Ajali mbaya Inyala Mkoani Mbeya, idadi ya waliofariki yafikia watu 19

Pole kwa wafiwa, pole kwa majeruhi

Ila next time picha muhimu mkuu wengine hawapajui wanapasikia tu

Nawasilisha..
 
Bila serikali kufanya jambo TUTAKOMA .

Barabara inatisha sana hii .

Yaani solution ni kuijenga kubwa kuanzia Ilongo Hadi Mbalizi na pili malori kuhamishwa njia Yao kwenye hii milima
 

Pamoja sana mkuu, umefanya vizuri, naamini litapokelewa na kufanyiwa kazi.
 
Hivi hakuna orodha ya majina ya waliofariki?
Walau tuwajue....
Kiukweli ilikuwa ngumu kuyajua maana Ile gari ya abiria ilikuwa inatoka mbeya kwenda njombe na kama ujuavyo polisi na Sheria zao.

Kama tu pale watu wameshuhudia vifo vingi sana lkni RPC anasema watu nane tu
 
Pole kwa wafiwa, pole kwa majeruhi

Ila next time picha muhimu mkuu wengine hawapajui wanapasikia tu

Nawasilisha..
Ok kaka .
Lkni kwa kifupi ukiwa unaingia mbeya ukishafika mpakani mwa wilaya mbarali na mbeya Kuna sehemu panaitwa Ilongo.

Sasa kuanzia hapo ndio mlima huanzia Hadi mlima nyoka ambapo ndio unakuwa unaingia ndani ya Jiji la mbeya .

Yaani kwa kifupi kata yote ya Inyala na Itewe ndizo zinapitiwa na huu mlima
 
Yes man, miundombinu ndio chanzo na pili ubovu wa haya magari maana ule mlima unahitaji gari Zima lenye break imara hasa likiwa na mzigo
 
Nimeshapaelewa
 
Nimepita maeneo hayo juzi, hakika Ni eneo korofi sana, serikali iangalie namna ya kudeal na maeneo haya kuanzia uyole , nanyala hadi hapo inyala
 
ukiwa mtumiaji wa barabara na unapaswa kujua kitu kinaitwa Defensive driving...

Hapo ambapo eneo ni finyu madereva wanapaswa kwenda mwendo mdogo na kuwa na tahadhari na kuacha uzembe....
Cha ajabu dereva wa bus au Lori anapita hapo kila siku ila akipata ajali atasema Kona Kali,muinuko mkali kana kwamba Kona hio au muinuko umetokea ghafla!
 
Serikali ipanue barabara ziwe angalau tatu kama wameshindwa kabisa kuzifanya nne.
Watu wanamalizwa kwa ajali wajameni!
 
Hadi wahusika waje kutekeleza hilo hiyo ardhi hapo itakuwa imekunywa damu ya kutosha.
Very sad
Ni kweli kabisa. Napafahamu mahali hapo ni barabara ya hovyo kupata kutokea. lakini pia wangepapanua wakaweka na climbing lane na parking ya dharura kwa malori.
 
Wanapaswa wakijifunze huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…