Ushirikina wa huo Ukanda hasa hasa kwa Makabila ya Mikoa ya Mbeya, Iringa na hata kule Rukwa wa kutoana Makafara ili Biashara zao ziende umevuka mipaka na hauvumiliki tena.Hizi ajali zitatumaliza jamani!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ushirikina wa huo Ukanda hasa hasa kwa Makabila ya Mikoa ya Mbeya, Iringa na hata kule Rukwa wa kutoana Makafara ili Biashara zao ziende umevuka mipaka na hauvumiliki tena.Hizi ajali zitatumaliza jamani!
Nilikuwa na wasiwasi na to yeye wangu Kama upo salamaCosta ya super Rojas ilibeba watu 40 waliopona ni 5 Tena nao wako mahututi ...sasa hao nane sijui imekuwaje
Mbona spika wa bunge ni wa kwenu kutoka Mbeya?Serikali ikome kutufanya watu wa Mbeya na Nyanda za Juu kafara wao..
Hii Barabara yote ni hatarishi,magari yanaongezeka kuanzia malori hadi magari binafsi na Yale ya IT..
Wabunge wa Mbeya bajeti ijayi msikubali upumbavu wa Serikali wa sijui tunamalizia upembuzi sijui upuuzi gani,mkatae..
Serikali ianze mara moja kujenga Mbeya bypass na kupanua hiyo barabara maana upande wa Inyala ni Majanga,upande wabalizi ni Majanga..
Ukisikiliza ajari zinazosababishwa na maroli Tanzania waweza kuamini dunia nzima hakuna maroli yapo Tanzania tu au Tanzania ndio inaongoza kwa maroli mengi kumbe tatizo ni barabara tu.Ok kaka .
Lkni kwa kifupi ukiwa unaingia mbeya ukishafika mpakani mwa wilaya mbarali na mbeya Kuna sehemu panaitwa Ilongo.
Sasa kuanzia hapo ndio mlima huanzia Hadi mlima nyoka ambapo ndio unakuwa unaingia ndani ya Jiji la mbeya .
Yaani kwa kifupi kata yote ya Inyala na Itewe ndizo zinapitiwa na huu mlima
Makala hii hapa chini niliiandika Facebook mwezi wa saba baada ya ile ajali mbaya ilioua watu zaidi ya 20 pale Inyala. Bado hatujasahau na hata arobaini za waliokufa zikiwa hazijatimia leo tena wamekufa wengi zaidi chanzo kikiwa kilekile, ufinyu wa barabara, mlima na mteremko mkali, kufeli breki n.k. Kama hatua za dharura hazitachukuliwa hakika tutalia sana maana hili eneo ni zaidi ya machinjio .
Niliandika hivi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Barabara ya Tunduma hadi Dar Es Salaam naamini ndio barabara ya kwanza nchini kupitisha magari mengi ya mizigo kwa kuwa inahudumia nchi karibu kumi. Ajabu barabara hii hasa kuanzia Igurusi ndipo tatizo linapoanzia hasa ajali kuanzia Ilongo hadi Mlima Nyoka kisha Mlima Iwambi na Mlima Senjele.
Huwa haziishi siku mbili bila kutokea ajali kwenye maeneo ya mlima Iwambi, Senjele, mlima nyoka hadi Ilongo, maana ndio maeneo yenye milima na miteremko mikali.
Shughuli kubwa ipo katikati ya jiji kuanzia Nsalaga hadi Mbalizi, hapo ndipo pana utitiri wa ajali za bajaji, pikipiki na magari maana ni barabara moja tu hutumika kwa vyombo vyote vya moto.
Kibaya zaidi barabara hii yote kuanzia Tunduma hadi Igawa ni barabara nyembamba na ya kizamani kwa kuwa ilijengwa zamani sana.
Kama Mzee Kinana ameliona hili tatizo nadhani imefikia wakati sasa amshauri boss wake ambaye ndiye rais wa nchi barabara mpya ijengwe haraka maana kwa wingi wa magari yanayopita Mbeya barabara haiwezi tena kuhimili.
Pia, kwa maoni ingependeza sana barabara ya malori itengwe na barabara ya magari madogo na haya ya abiria kama ilivyofanyika pale Arusha ambapo wamejenga barabara maalumu ya magari ya mizigo inayopita nje ya Jiji la Arusha kuanzia Ngaramtoni hadi USA river. Mfano, kwa hapa Mbeya kuanzia pale Ilongo barabara ya malori ijengwe mpya ipite bondeni kule chini ije itokezee Ndundu Uyole kisha ipite Isyesye ikatize Nanenane iende hadi Ivumwe juu ikatokezee Tazara ikunje Iwambi chini ikatokezee Mbalizi Nsalala ndio iendelee hadi Tunduma kisha hii ya sasa ijengwe mpya ibaki na magari ya abiria na magari madogo.
