TheMnyonge
JF-Expert Member
- Mar 25, 2022
- 738
- 1,886
Hivi hakuna orodha ya majina ya waliofariki?
Walau tuwajue....
Walau tuwajue....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole kwa wafiwa, pole kwa majeruhiMakala hii hapa chini niliiandika Facebook mwezi wa Saba baada ya Ile ajali mbaya ilioua watu zaidi ya 20 pale Inyala . Bado hatujasahau na hata arobaini za waliokufa zikiwa hazijatimia Leo Tena wamekufa wengi zaidi chanzo kikiwa kilekile, ufinyu wa Barabara, mlima na mteremko mkali, kufeli breki n.k . Kama hatua za zarura hatizochukuliwa hakika tutalia sana maana hili eneo ni zaidi ya machinjio .
Niliandika hivi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Barabara ya Tunduma Hadi Dar es salaam naamini ndio barabara ya kwanza nchini kupitisha magari mengi ya mizigo kwa kuwa inahudumia nchi karibu kumi. Ajabu barabara hii hasa kuanzia Igurusi ndipo tatizo linapoanzia hasa hasa ajali kuanzia Ilongo Hadi mlima nyoka kisha mlima Iwambi na Mlima Senjele.
Huwa haziishi siku mbili bila kutokea ajali kwenye maeneo ya mlima Iwambi, Senjele, mlima nyoka Hadi Ilongo maana ndio maeneo yenye milima na miteremko mikali.
Shughuli kubwa ipo katikati ya Jiji kuanzia Nsalaga Hadi mbalizi, hapo ndipo Pana utitiri wa ajali za bajaji, pikipiki na magari maana ni barabara Moja tu hutumika kwa vyombo vyote vya moto.
Kibaya zaidi barabara hii yote kuanzia Tunduma Hadi Igawa ni barabara nyembamba yakizamani kwa kuwa ilijengwa zamani sana .
Kama Mzee Kinana ameliona hili tatizo nadhani imefikia Wakati Sasa amshauri boss wake ambaye ndiye rais wa nchi barabara mpya ijengwe haraka maana kwa wingi wa magari yanayopita Mbeya barabara haiwezi Tena kuhimili.
Pia
Kwa maoni ingependeza sana barabara ya malori itengwe na barabara ya magari madogo na haya ya abiria kama ilivyofanyika pale Arusha ambapo wamejenga barabara maalumu ya magari ya mizigo inayopita nje ya Jiji la Arusha kuanzia Ngaramtoni Hadi USA river . Mfano, kwa hapa Mbeya kuanzia pale Ilongo barabara ya Malori ijengwe mpya ipite bondeni kule chini ije itokezee Ndundu Uyole kisha ipite Isyesye ikatize Nanenane iende Hadi Ivumwe juu ikatokezee Tazara ikunje Iwambi chini ikatokezee Mbalizi Nsalala ndio iendelee Hadi Tunduma kisha hii ya Sasa ijengwe mpya ibaki na magari ya abiria na magari madogo.
Nayasema haya sababu Huwa haziishi siku mbili bila Lori kupoteza mwelekeo barabara ya Mlima nyoka Hadi Shamwengo ambapo ndipo penye milima na miteremko mikali sana . Hata ajali ya mwezi huu iliyoua zaidi ya watu 20 pale Inyala akiwemo mwalimu Iddy Mwandete ilisababishwa na Lori kuvamia Costa na vibanda sababu ya kufail breki kwenye mteremko wa Itewe kwenda Inyala.
Eneo hili limekuwa hatari mno kwani licha ya barabara kuwa ndogo, mbovu na yenye Konakona inapita kwenye mlima na mteremko mkali ambapo magari ya mizigo Huwa rahisi kufeli breki .
Kwa katikati ya Jiji ndipo napo panahitajika ujenzi mkubwa wa barabara angalau kuwe na njia nne kama Ile barabara ya Majengo Hadi Tengeru.
Ukiwa katika Jiji la mbeya unashindwa kuelewa hili ni Jiji au wamelisingizia, maana barabara ni ndogo, imejaa mashimo na imebonyea sana hasa maeneo ya uyole njia panda, Mteremko wa Nzovwe na Maeneo ya kuelekea Sokoine. Barabara ni changamoto kubwa sana ambapo bila kujengwa mpya ajali na usumbufu utaendelea kuwa mkubwa maana Kuna ongezeko kubwa sana la magari na watu ndani ya mkoa hasa jijini.
Mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Songwe ni mikoa ambayo ni kama maghala ya Chakula hapa Tanzania. Unapozungumzia Mbeya unazungumia store ya Chakula lakini kiukweli kihuduma hasa barabara ni mkoa uliosahaulika sana. Wilaya ya Mbeya hasa halmashauri ya Mbeya vijijini ndio wilaya inayotoa viazi karibu mwaka mzima viazi vinavyoenda kuliwa Dar es salaam, Zanzibar, Nairobi, Kongo, Zambia na kwingineko lakini ndio halmashauri ambayo imesahaulika kabisa kwa barabara nzuri.
Kuna barabara ya Isyonye kwenda Makete, barabara ya Mswiswi kwenda Makete hizi ni barabara ambazo zibahitaji lami kwa haraka sana . Ni barabara ambazo zinapitisha malori yaliyobeba viazi, vitunguu swaumu, mahindi, mbao na mazao mengine mwaka mzima kwa wingi mkubwa lakini ajabu Kuna msimu hazipitiki sababu ya mashimo, matope na utelezi.
