Ajali mbaya Inyala Mkoani Mbeya, idadi ya waliofariki yafikia watu 19

Ajali mbaya Inyala Mkoani Mbeya, idadi ya waliofariki yafikia watu 19

Ajali mbaya imetokea katika eneo la Inyala mkoani Mbeya baada ya lori la mafuta kufeli breki na kugonga basi la abiria na gari ndogo na kusababisha vifo vya watu kadhaa na majeruhi. Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Kila tukiiambia Serikali Kuhusu hii Barabara lakini haielewi..

Balaa jingine litakuja kwenye barabara ya Chunya ikifunguka maana nayo imejengwa bila kuzingatia hizo hatari.
 
nina 100% watu wote wanaomkejeli kinana kwenye hii thread hawana magari ila kwa mwenye kumiliki gari hawez ongea utumbo huo abadani
Wajinga wajinga hao, kero ya askari kujazana barabarani wala haiwezi kuthibitiwa kwa kusingizia ajali. Mtu umekamilika ila bado unaombwa ombwa hela kwa visingizio vya makosa ambayo sio halisi.

Ajali ni kitu kimoja na kuomba rushwa ni kero ingine ikiwamo kupotezeana muda. Zamani dar moro masaa matatu, leo hio dar moro masaa 6
 
Haha !!
ukaguzi wa mara kwa mara ? Pia haisaidii, pananguka mqgari mapya kabisa hapo ,
Kuanzia uyole hadi unafika igawa ni kipande cha kuomba mungu tu , barabara ni finyu na sio rafiki.
Gari bovu ni hatari sana , lakini barabara mbovu ni hatari zaidi
Ni Barbara ya kutokea uyole kwenda wapi?
 
Za kubrashia viatu.
Lini traffic walisaidia kuzuia ajali?

Hopeless kabisa wakati nyie ndo mlisababisha ajali ziwe nyingi kwa kuruhusu magari chakacu yaingie barabarani baada ya kuomba buku mbili ya rushwa.
 
Ajali mbaya imetokea katika eneo la Inyala mkoani Mbeya baada ya lori la mafuta kufeli breki na kugonga basi la abiria na gari ndogo na kusababisha vifo vya watu kadhaa na majeruhi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

---
Watu nane wamefariki Dunia na wengine ambao idadi yao haijafahamika wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo Jumanne, Agosti 16 katika eneo ya Shamwengo karibu na kituo cha mafuta Inyala mkoani Mbeya.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, akieleza kuwa gari la kKampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga lilifeli breki na kuligonga basi la Super Rojas lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe.

“Waliopoteza maisha ni nane japokuwa bado idadi rasmi haijajulikana ila baadaye taarifa ya daktari itaeleza kwa ujumla, ila majeruhi wamesambazwa kwenye hospitali tofauti ikiwamo Igawilo na Mkoa,” amesema Kamanda Matei.
Ni Igawa au Igawilo?
Ajali mbaya imetokea katika eneo la Inyala mkoani Mbeya baada ya lori la mafuta kufeli breki na kugonga basi la abiria na gari ndogo na kusababisha vifo vya watu kadhaa na majeruhi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

---
Watu nane wamefariki Dunia na wengine ambao idadi yao haijafahamika wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo Jumanne, Agosti 16 katika eneo ya Shamwengo karibu na kituo cha mafuta Inyala mkoani Mbeya.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, akieleza kuwa gari la kKampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga lilifeli breki na kuligonga basi la Super Rojas lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe.

“Waliopoteza maisha ni nane japokuwa bado idadi rasmi haijajulikana ila baadaye taarifa ya daktari itaeleza kwa ujumla, ila majeruhi wamesambazwa kwenye hospitali tofauti ikiwamo Igawilo na Mkoa,” amesema Kamanda Matei.
Eneo hili la Inyala kila siku hutokea ajali ya lori, hauwezi kupita bila kukuta lori limeanguka.
 
Mkoa wa mbeya unabalaa gani?!
watu wa mbeya ongezeni maombi, punguzeni ushirikina.
 
