kiukweli mkuu sisi wanawake huwezi kutuelewa,juzi hapa mama alikuwa analia baada ya watoto wawili kufa kwa kansa ya ngozi
Tiririka nami(ni siri lakini navujisha)
Mwanamke mrembo cheupe aliolewa na hb wake mweusi kama alivyomchagua (anasema mmewe alikuwa andisamu),basi Mungu kawapa uzao mtoto wa kwanza wa kike akatoka kopy baba mtupu (sura ya baba na rangi ya kijaruo)mama hakupenda kabisa akasema iweje mimi mrembo mweupe nizae mtoto mweusi?akasema labda akiendelea kukua atabadilika rangi na kuwa mrembo kama yeye, lakini mpaka anafikisha miaka mitatu bado ni kopy ya baba yake akamwanzishia mkorogo na pia akaanza kumpost insta wanamsifia akajaa bichwa.
Akabeba mimba ya pili akatoka wa kike kopy ya baba,sasa akawaza na kuwazua akaona suluhisho ni kumuwahi akiwa na miezi miwili tu akamuanzishia mkorogo kweli akawa amewini mtoto white white,baada ya kutimiza mwaka mtoto akaanza kuumwa ugonjwa haueleweki ndo kuchunguza zaidi madaktari wakasema kansa inshamla tyari basi hakukaa sana akafa baada ya huyo akaja mkubwa japo alichukua mda kuliko yule mdogo lakini naye akafa kwa ugonjwa huohuo(siri anayo mama na hajawahi kumwambia mtu maana mme akijua ataua mtu,amebaki nalo moyoni anasema labda ningekuwa hata na elimu ya form four watoto wangu nisingewafanyia haya kiukweli anajuta