizo jitihada lakini hawana nyenzo muhimu kama ulizonazo wewe
 
Tatizo mnataka mkiwnzq tu mtoke na hela ndefu. Kubali kupata hasara hata miaka 3 wakati unajifunza
Ukiwa na mtaji wa kuanzia na kujaribu tena unakuwa na kiburi cha kusema haya unayosema.
Fresh graduate atatoa wapi pesa ya majaribio yote hayo?
Anaishi vipi muda wote wa majaribio? Yaani anakuka nini, anapataje matibabu na anavaa nini?

Pia ukiwa na watu wa kukubeba inawezekana usemayo.
 
Itakuwa hukuwa na muda wa kukisimamia kilimo. Ulilima kwa remote (maagizo mengi).

Nakubaliana nawe. Hata hivyo Kuna watu kibao wanaendesha maisha yao kwa kilimo. Wewe ulienda kubeep, na kilimo ukikibeep kinakupigia
Nimelima nikiwa hapohapo na ni mashamba ya nyumbani sikukodi hizo hela nilitumia kwenye mbegu,vibarua usafiri na vitu vingine inshort nilitamani nifanye kilimo ful time job bila kuadhiriwa lakini niliangukia pua Sasa kuna vijana wangapi wamekata tamaa katika mazingira Kama hayo
 
Back
Top Bottom