Ndio maana mkuu barabara zetu ndio tatizo kubwa, mengine ni mengineyo, mimi ningekua waziri wa mawasiliano hizi pass zote ndani ya T1 ningefanya yafuatayo:kabla hujaanza kushuka kitonga pass ningejenga compossory stop kwa magari yote above 10T,yaani ukifika pale lazima usimame, hii itasaidia to slow down momentum ya vehicles hizi, hivyo hivyo kwa Inyala Pass;,pia ningejenga arrester ili kudeal na magari yaliyo fail breaks, Zambia wanazo hasa kuelekea border ya Chilundu, yaani ukipata break failure unalielekeza gari upande wa arrester (imetengenezwa zaidi kwa mchanga na kokoto);
Hizo truck arrester wamejaribu kuweka pale mlima kolo kondoa , ila hazijawekewa maelezo na madereva wengi hawajui matumizi yake.
Arrester zenyewe pia hazijawekwa kitaalamu kwa truck loaded with 30 tons inaweza kupitiliza
 
barabara finyu..barabara tangu enzi za mkoloni..hata dereva wa lori akigindua tatizo kwenye gari hana pakujitetea zaidi kulipeleka mbele kwa mbele.
 
Mkoa wa mbeya unabalaa gani?!
watu wa mbeya ongezeni maombi, punguzeni ushirikina.
Sio swala la mabalaa , ni mipangilio tu, mbeya ni mkoa wenye boarder mbili busy , ni mkoa ambao unahitaji sana maboresho ya boarder roads ikiwezekano kuwe na dual carriage kuanzia igawa kwenda kasumulu na Tunduma
 
Inyala pipeline panahitaji dual carriage ways. Trafiki wa kinana watasema na hii wangeweza kuzuia kama wangalikuwepo barabarani.
Tunahitaji design Bora za barabara ni si wingi WA polisi wapenda rushwa, any way ajali zipo TU, Cha Muhimu kuomba Mungu
 
Makala hii hapa chini niliiandika Facebook mwezi wa saba baada ya ile ajali mbaya ilioua watu zaidi ya 20 pale Inyala. Bado hatujasahau na hata arobaini za waliokufa zikiwa hazijatimia leo tena wamekufa wengi zaidi chanzo kikiwa kilekile, ufinyu wa barabara, mlima na mteremko mkali, kufeli breki n.k. Kama hatua za dharura hazitachukuliwa hakika tutalia sana maana hili eneo ni zaidi ya machinjio .

Niliandika hivi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Barabara ya Tunduma hadi Dar Es Salaam naamini ndio barabara ya kwanza nchini kupitisha magari mengi ya mizigo kwa kuwa inahudumia nchi karibu kumi. Ajabu barabara hii hasa kuanzia Igurusi ndipo tatizo linapoanzia hasa ajali kuanzia Ilongo hadi Mlima Nyoka kisha Mlima Iwambi na Mlima Senjele.

Huwa haziishi siku mbili bila kutokea ajali kwenye maeneo ya mlima Iwambi, Senjele, mlima nyoka hadi Ilongo, maana ndio maeneo yenye milima na miteremko mikali.

Shughuli kubwa ipo katikati ya jiji kuanzia Nsalaga hadi Mbalizi, hapo ndipo pana utitiri wa ajali za bajaji, pikipiki na magari maana ni barabara moja tu hutumika kwa vyombo vyote vya moto.

Kibaya zaidi barabara hii yote kuanzia Tunduma hadi Igawa ni barabara nyembamba na ya kizamani kwa kuwa ilijengwa zamani sana.

Kama Mzee Kinana ameliona hili tatizo nadhani imefikia wakati sasa amshauri boss wake ambaye ndiye rais wa nchi barabara mpya ijengwe haraka maana kwa wingi wa magari yanayopita Mbeya barabara haiwezi tena kuhimili.