Nayasema haya sababu huwa haziishi siku mbili bila lori kupoteza mwelekeo barabara ya Mlima Nyoka hadi Shamwengo ambapo ndipo penye milima na miteremko mikali sana . Hata ajali ya mwezi huu iliyoua zaidi ya watu 20 pale Inyala akiwemo mwalimu Iddy Mwandete ilisababishwa na lori kuvamia Costa na vibanda sababu ya kufail breki kwenye mteremko wa Itewe kwenda Inyala.
Eneo hili limekuwa hatari mno kwani licha ya barabara kuwa ndogo, mbovu na yenye konakona inapita kwenye mlima na mteremko mkali ambapo magari ya mizigo huwa rahisi kufeli breki .
Kwa katikati ya jiji ndipo napo panahitajika ujenzi mkubwa wa barabara angalau kuwe na njia nne kama Ile barabara ya Majengo hadi Tengeru.
Ukiwa katika Jiji la Mbeya unashindwa kuelewa hili ni Jiji au wamelisingizia, maana barabara ni ndogo, imejaa mashimo na imebonyea sana hasa maeneo ya Uyole njia panda, mteremko wa Nzovwe na maeneo ya kuelekea Sokoine. Barabara ni changamoto kubwa sana ambapo bila kujengwa mpya ajali na usumbufu utaendelea kuwa mkubwa maana kuna ongezeko kubwa sana la magari na watu ndani ya mkoa hasa jijini.
Mkoa wa Mbeya na mkoa wa Songwe ni mikoa ambayo ni kama maghala ya chakula hapa Tanzania. Unapozungumzia Mbeya unazungumia store ya chakula lakini kiukweli kihuduma hasa barabara ni mkoa uliosahaulika sana. Wilaya ya Mbeya hasa Halmashauri ya Mbeya Vijijini ndio wilaya inayotoa viazi karibu mwaka mzima, viazi vinavyoenda kuliwa Dar es salaam, Zanzibar, Nairobi, Kongo, Zambia na kwingineko, lakini ndio halmashauri ambayo imesahaulika kabisa kwa barabara nzuri.
Kuna barabara ya Isyonye kwenda Makete, barabara ya Mswiswi kwenda Makete hizi ni barabara ambazo zinahitaji lami kwa haraka sana. Ni barabara ambazo zinapitisha malori yaliyobeba viazi, vitunguu swaumu, mahindi, mbao na mazao mengine mwaka mzima kwa wingi mkubwa lakini ajabu kuna msimu hazipitiki sababu ya mashimo, matope na utelezi.
Ipo barabara ya Mbalizi Hadi Izyira, Mbalizi Hadi Ikukwa n.k ni barabara muhimu kwa uchumi wa nchi hii lakini nani wakuzikumbuka ikiwa mbunge hata kuzizungumzia bungeni hatusikii?
Chondechonde serikali, ikumbukeni Mbeya kwa barabara maana hali sio nzuri kabisa. Hali ya barabara mkoa wa Mbeya ni mbaya ikizingatiwa Mbeya ni lango la nchi za SADC na ndio lango la kuingia border kubwa kuliko zote Tanzania yaani Tunduma.
Mfikishieni salam Rais, Waziri wa Fedha, Waziri wa Ujenzi, Spika wa Bunge na wadau wote wa maendeleo. Mzee Kinana alipita hapa jana awe balozi mzuri maana yeye ni shuhuda.
Ni hayo machache
Ndimi
Mwanshinga Jr
Wabunge wanafanya kazi gan huko mbeya?Makala hii hapa chini niliiandika Facebook mwezi wa saba baada ya ile ajali mbaya ilioua watu zaidi ya 20 pale Inyala. Bado hatujasahau na hata arobaini za waliokufa zikiwa hazijatimia leo tena wamekufa wengi zaidi chanzo kikiwa kilekile, ufinyu wa barabara, mlima na mteremko mkali, kufeli breki n.k. Kama hatua za dharura hazitachukuliwa hakika tutalia sana maana hili eneo ni zaidi ya machinjio .
Niliandika hivi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Barabara ya Tunduma hadi Dar Es Salaam naamini ndio barabara ya kwanza nchini kupitisha magari mengi ya mizigo kwa kuwa inahudumia nchi karibu kumi. Ajabu barabara hii hasa kuanzia Igurusi ndipo tatizo linapoanzia hasa ajali kuanzia Ilongo hadi Mlima Nyoka kisha Mlima Iwambi na Mlima Senjele.
Huwa haziishi siku mbili bila kutokea ajali kwenye maeneo ya mlima Iwambi, Senjele, mlima nyoka hadi Ilongo, maana ndio maeneo yenye milima na miteremko mikali.
Shughuli kubwa ipo katikati ya jiji kuanzia Nsalaga hadi Mbalizi, hapo ndipo pana utitiri wa ajali za bajaji, pikipiki na magari maana ni barabara moja tu hutumika kwa vyombo vyote vya moto.
Kibaya zaidi barabara hii yote kuanzia Tunduma hadi Igawa ni barabara nyembamba na ya kizamani kwa kuwa ilijengwa zamani sana.
