Air Tanzania, Soko la Afrika Kusini, Abiria ni wengi ajabu!

Air Tanzania, Soko la Afrika Kusini, Abiria ni wengi ajabu!

Business Model ya ATCL ni ya ajabu kidogo.

Naona tayari wana route ya kwenda Lusaka (Zambia ) na pia Harare (Zimbabwe).

Na route ya Dar kwenda Nairobi Kenya. Hii wamefanikiwa maana wana route mbili za ndege kutoka Dar kwenda Nairobi (nne kwa siku kati ya Dar na Nairobi)

Hizi ndio route pekee wanazoweza kuzimudu kibiashara.

Kwa route ya Dar kwenda Capetown huko tayari kuna Kenya Airways na Ethopian Airlines ; hao hatuwezi kupambana nao, hivyo tusahau kuhusu hiyo route.

Tena hapo Ethopian Airlines ina route ya kibabe sana kama umewahi kusafiri kutoka Bole kwenda Capetown kisha inatoka Capetown inapita Dar; hii maana yake ni kwamba abiria aliyeko Tanzania anapotaka kwenda South Afrika inabidi abebwe na Ethiopian Airlines mpaka Addis Ababa kisha anapanda tena Ethiopian Airlines kwenda Capetown.
Hii route inawapa wateja wengi haswa watalii kutoka South wanaokuja Tanzania.

Utaniuliza vipi kuhusu route ya Dar kwenda Maputo Msumbiji?
Hii route nayo Ethiopian AIRLINES imekaba haswa maana ana ndege inayopita Dar kwenda Blantayre (Chieka) pale Malawi kisha inapita Maputo (Msumbiji) na kwenda Johanesburg (Afrika Kusini ).

Bado unaweza kuniuliza vipi kuhusu Dar - kwenda Kigali kwa Kagame;
Hii route tayari Rwanda Air na Kenya Airways wamejiimalisha vya kutosha; hivyo ni ngumu kwa ATCL na Twiga wa Tanzania kuweka mguu hapo.

Unaweza kusema vipi kuhusu Bujumbura kwa Warundi;
Hii route ni kugombania goli, najua ATCL ina route japo inaenda mara chache huko. Hii route yupo Kenya Airways na mara kadhaa nimeiona Precision pia kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura (BJB). Lakini pia Hahn Air pia wana route hapo. Kwa hiyo sioni kama kuna soko la uhakika kwa ATCL.

Tumebakisha wapi; oooh Dar - kwenda Kinshasa (FIH)
Huku napo Ethiopian Airlines imetawala soko, kama ni Mtanzania na upo Kinshasa basi itakubidi upande Ethiopian Airlines; hawa jamaa wana route kutoka Bole (Addis Ababa) kisha inapita Dar na kwenda Kinshasa, hivyo hapo napo ni pagumu.

Ni kweli kuna abiria wengi huko Capetown na Johannesburg lakini ukweli ni kwamba soko lina wenyewe tayari. Tena waliopo sio wadogo ni wabobevu, wana uwezo mkubwa wa kibiashara na wanatoa nafasi ya kuunganisha route za ndege kuliko Air Tanzania.

Kwa mfano kama upo Capetown na unaenda Dubai, ni rahisi kushawishiwa kupanda Ethiopian Airline ambayo itapita Dar na kisha kwenda kukuacha Bore na ukaunga na Ethiopian nyingine inayokwenda Dubai kuliko kupanda Air Tanzania itakayokuacha Dar au KIA usijue pa kwenda.

Kwa wenye uzoefu na masuala haya ya biashara na route za ndege watakubaliana nami kuwa, inawezekana kabisa kuwa hatuwaza vizuri wakati tunanunua ndege kwa soko la kimataifa.

ATCL ina nafasi kubwa kwa soko la ndani; iwapo wataamua kuweka bei rafiki, wanaweza wasifike urahis wa bei za Fast Jet lakini wakishusha kidogo watakuwa na biashara nzuri sana. Ukiacha changamoto ndogondogo hapa wanajitahidi.

Kuna baadhi ya route ndege mara kadhaa huwa zinarudi zikiwa na nafasi za wazi sana , nina uzoefu na route ya Mbeya kuja Dar na ile Kigoma - Dar. Nadhani wakiangalia gharama inaweza kuwasaidia kupata abiria na route zaidi.

Soko la biashara kwa upande huu wa kusini Wahabeshi (Ethiopian Airline) wamelishika haswa.
Sijawahi kuona mtu mchawi kama wewe katika hii dunia... umejawa na roho ya kushindwa iliyopitiliza.... uogo na unafiki mkubwa.... mtu aliyekata tamaa ni hatari sana kwa usalama wa taifa.... wew badala ya kushaur njia bora ambazo ATCL na Serikali yetu inatakiwa kufanya ili iweze kuweka ushindani kwenye soko, umekalia kukatisha watu tamaa.... yaani ningekuwa na mjegeje usingepona kbs mtu kama ili uache kupotosha jamii ya kiTanzania. Nenda ukaombewe au hosp ukatatibiwe kosaikolojia... mawazo ya kushindwa achana nayo kbs ndugu yangu... Nchi inatutegemea sana....
 
