Ajabu na kweli: Padri wa kanisa katoliki kaoa mke na anavuta sigara kali!

Ukistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.

Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.

Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.

MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.

ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.

Nawasilisha.
Sasa hapo kuna maajabu gani?! Au, wewe bado upo miaka, ya, 1990?!
Siku,hizi, wachungaji wanazini na, wanakwaya, mama, mchungaji anatoka na shamba boi, maaskofu wanabaguana kikabila, wanamiriki baa, wananunua machangu doa,maofisini, kwa, wadada ni full kudanga!, hakuna, jipya siku hz,
Bsdala ya kupoteza muda kushangaa ya watu binafsi, we jiulize hv huwa kuna umuhimu kila mwaka kutenga bajeti ya kununua v8 toleo jipya kila moja inauzwa 250milioni+!?
Hv huwa, kuna haja ya, kuendelea, kugawa nchi na, kuongeza, mikoa?
Jiulize, kwanini wana nchi, wa, Uganda, wanavumilia maumivu ya dikiteta, wakati niger, misri,Tunisia, Mali, walikataa, wakaingia balabalani,?
Jiulize kwanini, vijana wa bongo, wanaona ni Bora Uwe chawa, upate ugsri wako, ulale mbele, mustakabali wa nchi, tutajua mbele ya safari!
 
Ukistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.

Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.

Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.

MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.

ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.

Nawasilisha.
Wewe ustaz umeshaenda kula maulidi yenu kesho
 
Mkuu utamu wa papuchi hauna mfano [emoji39][emoji39][emoji39]
Kuna mtu alisema sheikh na padri walikutana kwenye ndege, padri akaagiza msosi una nyama ya kiti moto na kwakuwa walikaa siti zilizofatana padri akamkaribisha sheikh, sheikh akasema situmii kiti moto, padri akamjibu"unakosa utamu" ... baada yakushuka kwenye ndege wakawa wanaagana basi sheikh akamwambia padri msalimie mkeo nae padri akajibu sisi hatuoi, sheikh akasema "mnakosa utamu"
 
Kuna padri mmoja aliniacha hoi kwa mshangao. Baada ya kumaliza misa kigangoni akaelekea kunywa pombe iliyokuwepo jirani, pombe yenyewe ni ya kienyeji. Baada ya kutoka kwenye pombe akabukia kiko mdomoni kisha akawasha gari yake kurudi parokiani. Mshangao ni kwamba inakuaje mtu wa Mungu atoke kwenye ibada na kukimbilia kunywa pombe kisha aongeze kilevi kingine cha tumbaku kwenye kiko na avute? Mungu gani huyo wa hovyo kuruhusu watumishi wake wawe walevi?
Hili ni suala la kushangaza sana. Unajua mapadri wengine wachumiatumbo tu......wapo kwenye upadri kuganga njaa na wala hawana wito wowote wa kumtumikia Mungu.
 
Back
Top Bottom