Ajabu sana, Waziri anakiri watanzania ni masikini halafu bado anaweka tozo

Ajabu sana, Waziri anakiri watanzania ni masikini halafu bado anaweka tozo

Pamoja na yote yaliyosemwa na yatakayosemwa lakini ukweli unabaki kuwa Nyerere aliishi maisha ya kawaida sana na hakuwapendelea hata watoto wake na wala hakujilimbikizia mali !! Japo alijitengenezea ufalme na kuwa na madaraka makubwa sana yasiyohojiwa na mtu yeyote lakini bado aliishi maisha ya kawaida sana na wala hakujilimbikizia mali wala hakufanya upendeleo wowote kwa ndugu zake wala kwa watoto wake!! Kwa ufupi ni kwamba pamoja na nguvu alizokuwanazo kimamlaka lakini hakuzitumia nguvu hizo kujilimbikizia mali wala kuishi maisha ya kifahari !!

KWa hiyo kama Nyerere aliishi maisha ya kawaida ndiyo tusijadili au tusahau mfumo mbovu alioujenga?
 
Unapoongelea swala kilimo kwa vijana atuambie ni kwa namna gani izo tozo zinaenda kumnufaisha kijana.
Nchi hii Ina vyanzo vingi vya maji walipaswa kujenga miundombinu ya umwagiliaji ya kwenye kila wilaya na si ivi ilivyo sasa.
Kwa akili ya kawaida unaenda kupeleka ruzuku kwenye mbolea wakati hao wakulima hawana uhakika wa mvua hii ni kupoteza pesa za walipakodi.
Hatuwezi kuwa tunapoteza pesa kila mwaka kwenye ruzuku ambako.hakuna matokeo chanya.
Weka miundo mbinu ya umwagiliaji vijana wawe na uhakika wa kilimo.
 
Huyu ndiye anayemharibia Rais wetu.
Jamaa ni mlaghai kuanzia utosi mpaka unyayo.

So huyo raos ye haoni yanayofanywa au kusikia wewe huko ndio unaona na kusikia!!!...
Huwo ni mpango wa huyo rais mwingulu unamuonea
 
Ukitaka kufatilia sana porojo za kisiasa hapa... nchini kila siku utaona mambo ni mapya tuu... ivi kwenye karne hii ambayo sayansi na teknolojia ilivyo panuka hivi bado tuu, serikali inazungumuzia mambo kama haya... mara
#Ukosefu wa matundu ya vyoo mashuleni
#Ukosefu wa madarasa mashuleni..
#ukosefu wa waalimu mashuleni
#ukosefu wa vitabu mashuleni...
#ukosefu wa maji
#uduma za afya
Hii nchii hatuwezi kufika popote tunapo taka iwepo
Tatizo la nchii hii siyo huyu waziri wa fedha wala viongozi wengine. TATIZO LA TANZANIA, NI WATANZANIA Wenyewe .....

Akili zetu zimelala sana, inabidi tuamuke na... tukiamuka tutajua tunakwama wapi, na wapi tuanzie..... NAOMBA TUANZE NA MAANDAMANO YA KATIBA ....HIYO NDIYO SULUHISHO LA MATATIZO YETU YOTE....
Sidhani kama suluhisho hapa ni Katiba, tunaweza kuwa na Katiba mpya lakini Viongozi wakapuuza misingi ya Katiba hiyo, hata haya ya hovyo yanayofanyika hakuna sehemu yoyote ya Katiba ambayo imeruhusu.

Kuhusu Maandamano naweza kukuunga mkono lakini yawe Maandamano ya kupinga uozo wa Serikali hii ya awamu ya sita, haiwezekani leo hii Wananchi masikini tunalia na kupanda kwa gharama za bidhaa ikiwemo chakula na bado tunawekewa Tozo na huku Serikali ikishindwa kupunguza matumizi ya anasa, hii haikubaliki.
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi ishu ambayo imekua gumzo nchini kuhusu masuala ya tozo kwenye miamala ya simu na benki ambapo hizi ni baadhi ya nukuu ya alichokisema.

“Kwanini mwaka huu tozo ziliendelea tena?, tumeendelea tena kwasababu tumeshafanya kwenye madarasa na vituo vya afya lakini kuna mambo ya msingi ambayo yana umuhimu wa kuchukuliwa hatua kwa haraka sana”

“Tunahitaji kuweka nguvu kubwa sana kwenye shughuli za uzalishaji, tatizo la ajira kwa Vijana ni kubwa mno, Watu wasio na kipato nchini ni wengi sana, kila wanapomaliza darasa la saba kuna Watoto laki mbili hawaendelei na kidato cha kwanza na kila wanapomaliza kidato cha nne kuna Watoto karibu laki tatu hawaendelei kidato cha tano, tumewahi kujiuliza wanaenda wapi na ‘future’ yao ipoje?”

