Ajabu na kweli: Padri wa kanisa katoliki kaoa mke na anavuta sigara kali!

Yaani nimecheka heading ya uzi kabla sijasoma uzi wenyewe 🤣🤣🤣
Nilivyosoma ndio kabisa nacheka mpk machozi……!!! Countrywide njoo Hatimaye baba Padre kafikiwa huku
 
Kuna padri mmoja aliniacha hoi kwa mshangao. Baada ya kumaliza misa kigangoni akaelekea kunywa pombe iliyokuwepo jirani, pombe yenyewe ni ya kienyeji. Baada ya kutoka kwenye pombe akabukia kiko mdomoni kisha akawasha gari yake kurudi parokiani. Mshangao ni kwamba inakuaje mtu wa Mungu atoke kwenye ibada na kukimbilia kunywa pombe kisha aongeze kilevi kingine cha tumbaku kwenye kiko na avute? Mungu gani huyo wa hovyo kuruhusu watumishi wake wawe walevi?
 
Ukistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.

Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.

Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.

MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.

ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.

Nawasilisha.
Picha iko wapi wewe! Namna gani wewe
 
Igizo
Kama ni halisia mtaje jina na alipo sisi wanasheria tutakulinda
 
Mbona babu yetu alikuwa anaishi na mwanamke na kuzaa nae watoto kabisa,

Huku songea hao wakuitwa ma padre wamezalisha hatari,halafu wanajifanya siri,

Hakunaga siri chini ya jua.
 
Ukistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.

Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.

Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.

MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.

ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.

Nawasilisha.

Mnajua fika nguvu ya kanisa ipo kwenye utowashi,ndio mana mnahangaika ili kanisa liingiwe na udhaifu,mwanaume aliyeoa na mwenye familia ni dhaifu mana hawezi kujali maslahi ya taasisi na kuacha ya familia.

Naomba kanisa lishikirie msimamo huo huo wa matowashi ambaye hawezi aondoke.
 
Ukistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.

Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.

Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.

MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.

ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.

Nawasilisha.
mi kwanza ncheke 🤣😂
mmhh tueleze kwanza wewe unavuta nini hapo ulipo?

hizo hasira dhidi ya huyo Padre zimetoka wapi?

na huyo Padre ameanza lini hayo mambo? Ulijiskiaje baada ya kuanguka chini?

sasa si umkataze asiende kuungama nyakati za usiku......

njia nyingine ni kuhama kanisa maana kupitia kikundi cha wanawake ndio maana anaenda kwa Padre mara kwa mara na hawezi acha na inaumiza sana ....

Fanya ivo usije ukapoteza maisha kwa presha, chako hicho kinaliwaje kizembe ivo
 
Back
Top Bottom