Aina ya maisha kwa vijana wa Arusha tunahitaji mjadala wa kitaifa

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Kuna clip zinatembea zikionesha vijana wa mkoa wa Arusha wakiwa mochwari kwaajili ya kuchukua mwili wa mwenzao aliyefariki kwa ajali ya pikipiki.

Namna ya maisha ya vijana wa Arusha wanavyoishi, kuvaa, kuongea, ku-behave nafikiri tunahitaji mjadala wa kitaifa. Yaani wanafanya mambo ya kizamani wenyewe wakiona ni ujanja.

Kama taifa tunakuwa na vijana wa namna gani? Wanaongea vibaya, wanavaa hovyo, heshima kwao sio kipaumbele yaani ni vurugu tupu.

 
😁😁😁😁
Ila binafsi yangu ukiacha kuvuka mipaka yao Ila napenda vile walivyo na identity yao lakini pia wanavyopakubali arachuga. I wish watanzania tungekuwa na hiki kitu maana sidhani kama tuna kitu kinachotutambulisha kiutamaduni kama wenzetu wa Nigeria, South Africa au Rwanda.

Na msiseme wamasai maana wakenya washajitambulisha nao kitambo maana hata bendera yao ina ngao ya kimasai
 
Ni bahati nzuri tu hii nchi serikali ya ccm wanaidhibiti kikamilifu kiusalama la sivyo tungekuwa na serikali legelege kwenye usalama huu mkoa unaweza kutoa hata kikundi cha uasi kwa aina ya vijana waliopo ni vijana wa hovyo kuliko maelezo vijana wasiojijali kwao maisha hayana thamani sababu bange na visungura ndio kila kitu kwao na maisha ya kuigaiga upumbavu.
 
Mmoj juzi anasema yeye alishakufaa siku nyingiii ule ni mwilii tuu so haogopi kifo wala kitu yoyotee yanii....nadhani kama huyo hapoo sijui kama yupo hai kifikra wala mawazooo...bhangiiiii kunakuchaa mpaka usiku.
 
si bora hivyo kuliko vijana wa dar wanaokulana wao kwa wao.....

najua nimeandika ujinga hapo ila dhumuni langu ni kuonesha ubaya kwa kujumuisha mambo.... sio wote wako hivyo, ingekua wote wako hivyo basi arusha isingekua jiji
 
Naomba kuelimishwa clip ni Nini?!
 
masela mavi na ujanja kuiga ila wengi mafala sana na kitambo fulani kabla akina Joe makini, Shindoman na JCB hawajatoka kimziki walikuwa wanatukubali sana wadarisalama na wengi ndoto yao ilikuwa kuja Darisalama.

Vilikuwa vinakujaga kuchana pale crystal na trip A, ila vilikuwa vikuwaadi vizuri sana kwasisi wadarisalaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…