“Tumeshajiuliza wale wanaohitimu na hawaingii Ofisini wanaenda wapi!?, hakuna Kijiji hata kimoja ambacho hakina Mhitimu ambaye hana kazi ndio maana Rais anasema tuweke nguvu kubwa kwenye shughuli za uzalishaji, ndio maana tumeweka pesa nyingi kwenye kilimo ili Vijana wengi watengeneze kipato…. hawa ambao hawana ajira”

“Mnyororo wa umasikini mkiubariki inakuwa unabaki hivyohivyo haundoki kwahiyo zaidi ya Trilioni 1 zimeenda kwenye kuongeza nguvu kwenye uzalishaji upande wa kilimo, uvuvi, Wamachinga” ——— amesema Waziri Nchemba,
Tuna mawaziri wa ajabu haijawai tokea
 
IMG_9336.jpg

ccm mbele kwa mbele
 
Kama Kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya kununua V8 Vx kwa ajili ya wakubwa mwaka 2022/23 zipelekwe kwenye ujenzi wa vyoo,madarasa, vituo vya Afya, visima vya maji nk. Badala ya tozo za miamala.
Rais wa Zambia,amekaa kununuliwa magari mpya wakati anaingia madarakani yeye na mawaziri wake wote na kazi inaendelea.Lakini hapa kwetu mawaziri wanashindana kununua magari ya kifahari na Kuna Mkurugenzi mmoja Kanda ya ziwa naye alitumia fedha za mrahaba kutoka Geita Gold Mine kununua V8vx ya milioni 500, fedha inayotosha kujenga kituo Cha Afya.
Serikali inunue magari ya kutoa huduma kwa wananchi au kwa taasisi ambazo hazina magari kabisa, badala ya magari ya kifahari.
Hata ukienda nchi wahisani, hawana magari ya kifahari kama hapa kwetu.
Ushauri
Serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima, badala ya kukimbilia kutoza wananchi,wapiga kura wetu,kodi mara mbili mbili
 
Siyo mimi nasema ila ni ukweli Nyerere ndiyo chanzo cha mfumo mbovu.
Pigania mfumo mbovu uvunjwe kwa nguvu zote !! Nyerere has gone forever kama alikosea sisi tulio hai bado tupiganie kuubadilisha huo mfumo mbaya !! Unaonaje tuanze na kupata katiba mpya !! Kumlaumu Nyerere hakutatusaidia chochote Mkuu !! The past has gone forget it , the future hasn’t arrived to hell with it but the present is here use it !!
 
Kama Kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya kununua V8 Vx kwa ajili ya wakubwa mwaka 2022/23 zipelekwe kwenye ujenzi wa vyoo,madarasa, vituo vya Afya, visima vya maji nk. Badala ya tozo za miamala.
Rais wa Zambia,amekaa kununuliwa magari mpya wakati anaingia madarakani yeye na mawaziri wake wote na kazi inaendelea.Lakini hapa kwetu mawaziri wanashindana kununua magari ya kifahari na Kuna Mkurugenzi mmoja Kanda ya ziwa naye alitumia fedha za mrahaba kutoka Geita Gold Mine kununua V8vx ya milioni 500, fedha inayotosha kujenga kituo Cha Afya.
Serikali inunue magari ya kutoa huduma kwa wananchi au kwa taasisi ambazo hazina magari kabisa, badala ya magari ya kifahari.
Hata ukienda nchi wahisani, hawana magari ya kifahari kama hapa kwetu.
Ushauri
Serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima, badala ya kukimbilia kutoza wananchi,wapiga kura wetu,kodi mara mbili mbili
Wenye huruma watazingatia huu ushauri !!
 
Tuliambiwa madarasa ya vijana wetu na vituo vya afya vinajengwa kwa fedha za UVIKO
Miradi ya lile Bwawa la Nyerere na SGR ni mikopo ndio inajenga
Leo hii tunaambiwa TOZO ndio zinatumika! Hapa nafikiri kuna kitu hakiko sawa na kinafichwa!
 
