Teslarati
JF-Expert Member
- Nov 21, 2019
- 2,621
- 10,466
- Thread starter
- #21
Aiseee.... Shukran sana chiefUtaratibu ni rahisi kabisa, tafuta wakili (unaweza nitafuta mimi pia) kisha mtaenda ofisi za mkemia kanda kama hamuishi Dar es salaam.
Kule kwa mkemia mtapewa semina fupijuu ya swala zima la DNA, kisha mtachukuliwa sampuli zitakazohifadhiwa na kwenda kupimwa.
Hii michakato inahusisha watu tofauti tofauti hapo kwa mkemia hivyo kuchakachua sio rahisi kiasi hicho. Majibu ya DNA atapewa Wakili na yeye wakili ndio atakayekuja kuwapatia ninyi majibu ila hatawapa muondoke nayo sababu yeye ndiye mwenye dhamana ya kuyahifadhi (sio mali yenu)
MUHIMU KUFAHAMU:
1. Hautaweza kupima na kupatiwa majibu bila ama amri ya Mahakama au Wakili, ukienda wewe binafsi hutofanikiwa
2. Majibu ya DNA Testatapatiwa wakili wenu na yeye ndiye atakayewasomea na kubaki nayo ili ayahifadhi
3. Malipo ya kwa mkemia ni 100,000/= kwa kila sampuli malipo ya wakili itategemea na wakili husika akizingatia heria ya malipo ya mawakili.
Kama kuna swali nitajibu kulingana na uzoefu na ufahamu wangu.
Sasa kwa nini majibu iwe ni mali ya wakili tena wakati kuanzia sampuli hadi malipo nafanya mimi? Na umesema wakili ndo anaewasomea wahusika majibu, je mimi sitaruhusiwa hata kuyaona ili kuhakikisha uhalali wake?