Sijui kama unajua chochote kuhusu ATCL au hii sekta ya usafirisha wa anga.
Labda nikueleze
i. ATCL ina deni la TZS 45 billion (USD19.4 million)
ii. ATCL imepata hasara ya TZS150 billion Tanzanian shilling (USD64.6 million) ndani ya miaka mitano.
Hayo madeni wanamalizia kulipa wakati hata hawajaanza kuyalipa?
Umeelezwa vizuri hapo na mtu anayejua kuhusu hizo route, huna mkataba wa kuingia na mtu ambaye ana uwezo wa kumtoa abiria South Africa, Mozambique, Malawi, Shelisheli au DRC. Unaingia naye mkataba ili umsaidie wapi?
ATCL inachoweza kufanya ni kumtoa abiria Songwe ili imlete Dar apande ndege ya kwenda sehemu nyingine duniani.
Mashirika ambayo Ethiopian wana ushirka nayo ni zaidi ya 100 unaweza kupita hapa kwenye official website badala ya kuchukua taarifa youtube
Interline and Partners Baggage Policy
Kuhusu Engineer Mantindi, ana uwezo mzuri wa management lakini hali ya soko kwa ATCL ni gumu sana. Anaongea kufurahisha wanasiasa tu.
Rudi nyuma angalia mipango ya ATCL tangu 2017 embu niambie wametimiza lipi?
Huwezi kujadili hoja kubwa kama hii kwa kusikiliza mahojiano.....
Mahojiano hayajawahi kubadili chochote katika nchi hii
Nikupe orodha ndogo kuhusu mahojiano yaliyojaa youtube ambayo yaliishia kuwa mahojiano tu.....
1. Professa Muhongo - alizungumza kuhusu Gas ya mtwara - Alisema ''baada ya uchumbaji kukamilika, bei ya umeme itashuka, umeme utakuwa wa kutosha na tutatuza nchi za jirani, akaendelea kusema '' gesi ya majumbani itasambazwa kwa kila nyumba''......
lipi limetimia hapo?
2. Mahojiano ya Kadogosa kuhusu SGR - watu wataanza kusafiri kwa treni ya mwendo kasi kwenda Morogoro mwishoni kwa 2021......vipi safari zimeshaanza ?
3. Mahojiano na kauli za Magu - ''Hii nchi tajiri sana, tembeeni vifua mbele''....vipi unatembea kifua mbele?
4. Mahojiano ya Mzee wa Msoga wakati wa kampeni mwaka 2000- Alisema katika miaka mitano ya utawala wake kila mtanzania atakuwa na maisha bora.....Unakumba ''Maisha bora kwa kila Mtanzania'' ,,,,,vipi una maisha bora?