Unapoongelea swala kilimo kwa vijana atuambie ni kwa namna gani izo tozo zinaenda kumnufaisha kijana.
Nchi hii Ina vyanzo vingi vya maji walipaswa kujenga miundombinu ya umwagiliaji ya kwenye kila wilaya na si ivi ilivyo sasa.
Kwa akili ya kawaida unaenda kupeleka ruzuku kwenye mbolea wakati hao wakulima hawana uhakika wa mvua hii ni kupoteza pesa za walipakodi.
Hatuwezi kuwa tunapoteza pesa kila mwaka kwenye ruzuku ambako.hakuna matokeo chanya.
Weka miundo mbinu ya umwagiliaji vijana wawe na uhakika wa kilimo.
Hakika kama wakubwa wangekuwa wanakopa pesa kwa ajili ya miundo mbinu ya umwagiliaji mashamba katika kila wilaya umasikini ungeambiwa bye bye katika Nchi hii. !! Lakini kutegemea mvua katika kilimo hasa kwa nyakati hizi za uharibifu wa mazingira uliokwisha kufanywa na binadamu duniani kote ni kujidanganya !! Kopeni pesa kwa ajili ya umwagiliaji nchi nzima kisha wekeni tozo za kila aina watu watalipa na hakuna atakayelalamika !! Kupanga ni kuchagua !!
 
Huyu ndiye anayemharibia Rais wetu.
Jamaa ni mlaghai kuanzia utosi mpaka unyayo.
Kwamba yeye na washauri wake wamepofushwa au hawasikii.hlo ni akizo la mama tozo Wala msimtwike mwigulu.mwigulu anatumika kama toilet peper.rais anamamlaka kisheria akiona mambo yanaenda ndivyo sivyo.ila kwa vile amelibaliki hili hakuna tatizo anaona mwa tz wanyooshwe tu .wakati wao mishahara Yao haikatwi kodi.na Ili mambo yaende sawa uwasikie na wajuu wanalalamika waweke tozo kwa asilimia unayoitoa kwenye mabenk na kwenye cm na kwenye pango za nyumba.kwamba asilimia 5 kwa Hela ya m 100 tutapata m5.hapo ndio tutafanya maendeleo nakwa haki.sio masikini anapata kwa mwezi sh 300,000 makato yanataka kulingana na mtu anayelipwa m 13 na Gali Bure afya Bure,dereva Bure,mafuta bule.semina kibao.huyu haya malalamiko ya maskin atayajulia wapi
 
Sidhani kama suluhisho hapa ni Katiba, tunaweza kuwa na Katiba mpya lakini Viongozi wakapuuza misingi ya Katiba hiyo, hata haya ya hovyo yanayofanyika hakuna sehemu yoyote ya Katiba ambayo imeruhusu.

Kuhusu Maandamano naweza kukuunga mkono lakini yawe Maandamano ya kupinga uozo wa Serikali hii ya awamu ya sita, haiwezekani leo hii Wananchi masikini tunalia na kupanda kwa gharama za bidhaa ikiwemo chakula na bado tunawekewa Tozo na huku Serikali ikishindwa kupunguza matumizi ya anasa, hii haikubaliki.
Katiba ikiwa nzuri haiwezi kumpa nafasi mtu yeyote kuivunja au kuichezea kwa sababu mihimili yote itakuwa na nguvu na haitokuwa inasubiri maagizo kutoka juu kuwashughulikia wale watakaobainika wameivunja katiba !! Sasa hivi mhimili mmoja mkuu ndio Alfa na Omega kwa mujibu wa katiba ilivyo !!
 
Wanatumia hela yangu kujinunulia V8!! Nimeumia sana.
 
Wanatumia hela yangu kujinunulia V8!! Nimeumia sana.
Wanakera sana, yaani sisi Wananchi masikini ndiyo tuwahudumie wao, ningewaelewa kama wangeacha kuishi maisha ya anasa kwa Kodi zetu.

Kuna wakati tuliaminishwa kuwa safari za Rais nje ya Nchi ni kwenda kutafuta Fedha, kama ndiyo kuna sababu gani ya kuwekeana Tozo umiza?
 
Katiba ikiwa nzuri haiwezi kumpa nafasi mtu yeyote kuivunja au kuichezea kwa sababu mihimili yote itakuwa na nguvu na haitokuwa inasubiri maagizo kutoka juu kuwashughulikia wale watakaobainika wameivunja katiba !! Sasa hivi mhimili mmoja mkuu ndio Alfa na Omega kwa mujibu wa katiba ilivyo !!
Usitegemee Katiba ya kuwabana Watawala katika Nchi hii, ndiyo maana hata Rasimu ya Katiba ya Walioba ilipigwa vita na ikakwama.
 
Back
Top Bottom