Ajabu sana, Waziri anakiri watanzania ni masikini halafu bado anaweka tozo

Kuna mwamba nimemsikia kwenye habari leo kajua kunikosha, watu wanaumia sana na hii mitozo!
 
 
Mwigulu ni [emoji117][emoji90][emoji90][emoji90]tu
 
Baada ya malalamiko toka kwa wananchi juu ya tozo, Mh Rais akaitisha kikao cha baraza la mawaziri, na kuwaagiza waingie kwenye press waendelee kutupandisha hasira.
Yaani Mwigulu ana jua Watanzania ni maskini, lakini bado ana waibia hata kile walicho hifadhi kujikimu maisha. Upuuzi mtupu. Hii ni kejeli kwa Watanzania.
 
Wananchi masikini lakini viongozi wao wanaishi maisha ya kifahari sana. Wanaendeshwa kwenye magari ya kifahari, wanaishi kwenye mijumba ya kifahari. Haya ndiyo matunda ya mfumo mbovu alioujenga Nyerere.
Nyerere alikuwa akiishi kimasikini na hata alipojengewa nyumba kubwa huko kijijini kwake Butiama alisema hana haja na nyumba kubwa maana yeye sio Tembo !! Nyerere alianzisha misingi mizuri lakini alishindwa kuikamilisha kwa kuondoka madarakani bila kuibadili katiba ambayo mwenyewe alikiri kuwa sio nzuri !! Kwa taarifa yako ni kwamba misingi mizuri ilikuja kubadilishwa na utawala wa Mzee Ruksa kupitia Azimio la Zanzibar !! Misingi yote mizuri ya utawala na nidhamu vikatupiliwa mbali !! Sasa hivi kila mtu anafikiria kujilimbikizia mimali tu !! Kila mtu akipata nafasi anafikiria namna gani atajirike kupitia mezani kwake na aishi kifahari !! Hii kitu kipindi cha Nyerere haikuwepo !! Kama wapo watu wamekaririshwa ubaya wa kumhusu Nyerere wawaulize watu waliokuwepo enzi hizo !! Siku zote historia hupotoshwa !!
 
Ukitaka kufatilia sana porojo za kisiasa hapa... nchini kila siku utaona mambo ni mapya tuu... ivi kwenye karne hii ambayo sayansi na teknolojia ilivyo panuka hivi bado tuu, serikali inazungumuzia mambo kama haya... mara
#Ukosefu wa matundu ya vyoo mashuleni
#Ukosefu wa madarasa mashuleni..
#ukosefu wa waalimu mashuleni
#ukosefu wa vitabu mashuleni...
#ukosefu wa maji
#uduma za afya
Hii nchii hatuwezi kufika popote tunapo taka iwepo
Tatizo la nchii hii siyo huyu waziri wa fedha wala viongozi wengine. TATIZO LA TANZANIA, NI WATANZANIA Wenyewe .....

Akili zetu zimelala sana, inabidi tuamuke na... tukiamuka tutajua tunakwama wapi, na wapi tuanzie..... NAOMBA TUANZE NA MAANDAMANO YA KATIBA ....HIYO NDIYO SULUHISHO LA MATATIZO YETU YOTE....
 
ukitaka kutawala vizuri watu maskini wakamue kwa tozo za kutosha wabaki empty, wakati wakizagaa mitaani huku na huko wakihaha kutafuta maisha na msosi we unakaa zako na benchi lako la ufundi Singida Big Stars kupiga stori na wabrazil!!

Kelele za "wajinga" zinaingia sikio moja na kutokea la pili ushahidi ni kwa hii sentensi "nimeona tuendelee na tozo kama mwaka jana".
 
Vyema kabisa
 
🤣
 
wakati anakiri kuwa Tanzania ni maskini lakini hapo hapo anashangingi la milioni 560
 

Unatumia propaganda kumsafisha huyo Nyerere lakini hasafishiki. Nyerere ndiye muasisi wa mfumo mbovu uliopo, ushahidi huu hapa

 
Pamoja na yote yaliyosemwa na yatakayosemwa lakini ukweli unabaki kuwa Nyerere aliishi maisha ya kawaida sana na hakuwapendelea hata watoto wake na wala hakujilimbikizia mali !! Japo alijitengenezea ufalme na kuwa na madaraka makubwa sana yasiyohojiwa na mtu yeyote lakini bado aliishi maisha ya kawaida sana na wala hakujilimbikizia mali wala hakufanya upendeleo wowote kwa ndugu zake wala kwa watoto wake!! Kwa ufupi ni kwamba pamoja na nguvu alizokuwanazo kimamlaka lakini hakuzitumia nguvu hizo kujilimbikizia mali wala kuishi maisha ya kifahari !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…