Ajali husababishwa na uzembe na ujinga wa kibinadamu. Hakuna Mungu, Shetani au uchawi unaosababisha ajali

Ajali husababishwa na uzembe na ujinga wa kibinadamu. Hakuna Mungu, Shetani au uchawi unaosababisha ajali

Infropreneur

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2022
Posts
14,578
Reaction score
31,662
Waafrika hasa watanzania hawatii wala kuzingatia sheria za barabarani halafu wakishapata ajali au ajali ikishatokea wanaanza kupayuka na kutoa maoni kama wehu, Mungu tunusuru! Allah tuokoe! Yesu tusaidie!

Wakati Dereva anakanyaga mafuta kisawasawa, speed kibati, mwendo wa ngiri mkia juu, kasi ya kuovateki ndege 🛫. Watu kimyaaaa!! wala hawasemi chochote. Wanatulia kama mirungi inayowahishwa kiwandani au kama wagonjwa mahututi wanaokimbizwa ICU.

Halafu ajali ikishatokea ndio wanaanza sasa mara Mungu! Mara kafara! mara ushirikina! mara Shetani! Mara mwisho wa mwaka ajali zimekuwa nyingi!

Wanasahau kabisa kuhusu mwendokasi, speed kibati mwendo wa ngiri mkia juu, uzembe wa dereva, ulevi, ubovu wa barabara na kutozingatia sheria za barabarani.

Waafrika hasa watanzania wana kasumba ya kuamini na kuhusisha ajali hasa za barabarani na dhana za Mungu, Shetani, kafara au uchawi.

Utasikia wakisema kauli kama, "Tumemkosea nini Mungu hadi ajali zinakuwa nyingi?" Kana kwamba huyo Mungu ndio analeta ajali.

Utasikia tena, "Tuzidishe maombi na kusali sana kwani ajali zimeongezeka sana". Kana kwamba bila maombi na sala kwa huyo Mungu, ajali ndio zinaongezeka.

Utasikia, "Lile eneo kuna uchawi na ushirikina sana ndio maana ajali nyingi hutokea sana pale"

Utasikia tena, "Kafara zimekuwa nyingi sana mwaka huu ndio maana ajali zimekuwa nyingi sana"

Utasikia, " Mwisho wa mwaka huu, shetani anataka roho za watu ndio maana ajali zinatokea sana"

Misemo yote hii ni ya kijinga, iliyojaa ujinga, inayoaminika na watu wajinga.

Pia misemo yote hii ina logical fallacies. Post hoc ergo propter hoc na non-sequitur .

Hakuna Mungu anayehusika na ajali.

Hakuna Shetani anayehusika na ajali.

Hakuna uchawi au ushirikina kwenye ajali.

Hakuna ajali inayotokea kwa sababu ya utoaji kafara.

Ajali zote husababishwa kwa uzembe na ujinga wa kibinadamu unaotokana na wanadamu.

Learn or perish.

Think or Sink.

Understand or buzz off.

I'm out.
 
Mbona mnaponda sana waafrika, kwani kwa wazungu hakuna ajali?
Wafrika Tunapenda kujishusha wenyewe alafu tunasingizia dini, Bara la asia limejawa na nchi zenye dini nyingi mno ila wao wanaendelea South Korea, Japan, China, India na nchi za waarabu zote ni za dini ila zimendelea, Norway na Sweden nahisi ndo nchi zenye Atheist wengi ila inazidiwa na nchi zenye dini. Ila utasikia ooh Afrika hatuendelei sababu ya dini
 
Are you here to advertise your ignorance?

Ulishawahi kusikia ajali imetokea polisi wakasema chanzo cha ajali ni Shetani, uchawi au ushirikina?
Kwa hiyo Police wanaposema "Risasi ilipigwa juu ili kuwarisha Watu, bahati mbaya ikawajeruhi watu 3 na kupelekea Vifo vyao..."

Kwa hiyo Kwa Akili Yako Utawaamini/Unawaamini Police...!?
Napata shida na uwezo wako wa kufikiri.
 
Kwa hiyo wewe statement za polisi ndio mwisho wa upeo wako?
This is red herring fallacy.

Hatuzungumzii habari za upeo hapa.

Nakuuliza hivi, 👇

Ulishawahi kusikia popote pale duniani kwamba kuna ajali imetokea na chanzo chake ni Mungu, Shetani au uchawi?

Answer the question?

Don't deviate from it.
 
Kwa hiyo Police wanaposema "Risasi ilipigwa juu ili kuwarisha Watu, bahati mbaya ikawajeruhi watu 3 na kupelekea Vifo vyao..."

Kwa hiyo Kwa Akili Yako Utawaamini/Unawaamini Police...!?
Napata shida na uwezo wako wa kufikiri.
Una elewa maana ya ajali za barabarani?

Kuna sehemu nimeongelea habari za risasi?

Au unaleta mifano yako ambayo ni illogical.
 
Una elewa maana ya ajali za barabarani?

Kuna sehemu nimeongelea habari za risasi?

Au unaleta mifano yako ambayo ni illogical.
Umesema wewe Huwa unaamini statement ya Police, means pale Police wanaposema Jambo wewe ndiyo unaamini...!

Nikakupa mfano wa matukio ambayo Police hutoa Statements, nikakuuliza unaamini hata Hilo....!?

Otherwise edit comment Yako, coz unataka sisi tuamini uko vizuri kichwani, then maneno Yako mwenyewe yanatuambia hufikilii sawasawa.
 
Back
Top Bottom