Ajali mbaya Inyala Mkoani Mbeya, idadi ya waliofariki yafikia watu 19

Hayo ndio machache? Huwajui watz kuhusu kusoma
 
Serikali ikome kutufanya watu wa Mbeya na Nyanda za Juu kafara wao..

Hii Barabara yote ni hatarishi,magari yanaongezeka kuanzia malori hadi magari binafsi na Yale ya IT..

Wabunge wa Mbeya bajeti ijayi msikubali upumbavu wa Serikali wa sijui tunamalizia upembuzi sijui upuuzi gani,mkatae..

Serikali ianze mara moja kujenga Mbeya bypass na kupanua hiyo barabara maana upande wa Inyala ni Majanga,upande wabalizi ni Majanga..
 
Wabunge wa Mkoa wa Mbeya na Songwe mwaka ujao msikubali msibukali upuuzi wowote wa serikali na blaa blaa za hiyo barabara..

Malori yameongezeka kadiri uchumi wa Nchi na Nchi jirani unavyokua,magari binafsi kuanzia IT hadi ya watu binafsi nayo hivyo hivyo,barabara inazidi kusongamana..

Lazima hiyo barabarani ipanuliwe haraka,na Mbeya bypass ijengwe maana Hapo Uyole kwenda Inyala ni Majanga,Meta kwenda Mbalizi kote ni Majanga,hivyo hivyo ukienda hadi Tunduma.
 
ukiwa mtumiaji wa barabara na unapaswa kujua kitu kinaitwa Defensive driving...

Hapo ambapo eneo ni finyu madereva wanapaswa kwenda mwendo mdogo na kuwa na tahadhari na kuacha uzembe....
 
Hakika, yaani ni kama wameamua watumiaji wa hii barabara hasa wenyeji wa Mbeya kuwa Mbuzi wa kafara .

Yaani umeongea points sana maana barabara ni ndogo afu Ina mzigo wa magari ya IT, malori maelfu, mabasi na magari madogo na ya kawaida . Kibaya zaidi barabara ni ndogo na ni mbovu .

Kuanzia Shamwengo Hadi Mlima nyoka ni Kama machinjio pananuka damu za walipa Kodi wanaokomolewa makusudi.

Nilishauri hii barabara waihanishie kule chini malori yajitenge maana ni mengi na ndio yanayokata breki na kuua watu Kila Wakati.

Yaani ni mengi yakusema ila ukweli inatisha sana, mbunge wetu mwenyewe ni bubu tu maana mlima Iwambi na Inyala kote ni kwake Sasa sijui haoni .


Au kwakuwa wao hupita kwa ulinzi na ving'ora.!!!!
 
Hawana habari kila siku kusifia utendaji wa rais pumbavuu kabisa huku raia wakifa kila siku

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Lakini nadhani Kuna kitu wanaficha, hivi kipi kigumu kumueleza ukweli rais au waziri mkuu ??!

Pili naamini rais anajua huu ukweli wa hii barabara maana spika ni mwenyeji hapa .

Kiukweli sijui naweza pata wapi namba ya raisi nimfowardie hiki Kilio maana it's too much .

Leo watu wamekufa hatujui nani anafuata maana sote tunaitumia hii barabara
 
Mkuu, tujitahidi kuandika machache yanayo eleweka, mengi mno.
Nimekuelewa sana ndugu japokuwa niliandika ombi , pendekezo na ushauri kwa kuwa ni mwenyeji wa haya Maeneo ndio maana nimeandika kuwa wajitahidi kuhamisha malori kwa kuyajengea njia Yao kule chini itengane na hii ya njia ya Sasa.

Lkni nimekuelewa sana
 
Nimepita hapo siku si nyingi, hiko kipande cha Ilongo mpaka Uyole na Kedeghe mpaka Mbalizi ni hatari mno.

Barabara nyembamba na miteremko ni mikali. ?Malori makubwa, ma-bus yaendayo kasi, gaei ndogo, bajaji na pikipiki vyote humohumo.

MUNGU tu huwa anatuepusha. Serikali ifanye jambo pale, tena mapema.
 
Kila ajali inayotokea lazima umhusishe kinana, kuwa makini na maneno yako ndugu traffic, watakukamata wakusweke ndani 😅
 
Kinatokea kijitu kinasema askari warudi barabarani kumbe ni kipiga deal ya rushwa kumbe ajali nyingi ni ubovu wa miundombinu

 
ukiwa mtumiaji wa barabara na unapaswa kujua kitu kinaitwa Defensive driving...

Hapo ambapo eneo ni finyu madereva wanapaswa kwenda mwendo mdogo na kuwa na tahadhari na kuacha uzembe....
Tatizo la hili eneo sio Mwendo. Tatizo ni mteremko na Mlima kuwa mkali pia ufinyu wa Barabara, barabara kuwa mbovu na zaidi barabara Ina magari mengi kuliko uwezo wake .

Inahudumia magari ya Kila namna, makubwa kwa madogo ya mizigo na ya abiria .

Yaani kwa ujumla panatakiwa hatua za haraka sana maana Hali ni mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…