Business Model ya ATCL ni ya ajabu kidogo.
Naona tayari wana route ya kwenda Lusaka (Zambia ) na pia Harare (Zimbabwe).
Na route ya Dar kwenda Nairobi Kenya. Hii wamefanikiwa maana wana route mbili za ndege kutoka Dar kwenda Nairobi (nne kwa siku kati ya Dar na Nairobi)
Hizi ndio route pekee wanazoweza kuzimudu kibiashara.
Kwa route ya Dar kwenda Capetown huko tayari kuna Kenya Airways na Ethopian Airlines ; hao hatuwezi kupambana nao, hivyo tusahau kuhusu hiyo route.
Tena hapo Ethopian Airlines ina route ya kibabe sana kama umewahi kusafiri kutoka Bole kwenda Capetown kisha inatoka Capetown inapita Dar; hii maana yake ni kwamba abiria aliyeko Tanzania anapotaka kwenda South Afrika inabidi abebwe na Ethiopian Airlines mpaka Addis Ababa kisha anapanda tena Ethiopian Airlines kwenda Capetown.
Hii route inawapa wateja wengi haswa watalii kutoka South wanaokuja Tanzania.
Utaniuliza vipi kuhusu route ya Dar kwenda Maputo Msumbiji?
Hii route nayo Ethiopian AIRLINES imekaba haswa maana ana ndege inayopita Dar kwenda Blantayre (Chieka) pale Malawi kisha inapita Maputo (Msumbiji) na kwenda Johanesburg (Afrika Kusini ).
Bado unaweza kuniuliza vipi kuhusu Dar - kwenda Kigali kwa Kagame;
Hii route tayari Rwanda Air na Kenya Airways wamejiimalisha vya kutosha; hivyo ni ngumu kwa ATCL na Twiga wa Tanzania kuweka mguu hapo.
Unaweza kusema vipi kuhusu Bujumbura kwa Warundi;
Hii route ni kugombania goli, najua ATCL ina route japo inaenda mara chache huko. Hii route yupo Kenya Airways na mara kadhaa nimeiona Precision pia kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura (BJB). Lakini pia Hahn Air pia wana route hapo. Kwa hiyo sioni kama kuna soko la uhakika kwa ATCL.
Tumebakisha wapi; oooh Dar - kwenda Kinshasa (FIH)
Huku napo Ethiopian Airlines imetawala soko, kama ni Mtanzania na upo Kinshasa basi itakubidi upande Ethiopian Airlines; hawa jamaa wana route kutoka Bole (Addis Ababa) kisha inapita Dar na kwenda Kinshasa, hivyo hapo napo ni pagumu.
Ni kweli kuna abiria wengi huko Capetown na Johannesburg lakini ukweli ni kwamba soko lina wenyewe tayari. Tena waliopo sio wadogo ni wabobevu, wana uwezo mkubwa wa kibiashara na wanatoa nafasi ya kuunganisha route za ndege kuliko Air Tanzania.
Kwa mfano kama upo Capetown na unaenda Dubai, ni rahisi kushawishiwa kupanda Ethiopian Airline ambayo itapita Dar na kisha kwenda kukuacha Bore na ukaunga na Ethiopian nyingine inayokwenda Dubai kuliko kupanda Air Tanzania itakayokuacha Dar au KIA usijue pa kwenda.
Kwa wenye uzoefu na masuala haya ya biashara na route za ndege watakubaliana nami kuwa, inawezekana kabisa kuwa hatuwaza vizuri wakati tunanunua ndege kwa soko la kimataifa.
ATCL ina nafasi kubwa kwa soko la ndani; iwapo wataamua kuweka bei rafiki, wanaweza wasifike urahis wa bei za Fast Jet lakini wakishusha kidogo watakuwa na biashara nzuri sana. Ukiacha changamoto ndogondogo hapa wanajitahidi.
Kuna baadhi ya route ndege mara kadhaa huwa zinarudi zikiwa na nafasi za wazi sana , nina uzoefu na route ya Mbeya kuja Dar na ile Kigoma - Dar. Nadhani wakiangalia gharama inaweza kuwasaidia kupata abiria na route zaidi.
Soko la biashara kwa upande huu wa kusini Wahabeshi (Ethiopian Airline) wamelishika haswa.
ATCL wana malzia kulipa madeni ili waweze fanya biashara vyema...
pia kuna mikataba ktk baadhi ya njia huwa wana ingia, kwa mfano KQ na hao wa sauzi... hata ATCL wapo na wana taka kuweka alliance ktk baadhi ya njia...
Biashara si vile unavyo iona kwa nje na kuifikiria, pia ni namna ya kupata faida kwa kushirikiana na mshindani au kwa kwenda mwenyewe...
KQ, Ethiopian... wana mashirikiano na ndege za ulaya kwa kuwa pelekea wateja na wao wana waletea wateja ktk baadhi ya njia...
hivyo msikilize Ndg Matindi atakwambia jinsi walivyo jipanga kuona wapi wanapo elekea...
nenda youtube kaangalie mahojiano yake ya mwaka huu na azam tv itakusaidia mkuu...
===================================================================================================
Hayo yamezungumzwa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, wakati akizungumza na menejimenti ya ATCL, na kusisisitiza kwamba pamoja na maboresho yanayofanyika kwa sasa Shirika linakamilisha mpango biashara wa muda mrefu ili kuhakikisha ATCL inajiendesha kwa faida pamoja na kulipa madeni yaliyopo.
“Serikali imeendelea kuwekeza kwenye Shirika hili na niwahakikishie maboresho ya viwanja vya ndege nchini yatachochea kwa kiasi kikubwa ongezeko la mapato na hatimaye madeni yanayoripotiwa yatalipwa", amesisitiza Dkt. Possi.
Aidha, Dkt Possi ameipongeza Menejimenti ya ATCL kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwataka kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazokabili Shirika hilo ikiwemo mabadiliko ya ratiba yanaripotiwa mapema kwa abiria ili kuwafanya abiria kuendelea kuliamini na kutumia Shirika hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Eng. Ladislaus Matindi, amemuhakikishia Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa Shirika linaendelea kuboresha utendaji na huduma ili likue na kuendelea kuaminika kwa utoaji huduma bora kwa zaidi ya vituo 15 vya ndani ya nchi na zaidi ya vituo sita vya nje ya nchi inavyovihudumia.
Eng. Matindi ameongeza kuwa kwa mwaka huu Shirika linakamilisha mazungumzo na mashirika makubwa ya ndege kama KLM na Emirates ili kuboresha huduma pale itakapoanza safari zake kwa vituo vya Uingereza na maeneo mengine kimataifa.
“Tayari tunashirikiano na mashirika makubwa ya ndege kama Air India ambao wanachukua abiria wetu tunaowapeleka Mumbai kuwapeleka kwenye maeneo mengine, lakini kwa sasa tunakamilisha mazungumzo na KLM na Emirate ili kuboresha huduma pale tutakapoanza safari za Uingereza na maeneo mengine", amefafanua Eng. Matindi.
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa sasa ina ndege 11 ambazo ni Boeing 787 ndege mbili, A220-330 ndege nne, Dash 8-Q400 ndege tano na tayari Serikali inaendelea na manunuzi ya ndege nyingine tano ambazo zinatajiwa kuanza kuwasili nchini mwaka 2023