Ajabu na kweli: Padri wa kanisa katoliki kaoa mke na anavuta sigara kali!

Jiandae na mashambulizi kutoka kwa wanafunzi na waumini wao.... ila ukweli mchungu, mapadre wanaishi maisha ya kidunia mnoooo.
Kwa hiyo na sisi wa kidunia tukigombana na wake zetu tukawe mapadri au?

PADRI akikosea mnasema akaoe na sisi tulioa tukikosea tukawe mapadri au ?

Kwani mapadri walishushwa toka mbinguni? au wamezaliwa kama wewe na mwanadamu na wamekulia kwenye mazingira kama yako
 
Padre ni mwanadamu kama wewe si malaika. Sidhani kama inapaswa kushangaza mtafute Mungu tuache kutafuta watu au makanisa. Maisha ya mtu muachie mwenyewe na Mungu wake.
 
Ukistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.

Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.

Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.

MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.

ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.

Nawasilisha.
Zambi za Padre zinamhusu Padre huyo kwa Mungu wake. Dhambi anayoichuma Padre haina tofauti na mtu mwenye ndoa yake anapo date na changu doa au kimada.

Achana na Kanisa Talatifu Katoliki la Mitume.
 
Sishangai...wana mambo........
 
Hadi Leo hii unawaamini hao RC? Hao ni matapeli kama wengine ila Wacha wajinga ndio waendelee kuliwa maana haiwezekani wote tukawa wajanja.
 
Kuna padri mmoja aliniacha hoi kwa mshangao. Baada ya kumaliza misa kigangoni akaelekea kunywa pombe iliyokuwepo jirani, pombe yenyewe ni ya kienyeji. Baada ya kutoka kwenye pombe akabukia kiko mdomoni kisha akawasha gari yake kurudi parokiani. Mshangao ni kwamba inakuaje mtu wa Mungu atoke kwenye ibada na kukimbilia kunywa pombe kisha aongeze kilevi kingine cha tumbaku kwenye kiko na avute? Mungu gani huyo wa hovyo kuruhusu watumishi wake wawe walevi?
Ukristo ndio umeruhusu hata kanisani wanakunywa kabisa
 
Kwa hiyo na sisi wa kidunia tukigombana na wake zetu tukawe mapadri au?

PADRI akikosea mnasema akaoe na sisi tulioa tukikosea tukawe mapadri au ?

Kwani mapadri walishushwa toka mbinguni? au wamezaliwa kama wewe na mwanadamu na wamekulia kwenye mazingira kama yako
Ungeelewa maana ya Upadri kwanza ndio mada husika, suala la ubinadam na blah blah zingine hazipo kwenye mafundisho ya Upadri,
Wametaka kuishi maisha ya utawa bila shuruti sasa tukiona wanakengeuka lazima tushtuke na kuhoji.
 
KWANI MAPADRE SIKU HIZI WANAISHI KWAO? UONGO MTUPU MAPADRE WANAISHIPAROKIANI AU KWENYE NYUMZA ZA MAPADRE JAPO WAPO WENYE WATOTO ILA HUWEZI KUWAKUTA ETI WANAISHI NAO PAROKIANI HUO NI UONGO WA MCHANA KWEUPEEEEEE
 
Ukistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.

Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.

Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.

MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.

ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.

Nawasilisha.
Mkuu mtiririko wako wote waweza kuwa sahihi, lakini hili la kuambiwa habari za mke wa padre kisha ukaishiwa nguvu na kuchutama "umebonyeza sana".
Jambo la maisha private ya mtu laweza kukuvunja nguvu kiasi hicho hadi uchutame?
Mavimada na watoto wa mapadre mitaani haujawahi kuona ama kusikia?
Basi pole.
 
Mpaka hapo wewe siyo mkatoliki. Unashauri waoe? Kuwa serious. Kwanini alikubali wito? Unajikanyaga. Eti wana matamanio. Alichagua utume. Hivyo kama anaishi maiaha hayo basi hana wito
Mbona silaa aliacha. Wako masista pia wameacha utawa wameolewa swma wengi huwa wanakuaga kama wamechanganyikiwa hivi.

Kuna huyo sista Regis alikua mrembo balaa na shepu lake. Kaolewaaa. Plus sista Leonidas. Just few to mention.
 
KWANI MAPADRE SIKU HIZI WANAISHI KWAO? UONGO MTUPU MAPADRE WANAISHIPAROKIANI AU KWENYE NYUMZA ZA MAPADRE JAPO WAPO WENYE WATOTO ILA HUWEZI KUWAKUTA ETI WANAISHI NAO PAROKIANI HUO NI UONGO WA MCHANA KWEUPEEEEEE
[emoji3581][emoji817] True !!
 
Mkuu mtiririko wako wote waweza kuwa sahihi, lakini hili la kuambiwa habari za mke wa padre kisha ukaishiwa nguvu na kuchutama "umebonyeza sana".
Jambo la maisha private ya mtu laweza kukuvunja nguvu kiasi hicho hadi uchutame?
Mavimada na watoto wa mapadre mitaani haujawahi kuona ama kusikia?
Basi pole.
Mkuu kilichonivunja nguvu ni ukweli kuwa mapadre hawaruhusiwi kuoa lakini huyu hapa kaoa na wananchi wote wanafahamu kuwa ana mke lakini wamekaa kimya. Bahati mbaya sijawahi kuona mtoto wa padre wala kusikia tetesi kuwa mtoto fulani ni wa padre.

Kama kweli kuna mapdre wana watoto mtaani na wanajulikana, basi taasi ya kanisa katoliki imeingiliwa mno na mamluki. Ipo haja ya kufanya mageuzi makubwa ndani ya kanisa katoliki, hasa hili la kuwaruhusu mapdre kuoa.
 
Back
Top Bottom