Business Model ya ATCL ni ya ajabu kidogo.
Naona tayari wana route ya kwenda Lusaka (Zambia ) na pia Harare (Zimbabwe).
Na route ya Dar kwenda Nairobi Kenya. Hii wamefanikiwa maana wana route mbili za ndege kutoka Dar kwenda Nairobi (nne kwa siku kati ya Dar na Nairobi)
Hizi ndio route pekee wanazoweza kuzimudu kibiashara.
Kwa route ya Dar kwenda Capetown huko tayari kuna Kenya Airways na Ethopian Airlines ; hao hatuwezi kupambana nao, hivyo tusahau kuhusu hiyo route.
Tena hapo Ethopian Airlines ina route ya kibabe sana kama umewahi kusafiri kutoka Bole kwenda Capetown kisha inatoka Capetown inapita Dar; hii maana yake ni kwamba abiria aliyeko Tanzania anapotaka kwenda South Afrika inabidi abebwe na Ethiopian Airlines mpaka Addis Ababa kisha anapanda tena Ethiopian Airlines kwenda Capetown.
Hii route inawapa wateja wengi haswa watalii kutoka South wanaokuja Tanzania.
Utaniuliza vipi kuhusu route ya Dar kwenda Maputo Msumbiji?
Hii route nayo Ethiopian AIRLINES imekaba haswa maana ana ndege inayopita Dar kwenda Blantayre (Chieka) pale Malawi kisha inapita Maputo (Msumbiji) na kwenda Johanesburg (Afrika Kusini ).
Bado unaweza kuniuliza vipi kuhusu Dar - kwenda Kigali kwa Kagame;
Hii route tayari Rwanda Air na Kenya Airways wamejiimalisha vya kutosha; hivyo ni ngumu kwa ATCL na Twiga wa Tanzania kuweka mguu hapo.
Unaweza kusema vipi kuhusu Bujumbura kwa Warundi;
Hii route ni kugombania goli, najua ATCL ina route japo inaenda mara chache huko. Hii route yupo Kenya Airways na mara kadhaa nimeiona Precision pia kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura (BJB). Lakini pia Hahn Air pia wana route hapo. Kwa hiyo sioni kama kuna soko la uhakika kwa ATCL.
Tumebakisha wapi; oooh Dar - kwenda Kinshasa (FIH)
Huku napo Ethiopian Airlines imetawala soko, kama ni Mtanzania na upo Kinshasa basi itakubidi upande Ethiopian Airlines; hawa jamaa wana route kutoka Bole (Addis Ababa) kisha inapita Dar na kwenda Kinshasa, hivyo hapo napo ni pagumu.
Ni kweli kuna abiria wengi huko Capetown na Johannesburg lakini ukweli ni kwamba soko lina wenyewe tayari. Tena waliopo sio wadogo ni wabobevu, wana uwezo mkubwa wa kibiashara na wanatoa nafasi ya kuunganisha route za ndege kuliko Air Tanzania.
Kwa mfano kama upo Capetown na unaenda Dubai, ni rahisi kushawishiwa kupanda Ethiopian Airline ambayo itapita Dar na kisha kwenda kukuacha Bore na ukaunga na Ethiopian nyingine inayokwenda Dubai kuliko kupanda Air Tanzania itakayokuacha Dar au KIA usijue pa kwenda.
Kwa wenye uzoefu na masuala haya ya biashara na route za ndege watakubaliana nami kuwa, inawezekana kabisa kuwa hatuwaza vizuri wakati tunanunua ndege kwa soko la kimataifa.
ATCL ina nafasi kubwa kwa soko la ndani; iwapo wataamua kuweka bei rafiki, wanaweza wasifike urahis wa bei za Fast Jet lakini wakishusha kidogo watakuwa na biashara nzuri sana. Ukiacha changamoto ndogondogo hapa wanajitahidi.
Kuna baadhi ya route ndege mara kadhaa huwa zinarudi zikiwa na nafasi za wazi sana , nina uzoefu na route ya Mbeya kuja Dar na ile Kigoma - Dar. Nadhani wakiangalia gharama inaweza kuwasaidia kupata abiria na route zaidi.
Soko la biashara kwa upande huu wa kusini Wahabeshi (Ethiopian Airline) wamelishika haswa.