Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kesi ipo Mahakamani, kasimamishwa kuhudumu.
Ukistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.
Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.
Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.
MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.
ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.
Nawasilisha.
Ukristo ni sanaaYaani umezaliwa na uume tena uko madhubuti halafu uliokutana nao tu duniani wanakukataza usiutumie kula raha za dunia ?
Wakristo wajinga,yaan Mnavyowatetea hao mapadri mabazaziSasa nawewe ulienda kuungama dhambi zako au ulienda kufanya nini kwenye nyumba za watu? Unatakiwa kwenda kanisani si kwenye makazi yao.
Hapana usiongezee lolote 😂😂😂Mmmh vp kuna cha kuongezea hapo[emoji23][emoji23][emoji23]
wanasema binaadamu hawezi kuacha tabia zake za asiliUkistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.
Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.
Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.
MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.
ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.
Nawasilisha.
Weeeh apia,Bora hata huyo padre kaoa mke kuliko kudanga kwa siri...bora na huyo anayevuta sigara kali kuliko wanavuta mpaka bangi
kwani uislam ni nini?Ukristo ni sanaa
sigara kali ndio bangiBora hata huyo padre kaoa mke kuliko kudanga kwa siri...bora na huyo anayevuta sigara kali kuliko wanavuta mpaka bangi