Ipo barabara ya Mbalizi Hadi Izyira, Mbalizi Hadi Ikukwa n.k ni barabara muhimu kwa uchumi wa nchi hii lakini nani wakuzikumbuka Ikiwa mbunge hata kuzizungumzia bungeni hatusikii,!!
Chondechonde Serikali, ikumbukeni mbeya kwa barabara maana Hali sio nzuri kabisa. Hali ya barabara mkoa wa Mbeya ni mbaya ikizingatiwa mbeya ni lango la nchi za SADDC na ndio lango la kuingia border kubwa kuliko zote Tanzania yaani Tunduma.
Mfikishieni Salam Rais, waziri wa fedha, waziri wa ujenzi, spika wa bunge na wadau wote wa maendeleo. Mzee Kinana alipita hapa Jana awe Balozi mzuri maana yeye ni shuhuda.
Ni hayo machache
Ndimi
Mwanshinga Jr
Bila serikali kufanya jambo TUTAKOMA .Nimepita hapo siku si nyingi, hiko kipande cha Ilongo mpaka Uyole na Kedeghe mpaka Mbalizi ni hatari mno.
Barabara nyembamba na miteremko ni mikali. ?Malori makubwa, ma-bus yaendayo kasi, gaei ndogo, bajaji na pikipiki vyote humohumo.
MUNGU tu huwa anatuepusha. Serikali ifanye jambo pale, tena mapema.
Nimekuelewa sana ndugu japokuwa niliandika ombi , pendekezo na ushauri kwa kuwa ni mwenyeji wa haya Maeneo ndio maana nimeandika kuwa wajitahidi kuhamisha malori kwa kuyajengea njia Yao kule chini itengane na hii ya njia ya Sasa.
Lkni nimekuelewa sana
Kiukweli ilikuwa ngumu kuyajua maana Ile gari ya abiria ilikuwa inatoka mbeya kwenda njombe na kama ujuavyo polisi na Sheria zao.Hivi hakuna orodha ya majina ya waliofariki?
Walau tuwajue....
Ok kaka .Pole kwa wafiwa, pole kwa majeruhi
Ila next time picha muhimu mkuu wengine hawapajui wanapasikia tu
Nawasilisha..
Yes man, miundombinu ndio chanzo na pili ubovu wa haya magari maana ule mlima unahitaji gari Zima lenye break imara hasa likiwa na mzigoKinatokea kijitu kinasema askari warudi barabarani kumbe ni kipiga deal ya rushwa kumbe ajali nyingi ni ubovu wa miundombinu
Mkuu wa Polisi rudisha Askari barabarani, Watanzania watakwisha kwa ajali
Askari wa barabarani pamoja na mapungufu yao wanasaidia sana kupunguza ajali barabarani kwa zaidi ya 70% askari wanaepusha ajali zinazozuilika. Ila unaskia matamko ya mwanasiasa anayetembea kwa king'ora, asiyejua foleni anatafuta publicity anasema traffic wapungue barabarani. Kwenye nchi hizi...www.jamiiforums.com
NimeshapaelewaOk kaka .
Lkni kwa kifupi ukiwa unaingia mbeya ukishafika mpakani mwa wilaya mbarali na mbeya Kuna sehemu panaitwa Ilongo.
Sasa kuanzia hapo ndio mlima huanzia Hadi mlima nyoka ambapo ndio unakuwa unaingia ndani ya Jiji la mbeya .
Yaani kwa kifupi kata yote ya Inyala na Itewe ndizo zinapitiwa na huu mlima
Nimepita maeneo hayo juzi, hakika Ni eneo korofi sana, serikali iangalie namna ya kudeal na maeneo haya kuanzia uyole , nanyala hadi hapo inyalaHaha !!
ukaguzi wa mara kwa mara ? Pia haisaidii, pananguka mqgari mapya kabisa hapo,
Kuanzia uyole hadi unafika igawa ni kipande cha kuomba mungu tu , barabara ni finyu na sio rafiki.
Gari bovu ni hatari sana , lakini barabara mbovu ni hatari zaidi
Askari huwa wanasumbua sana barabarani wacha waondoke tuwe huru.Bongo ajali zinawamaliza watu kama sisimizi
Ova
Cha ajabu dereva wa bus au Lori anapita hapo kila siku ila akipata ajali atasema Kona Kali,muinuko mkali kana kwamba Kona hio au muinuko umetokea ghafla!ukiwa mtumiaji wa barabara na unapaswa kujua kitu kinaitwa Defensive driving...
Hapo ambapo eneo ni finyu madereva wanapaswa kwenda mwendo mdogo na kuwa na tahadhari na kuacha uzembe....
Ni kweli kabisa. Napafahamu mahali hapo ni barabara ya hovyo kupata kutokea. lakini pia wangepapanua wakaweka na climbing lane na parking ya dharura kwa malori.
Tatizo la Mkoa wa Mbeya ni ushirikina. Ajali nyingi zinazotokea Mbeya zinasababishwa na "ushirikina".
Ndio maana mkuu barabara zetu ndio tatizo kubwa, mengine ni mengineyo, mimi ningekua waziri wa mawasiliano hizi pass zote ndani ya T1 ningefanya yafuatayo:kabla hujaanza kushuka kitonga pass ningejenga compossory stop kwa magari yote above 10T,yaani ukifika pale lazima usimame, hii itasaidia to slow down momentum ya vehicles hizi, hivyo hivyo kwa Inyala Pass;,pia ningejenga arrester ili kudeal na magari yaliyo fail breaks, Zambia wanazo hasa kuelekea border ya Chilundu, yaani ukipata break failure unalielekeza gari upande wa arrester (imetengenezwa zaidi kwa mchanga na kokoto);