Pia, kwa maoni ingependeza sana barabara ya malori itengwe na barabara ya magari madogo na haya ya abiria kama ilivyofanyika pale Arusha ambapo wamejenga barabara maalumu ya magari ya mizigo inayopita nje ya Jiji la Arusha kuanzia Ngaramtoni hadi USA river. Mfano, kwa hapa Mbeya kuanzia pale Ilongo barabara ya malori ijengwe mpya ipite bondeni kule chini ije itokezee Ndundu Uyole kisha ipite Isyesye ikatize Nanenane iende hadi Ivumwe juu ikatokezee Tazara ikunje Iwambi chini ikatokezee Mbalizi Nsalala ndio iendelee hadi Tunduma kisha hii ya sasa ijengwe mpya ibaki na magari ya abiria na magari madogo.

Nayasema haya sababu huwa haziishi siku mbili bila lori kupoteza mwelekeo barabara ya Mlima Nyoka hadi Shamwengo ambapo ndipo penye milima na miteremko mikali sana . Hata ajali ya mwezi huu iliyoua zaidi ya watu 20 pale Inyala akiwemo mwalimu Iddy Mwandete ilisababishwa na lori kuvamia Costa na vibanda sababu ya kufail breki kwenye mteremko wa Itewe kwenda Inyala.

Eneo hili limekuwa hatari mno kwani licha ya barabara kuwa ndogo, mbovu na yenye konakona inapita kwenye mlima na mteremko mkali ambapo magari ya mizigo huwa rahisi kufeli breki .

Kwa katikati ya jiji ndipo napo panahitajika ujenzi mkubwa wa barabara angalau kuwe na njia nne kama Ile barabara ya Majengo hadi Tengeru.

Ukiwa katika Jiji la Mbeya unashindwa kuelewa hili ni Jiji au wamelisingizia, maana barabara ni ndogo, imejaa mashimo na imebonyea sana hasa maeneo ya Uyole njia panda, mteremko wa Nzovwe na maeneo ya kuelekea Sokoine. Barabara ni changamoto kubwa sana ambapo bila kujengwa mpya ajali na usumbufu utaendelea kuwa mkubwa maana kuna ongezeko kubwa sana la magari na watu ndani ya mkoa hasa jijini.

Mkoa wa Mbeya na mkoa wa Songwe ni mikoa ambayo ni kama maghala ya chakula hapa Tanzania. Unapozungumzia Mbeya unazungumia store ya chakula lakini kiukweli kihuduma hasa barabara ni mkoa uliosahaulika sana. Wilaya ya Mbeya hasa Halmashauri ya Mbeya Vijijini ndio wilaya inayotoa viazi karibu mwaka mzima, viazi vinavyoenda kuliwa Dar es salaam, Zanzibar, Nairobi, Kongo, Zambia na kwingineko, lakini ndio halmashauri ambayo imesahaulika kabisa kwa barabara nzuri.

Kuna barabara ya Isyonye kwenda Makete, barabara ya Mswiswi kwenda Makete hizi ni barabara ambazo zinahitaji lami kwa haraka sana. Ni barabara ambazo zinapitisha malori yaliyobeba viazi, vitunguu swaumu, mahindi, mbao na mazao mengine mwaka mzima kwa wingi mkubwa lakini ajabu kuna msimu hazipitiki sababu ya mashimo, matope na utelezi.

Ipo barabara ya Mbalizi Hadi Izyira, Mbalizi Hadi Ikukwa n.k ni barabara muhimu kwa uchumi wa nchi hii lakini nani wakuzikumbuka ikiwa mbunge hata kuzizungumzia bungeni hatusikii?

Chondechonde serikali, ikumbukeni Mbeya kwa barabara maana hali sio nzuri kabisa. Hali ya barabara mkoa wa Mbeya ni mbaya ikizingatiwa Mbeya ni lango la nchi za SADC na ndio lango la kuingia border kubwa kuliko zote Tanzania yaani Tunduma.

Mfikishieni salam Rais, Waziri wa Fedha, Waziri wa Ujenzi, Spika wa Bunge na wadau wote wa maendeleo. Mzee Kinana alipita hapa jana awe balozi mzuri maana yeye ni shuhuda.

Ni hayo machache
Ndimi
Mwanshinga Jr
 
Back
Top Bottom