Ajali mbaya, madereva muwe makini

Ajali mbaya, madereva muwe makini

Pumziko La Amani Wapate waliotutangulia.

Kama limeacha njia huenda tairi ilipasuka,au ilichomoka ....au hata Muendeshaji kusinzia.
 
Bila uchunguzi? Kama walipigwa nyundo za vichwa, halafu gari ikasukumizwa huko?
Kwani uchunguzi unachukua wiki ngapi mdau?Unajuaje kama uchunguzi wa miili ulifanyika kabla ya maziko je?Tuache kuwa negative kwa kila linalofanywa na na wengine. Mathalani kabda miili imeharibika vibaya inamwagika ubongo we uiweke tuuu unasubiri uchunguzi kweli!??
 
Hizo pajero ni class moja na akina LC na Nissan Patrol lakini pajero haina ubavu wa kupambana nazo.Hata bei yake sokoni Iko chini
Dah... Mzee Kigogo hebu pitia kidogo performance za haya magari...ukubwa wa injini.....ulaji wa mafuta...na uchafuzi wa hewa....Kisha pitia kipimo cha zamani cha magari jamii yake.... Paris - Dakar....Kisha uje kukana maneno yako 🤣🤣🤣🤭
 
Wasamaria wema wamesaidia kutoa tairi lisiungue
Kwenye ajali kama hii kuhoji kwa nini hakuna tairi ni ukorofi tu.

Maana uwezekano wa tairi kuchomoka kutokana na vishindo vya kukita chini ni mkubwa tu.
 
Ushawahi kuendesha au kukutana na ile Pajero ya CC3500 V6 Petrol? Zile ambazo TRA walikuwa nazo 2005? Ukigusa ile utaheshimu Pajero.
Dah....bahati mbaya hakuta kuwa na Pajero tena.....kiwanda kinafungwa....RIP Pajero 🤭
 
Juzi juzi tena kuna basi nyekundu jina halikuonekana iligongana na Fuso watu 5 wakapoteza maisha. Hio Habari ilikuwa Kwenye muhtasari wa taarifa ya Habari Itv Lakini kwa Mshangao hawakuileta hio Habari .

Nashauri jeshi la trafiki wawekeze Kwenye drones Katika barabara za mijini na za kwenda mikoani zibaini wavunjifu wa sheria za barabarani
 
Dah.... Labda aliposema performance Kali ndiyo kajichanganya...hakuelezea...lakini M/Pajero naikubali sana....na... imekuwa na best performance kwa kundi lake mara nyingi zaidi kuliko gari lolote. 🤣🤣🤣🤣🤭
😄😄😄 Kwny Dakar rally kale ka short chasis ka Pajero kameshinda Sana mzee.Hapo sina ubishi
 
Mwenyewe nimeshangaa sababu hata kale kaji Opa kangu on full speed kanakamua horses zaidi ya hizo! Pajero toka lini ikawa performance car?

Hio ni gari ya Towing zaidi sababu torque yake ni kali ila sio speed!
😄😄😄 nimeliendesha Sana Hilo Gari,halina maajabu kabisa kwny performance Ila lilikua tamu kwny kunesa nesa mzee.
 
Uko sahihi sana. Mara nyingi watu wanatumia usemi "Aa, mungu yupo tutafika salama!" Mungu Mwenyewe anasema:"Hapendi kujaribiwa!" Siku zote Huwa hamsaidii mtu mzembe.

Yaani unakuta dereva hajaangalia upepo wa matairi wiki kadhaa au shock ups zote zimeisha au unakuta katika mtikisiko wa gari kila kukicha bolts zinalegea

Ni uzembe na ushamba wa wengine kuwa na gari ingali hajui hata service inahitajika lini

Na Mabasi hivyo hivyo yaani vyombo vya usafiri vyote
 
Uko sahihi juzi naelekea sehemu gari imezingua wakajifanya mafundi wakafunga kamba sijui nini...kila tukisogea gari inasumbua mbona hatukufika....yaani madereva wanachukuliaga poa sana but mwisho wa siku mambo yanaharibika!

Kweli kabisa nawajua hao wanaojifajya wajanja kumbe wajinga
Mimi hata bulb kama haifanyi kazi lazima nibadili kabla ya safari

Sasa unakuta Bus limekata spring halafu mpumbavu mmoja anashuka na kamba anaanza kufunga
Yaani hilo gari linatakiwa lisuendelee na safari mpaka lisukwe upya

Bado madereva wanahitaji elimu ya theory kabla ya practical
 
Yaani unakuta dereva hajaangalia upepo wa matairi wiki kadhaa au shock ups zote zimeisha au unakuta katika mtikisiko wa gari kila kukicha bolts zinalegea

Ni uzembe na ushamba wa wengine kuwa na gari ingali hajui hata service inahitajika lini

Na Mabasi hivyo hivyo yaani vyombo vya usafiri vyote
Uko sahihi sana. Ila bado unaweza kufanya hayo yote na bado ukapata ajali tu.Uko barabarani anatokea mlevi mmoja na bodaboda yake unamkwepa hamad uko mtoni ajali tayari. Haya mambo ni kuomba Mungu tu
 
Uko sahihi sana. Ila bado unaweza kufanya hayo yote na bado ukapata ajali tu.Uko barabarani anatokea mlevi mmoja na bodaboda yake unamkwepa hamad uko mtoni ajali tayari. Haya mambo ni kuomba Mungu tu

Hapo uko sahihi kabisa
Ajali zinatokea sana na kwa njia tofauti ila yote hayo ni makosa ya wizara ya ndani ambayo haitendi haki katika usalama wa watu barabarani

Huyo mlevi asingekuwa barabarani kama hakuna Rushwa

Mlevi ingekuwa anashikwa kalewa na sheria ni kumfungia miaka mitatu leseni na faini 1m hapo wengi wangeacha kuendesha wakiwa wamelewa

Nakumbuka kuna siku miaka ya nyuma nimeingia mwanza nimechoka na gari nikaiacha hotel isafishwe
Nikaamua kupanda bus kuelekea mahali kuwaona ndugu
Kupanda lile mini bus likawa linayumba traffic akasimamisha akaingia ndani akamkuta dereva kalewa vibaya sana

Alichosema sikuamini
Aah na wewe Fulani umezidi sasa wee konda hebu shika usukani mwache akae nyuma huyo

Sio hadithi hii nilishuhudia kwa macho yangu

Sasa hapo akigonga au kutuangusha kwenye mtaro kosa la nani? [emoji1986]
 
Back
Top Bottom