Aisee, wanawake mtatunyoosha, hii clip imenifikirisha sana, naenda kupima DNA watoto wangu wote

Aisee, wanawake mtatunyoosha, hii clip imenifikirisha sana, naenda kupima DNA watoto wangu wote

Teslarati

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2019
Posts
2,621
Reaction score
10,466
Nisiseme mengi, kuna clip inazagaa mwanamke mmoja anajisifia kalea mtoto kwa kutumia baba watatu na hawajuani. Yaan anamaanisha mababa watatu wamelea na kuhudumia mtoto kila mmoja akijua huyo mtoto ni wake, mchezo mzima kacheza huyo mwanamke.

Najua hapo alikua anaigiza tu ila hio clip imenifikirisha sana sababu inaonekana inaakisi uhalisia. Hapa nikipata likizo ntafanya juu chini nipime DNA watoto wangu wote, wataalam toeni muongozo namna ya kupima DNA Tafadhari
 
Dna yenyewe mpaka south ndo zipo fresh huku bongo eti hawataki kuvunja ndoa za watu 🤣🤣🤣🤣 ama kweli ngoja nikue tu yaani 👿
Hii nadhan ilikua zamani, ukiwa na court order inawezekana ukapima.

Naenda mahakamani nawaambia nataka kuandika wosia hivo nataka kujua kina nani ni watoto wangu halali
 
Watakwambia wote wa kwako. Hata kama wakiwa wote sio wa kwako. Unahis serikal ndo inataka mzigo??
Uvivu wao tu, majibu ya ukweli yatoke halafu kama mwanamke kadanganya tunambana aseme baba ni nani, na huyo baba ndo anapelekewa mzigo. Ila mara nyingi wanawake wanajua mhusika ni nani, ni vile tu wanaamua kutuumiza
 
Serikali ina siasa kaka. Haiko tayari kuona the big effect. Inajua kwamba waweza m-abandon mke na watoto lets say wawili kisa imekwambia watt sio wako. Inajua fika watt wa mitaani na uhalifu vitaongezeka. So sio rahisi kupata majibu ya ukweli unless wewe ni kibopa wa gvt.
 
Nisiseme mengi, kuna clip inazagaa mwanamke mmoja anajisifia kalea mtoto kwa kutumia baba watatu na hawajuani. Yaan anamaanisha mababa watatu wamelea na kuhudumia mtoto kila mmoja akijua huyo mtoto ni wake, mchezo mzima kacheza huyo mwanamke.

Najua hapo alikua anaigiza tu ila hio clip imenifikirisha sana sababu inaonekana inaakisi uhalisia. Hapa nikipata likizo ntafanya juu chini nipime DNA watoto wangu wote, wataalam toeni muongozo namna ya kupima DNA Tafadhari

View attachment 2495130

💣💣💣💣💣
 
hawawezi na hawataweza kusema hivyo, nimesimamia DNA tatu tofauti na zote wanaume walipigwa na vitu vizito tena vizito kweli.
Haya sasa, tupe utaratibu chief. Unajua hamna kitu inauma kufikiria kama unakuja gundua mali zako anakula mtoto asie wako na mwanamke ambae kumbe alikua malaya tu kwako
 
Serikali ina siasa kaka. Haiko tayari kuona the big effect. Inajua kwamba waweza m-abandon mke na watoto lets say wawili kisa imekwambia watt sio wako. Inajua fika watt wa mitaani na uhalifu vitaongezeka. So sio rahisi kupata majibu ya ukweli unless wewe ni kibopa wa gvt.
Ghaii... kama hii ni kweli basi shida sana
 
Utaratibu ni rahisi kabisa, tafuta wakili (unaweza nitafuta mimi pia) kisha mtaenda ofisi za mkemia kanda kama hamuishi Dar es salaam.

Kule kwa mkemia mtapewa semina fupijuu ya swala zima la DNA, kisha mtachukuliwa sampuli zitakazohifadhiwa na kwenda kupimwa.

Hii michakato inahusisha watu tofauti tofauti hapo kwa mkemia hivyo kuchakachua sio rahisi kiasi hicho. Majibu ya DNA atapewa Wakili na yeye wakili ndio atakayekuja kuwapatia ninyi majibu ila hatawapa muondoke nayo sababu yeye ndiye mwenye dhamana ya kuyahifadhi (sio mali yenu)

MUHIMU KUFAHAMU:
1. Hautaweza kupima na kupatiwa majibu bila ama amri ya Mahakama au Wakili, ukienda wewe binafsi hutofanikiwa

2. Majibu ya DNA Testatapatiwa wakili wenu na yeye ndiye atakayewasomea na kubaki nayo ili ayahifadhi

3. Malipo ya kwa mkemia ni 100,000/= kwa kila sampuli malipo ya wakili itategemea na wakili husika akizingatia heria ya malipo ya mawakili.

Kama kuna swali nitajibu kulingana na uzoefu na ufahamu wangu.
 
Back
Top Bottom