Aina 7 Za Simu Kali Kuliko Iphones, Pixels na Samsung Ila HAzijulikani sana Tanzania

Aina 7 Za Simu Kali Kuliko Iphones, Pixels na Samsung Ila HAzijulikani sana Tanzania

Sasa velvet si midrange izo ungeenda na level za hizo S26
Mimi pia nmetumia zote Samsung ni best lakini ukicompare price durability na technology basi baadhi ya brand znashindana nae vizuri sana
Mkuu mimi kwa Samsung wamenivutia ktk mambo mawili au matatu

1. One UI yao ni nzuri sana saana, sijaona simu ya Android yenye customazation bora na feautures bora kama Samsung.

2. App za Samsung zenyewe ni premium kama app za iphone. Watumiaji wa Iphone wananielewa nikisema ubora wa Apps za Iphone.

3. Kwenye hardware, KIOO cha Samsung ni balaa saaaana.
 
Kumbe Kila simu ktk hizi zinazosifiwa zinazidiana kwenye Eneo moja ama jingine, there is no answer ideal phone that fits all features
Sasa mkuu tukisema nani yupo best at least kwa kila angle hapo ndipo SAMSUNG anaibuka kuwa bingwa. Ana Display kali, ana Camera kali sana siku hizi ukicompare na Pixel na Iphone na kwa picha tu anaweza akawakalisha ila kwa video na sound iphone ni KING.

Kwa software, Samsung ndie aliyeiboresha na kuwekeza saaana Android yake (ONE UI) kwa kiasi kikubwa kuliko wapinzani wake. Kumbuka hapa tunazungumzia Samsung flagships na sio hizi A series sijui A07, A23 nk
 
Mkuu mimi kwa Samsung wamenivutia ktk mambo mawili au matatu

1. One UI yao ni nzuri sana saana, sijaona simu ya Android yenye customazation bora na feautures bora kama Samsung.

2. App za Samsung zenyewe ni premium kama app za iphone. Watumiaji wa Iphone wananielewa nikisema ubora wa Apps za Iphone.

3. Kwenye hardware, KIOO cha Samsung ni balaa saaaana.
Kiuhalisia hii 2026 Samsung (S series) ndio simu zilizokamilika kuliko simu zote duniani. Hakuna simu zipo full package kama Samsung.
iPhone pia zimekamilika asilimia kubwa except iOS ipo limited kuliko Android kwenye mambo ya kuaccess third party applications na customization
Oppo, vivo, Honor na Xiaomi wanatengeneza more capable phones kuliko Motorola.

Nokia ilishakufa sasahivi wamezibadili jina zinaitwa HMD, HMD wanaboronga tu, hamna kitu pale

Google Pixel sio full package kama Apple, Samsung, Xiaomi, vivo, Honor na Oppo kutokana na kutumia processor zao za Google Tensor wakati wenzao wana Snapdragon lakini wanajitahidi kwenye Camera, AI enhancement kwenye telephoto shots, clean Android experience, design na simplicity

Tecno na Infinix wako busy na midrange na low end. Huko juu hata hawana mpango nako, wana soko lao wanalitarget hilohili so usitegemee Tecno au Infinix kutoa simu za kushindana na Samsung Galaxy S26 Ultra, Xiaomi 17 Ultra au Oppo Find X9 Ultra

Sony simu nzao ni nzuri ila ni expensive, hazijafikia Samsung, Apple, Xiaomi, Oppo na vivo lakini hazijaachwa nyuma kihivyo. Ziko better kuliko Pixel kwenye chipset na Pixel zinazidi Sony kwa camera na AI. Sony wanaweka 3.5mm jack na SD slot kwenye flagship zao
 
Kuna jamaa hapo juu nilikuwa nabishana nae kuhusu oppo nimeamua nimuache tu kwa kweli.
Huwezi kutumia vi oppo vya 2015 mlivyojaza huko madukani kwenu kama benchmark ya simu za Oppo, watu walishatoka huko

Wabongo wengi dunia imewaacha sana, hamuelewi flagship zilipofikia hii 2026 kwa hiyo hata sishangai
 
Haya sawa.
 
Nilitaka kumjibu jamaa hapo kwamba Motorolla hasa ile g60 sijui 60 pro ni simu kali saaana, iko very smoothly, naweza sema sijaona ona simu yenye touch na scrolling laini kama ile. Display kali mno, Pixel hana simu inayofika ile level. Pixel tunampa heshima yake kubwa kwa picha za mchana na usiku wakati wa giza.
👍
 
Nadhani unaongelea Motorola Edge 60 Pro, hii ni midrange sio flagship. Inatumia MediaTek Dimensity 8350 Extreme. And while sipingi, ni midrange nzuri sana lakini hapa nilikuwa naongelea flagships. Yani simu za juu za kampuni
Kama ukichukua Motorola ya juu zaidi na Oppo ya juu zaidi, Oppo ni better
Pia Motorola kuzidi Pixel sio kitu cha ajabu ukizingatia Motorola anatumia superior chipsets za Snapdragon ambazo ni bora kuliko Google Tensor za Pixel. Lakini pia Pixel zinazidi Motorola in Camera and AI
 
Jamaa niko sokoni muda mrefu nisielewe vipi!
Ona tena unarudia kutamka oppo!
Kaka ninazo oppo hata kuingia whatsapp tu mtihani..
shida yako unatumia oppo za dubai famba sio oppo original zenyewe usibishie ..... hizo oppo ambazo unasemea wewe hata hazitambuliki na oopo wenyewe hahaahaha

hapa dukani sina oppo ya chini ya milioni ..... ko wewe najua unazungumzia oppo za laki 1 moja zile mzee
 
Sasa bwana baraka John huu Uzi mbona kama umelenga matajiri tu wa JF,sisi hoe hae pangu pakavu usitutenge tutajie na simu za laki 3 kushuka chini zenye camera Kali maana sisi watu wa daraja la chini kati tunaangalia camera Kali Cha kwanza na bei iwe nafuu,tupe ufafanuzi wa simu hizo.Naandika kama mbunge wa wananchi wa daraja la chini kati
 
Back
Top Bottom