Kama Mzee Kinana ameliona hili tatizo nadhani imefikia wakati sasa amshauri boss wake ambaye ndiye rais wa nchi barabara mpya ijengwe haraka maana kwa wingi wa magari yanayopita Mbeya barabara haiwezi tena kuhimili.
Pia, kwa maoni ingependeza sana barabara ya malori itengwe na barabara ya magari madogo na haya ya abiria kama ilivyofanyika pale Arusha ambapo wamejenga barabara maalumu ya magari ya mizigo inayopita nje ya Jiji la Arusha kuanzia Ngaramtoni hadi USA river. Mfano, kwa hapa Mbeya kuanzia pale Ilongo barabara ya malori ijengwe mpya ipite bondeni kule chini ije itokezee Ndundu Uyole kisha ipite Isyesye ikatize Nanenane iende hadi Ivumwe juu ikatokezee Tazara ikunje Iwambi chini ikatokezee Mbalizi Nsalala ndio iendelee hadi Tunduma kisha hii ya sasa ijengwe mpya ibaki na magari ya abiria na magari madogo.
Nayasema haya sababu huwa haziishi siku mbili bila lori kupoteza mwelekeo barabara ya Mlima Nyoka hadi Shamwengo ambapo ndipo penye milima na miteremko mikali sana . Hata ajali ya mwezi huu iliyoua zaidi ya watu 20 pale Inyala akiwemo mwalimu Iddy Mwandete ilisababishwa na lori kuvamia Costa na vibanda sababu ya kufail breki kwenye mteremko wa Itewe kwenda Inyala.
Eneo hili limekuwa hatari mno kwani licha ya barabara kuwa ndogo, mbovu na yenye konakona inapita kwenye mlima na mteremko mkali ambapo magari ya mizigo huwa rahisi kufeli breki .
Kwa katikati ya jiji ndipo napo panahitajika ujenzi mkubwa wa barabara angalau kuwe na njia nne kama Ile barabara ya Majengo hadi Tengeru.
Ukiwa katika Jiji la Mbeya unashindwa kuelewa hili ni Jiji au wamelisingizia, maana barabara ni ndogo, imejaa mashimo na imebonyea sana hasa maeneo ya Uyole njia panda, mteremko wa Nzovwe na maeneo ya kuelekea Sokoine. Barabara ni changamoto kubwa sana ambapo bila kujengwa mpya ajali na usumbufu utaendelea kuwa mkubwa maana kuna ongezeko kubwa sana la magari na watu ndani ya mkoa hasa jijini.
Mkoa wa Mbeya na mkoa wa Songwe ni mikoa ambayo ni kama maghala ya chakula hapa Tanzania. Unapozungumzia Mbeya unazungumia store ya chakula lakini kiukweli kihuduma hasa barabara ni mkoa uliosahaulika sana. Wilaya ya Mbeya hasa Halmashauri ya Mbeya Vijijini ndio wilaya inayotoa viazi karibu mwaka mzima, viazi vinavyoenda kuliwa Dar es salaam, Zanzibar, Nairobi, Kongo, Zambia na kwingineko, lakini ndio halmashauri ambayo imesahaulika kabisa kwa barabara nzuri.
Kuna barabara ya Isyonye kwenda Makete, barabara ya Mswiswi kwenda Makete hizi ni barabara ambazo zinahitaji lami kwa haraka sana. Ni barabara ambazo zinapitisha malori yaliyobeba viazi, vitunguu swaumu, mahindi, mbao na mazao mengine mwaka mzima kwa wingi mkubwa lakini ajabu kuna msimu hazipitiki sababu ya mashimo, matope na utelezi.
Ipo barabara ya Mbalizi Hadi Izyira, Mbalizi Hadi Ikukwa n.k ni barabara muhimu kwa uchumi wa nchi hii lakini nani wakuzikumbuka ikiwa mbunge hata kuzizungumzia bungeni hatusikii?
Chondechonde serikali, ikumbukeni Mbeya kwa barabara maana hali sio nzuri kabisa. Hali ya barabara mkoa wa Mbeya ni mbaya ikizingatiwa Mbeya ni lango la nchi za SADC na ndio lango la kuingia border kubwa kuliko zote Tanzania yaani Tunduma.
Mfikishieni salam Rais, Waziri wa Fedha, Waziri wa Ujenzi, Spika wa Bunge na wadau wote wa maendeleo. Mzee Kinana alipita hapa jana awe balozi mzuri maana yeye ni shuhuda.
Ni hayo machache
Ndimi
Mwanshinga Jr
Nipo love,nimepona🙏Nilikuwa na wasiwasi na to yeye wangu Kama upo salama
Ni kweli hata wakijazwa wengi wanachokifanya ni kukusanya Rushwa.Trafiki wenvgi kwa sasa wapo kwenye kipindi cha mpito kuombea mabalaa yatokee kwa wingi barabarani ili waseme yanatokea kwa sababu wao hawapo .