Kuna haja ya kuwaruhusu mapadre kuoa na masista kuolewa. Kitendo cha mapadre kuwageuza masista kuwa "wake" zao kimeota mizizi ndani ya kanisa katoliki. Sioni sababu ya msingi ya kuendelea kuwatesa hawa watu kwa kisingizio cha kumtumikia Mungu. Mbona maaskofu wa madhehebu mengine, akina Dr Malasusa, wameona na wanapiga injili bila shida. Kanisa katoliki acheni huu uhafidhina usiokuwa na kichwa wala miguu. Kama hilo haliwezekani, basi wawaruhusu mapdre kuwaoa masista hadharani kuliko wanavyowageuza kuwa wake zao kwa kificho.