Naunga mkono hoja, tena it's about time ATC wa claim back our landing rights kutua London zilizokuwa zinashikiliwa na ATC, serikali ilipoingia ubia wa ATC na SAA kuanzisha Alliance Air, landing rights zetu za kutua London zilikabidhiwa kwa Alliance Air dege hilo likawa linatua London. Alliance Ilipokufa ilibidi tugawane fito, lakini kutokana na operating kwa hasara, SAA walitaifisha kila kitu including our landing rights za London.
P
SA kimewaka tayari Comair (Kulula.com+BA) chali. Njia nyeupe kwa ATC kuomba fifth freedom rights...tutue OR Tambo then CPT kisha Dar...from Dar tuongeze Dubai, Beijing, New York,JFK na London, Heathrow.
 
Air Tanzania changamkieni Soko la Afrika Kusini (Johannesburg na Cape Town) abiria Ni wa kuchota. Maana SAA imesitisha safari za kimataifa hivyo ni fursa kwa ATCL kwenda huko kama majirani zetu Kenya Airways, Ethiopian airlines na Rwandair.

View attachment 2246886View attachment 2246899
Kuna masuala yana sheria zake,kabla hujatoa maoni kwenye mambo hayo jifunze sheria zake
 
Internal routes zimewashida ku capitalize sembuse hizo za kimataifa ATCL hawawezi biashara ya ushindani,.......bora fast jet irudi tu angalau ilikua na ushindani mzuri
Fast Jet ilikuwa na ushindani mzuri, ilikuwa inashindana na nani?
 
Haya mambo makubwa huwa hayajadiliwi kwa video za YouTube.

ATCL haikuwa active kwa miaka mingi, huwezi kuingia na kushindana na hao, unatakiwa ianze taratibu kwa soko la ndani kwanza.

Biashara ya usafirishaji wa anga sio kama biashara ya Daladala Mbagala kwenda Kawe [emoji23][emoji23]
TZ kila mtu ni mpishi, kila mtu anajua kuelezea nadhari nyingi. ATCL walikuwa wamekufa kabisa kwa wingi wa madeni.

Haiwezekani wakaamka ghafla tu wakauweza ushindani wa Ethiopian Airline. Tukumbuke kuwa hizi siasa za kila mtu kutaka kuwa na sauti na maamuzi ndani ya shirika linaloongozwa kisomi ndio yalitufikisha hapa tulipo.

Matinyi na wasaidizi wake waachwe wafanye kazi ngumu ya kulifufua shirika.
 
Sijawahi kuona mtu mchawi kama wewe katika hii dunia... umejawa na roho ya kushindwa iliyopitiliza.... uogo na unafiki mkubwa.... mtu aliyekata tamaa ni hatari sana kwa usalama wa taifa.... wew badala ya kushaur njia bora ambazo ATCL na Serikali yetu inatakiwa kufanya ili iweze kuweka ushindani kwenye soko, umekalia kukatisha watu tamaa.... yaani ningekuwa na mjegeje usingepona kbs mtu kama ili uache kupotosha jamii ya kiTanzania. Nenda ukaombewe au hosp ukatatibiwe kosaikolojia... mawazo ya kushindwa achana nayo kbs ndugu yangu... Nchi inatutegemea sana....
Akili za kimaskini siku zote hazioni jema hata moja. Anachosahau ni kuwa ATCL na TCAA zinaongozwa na wasomi wenye uthubutu.

Madeni ya ATCL yanazidi kupungua siku baada ya siku na miaka michache ijayo faida itaanza kuonekana, Walioua shirika miaka ya nyuma wakaliacha hoi kwa madeni ni hawa hawa wanaoandika riwaya ndefu zilizojaa ujuaji usio na msaada kwa uendeshaji wa mashirika yetu.
 
ATC fursa umejileta yenyewe hiyoo
 
Route zetu za kusubiria waheshimiwa wacheleweshaji ndege, kimataifa wataweza!?!
Wabakie Tu na route ya Dodoma Mwanza Kilimanjaro Mbeya, na kule Mpanda sijui bado wanaenda!?
Hakuna kitu kinaniudhi kama hii issue ya kusubiria Waheshimiwa. Kuna siku tulichleweshwa Uwanja wa Ndege wa Dar kwa muda wa masaa 4, kisa kuna Mheshimiwa yupo kwa meeting anatakiwa apande hiyo ndege. Kuanzia wakati huo huwa sipandi ATCL napanda zangu Precision Air.
 
Hamna linaloshindikana ATCL wakiamua na wakipewa support na serikali. Kumbuka hao wote wanategemea kwa kiwango kikubwa abiria wanaotembelea Tanzania. Tanzania haina cha kupoteza kwa maamuzi yoyote itakayoamua katika hizo route.
ATCL ili wafanikiwe wanatakiwa wabadilishe mindset zao kwanza. Usafiri wa Ndege hauendeshwi kama Daladala ya Kariakoo - Buza kwa Lulenge!
 
Swali tu: hivi Air Tanzania wana strategic business planners wanaoangalia kila siku mabadiliko ya hali ya usafiri duniani kote? Sidhani! Route ya Dar-Cairo- Athens ingekuwa ni killer route. Nimesafiri lakini leg ya kutoka Cairo Athens ilikuwa fully booked kwa miezi miwili ijayo! Hakuna ndege!
 
Back
Top Bottom