TANZIA Ajali Mbeya: Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamefariki dunia

TANZIA Ajali Mbeya: Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamefariki dunia

Mkuu nilikuwa najiuliza kwanii serikali iko kimya juu ya maeneo hatarishi!

Kila siku ajali zinatokea maeneo yale yale, Je kamatai ya Taifa ya usalama barabarani hawaoni hili.

Kitu kingine ambacho ni mzizi hasa kwa Dar es Salaam, Je wameshindwa kubuni njia ya kupunguza ajali hasa maeneo ya mataa yanapokuwa yamezima mfano.
Barabara ya morogoro road maeneo ya taa za Bucha, Baruti Suka ni maeneo ambayo hazipitu siku mbili bila mtu kugongwa au magari kugongana!

Tunahitaji kuja na suluhisho la kudumu kwa maeneo haya, watu tunateketea kila uchwao.

Vyuo kama DIT, St joseph, CoET, MUST, Arusha Tech, VETA mko wapi kuja na suluhisho la taa zinazo dumu!
Vyuo vingi ni teaching oriented na siyo research oriented,hivyo unakuta siyo rahisi kufanya tafiti yakinifu,na kuja na suluhisho lenye tija kwa jamii.Pole kwa waathirika wa hiyo ajali.
 
Kwanini serikali ya CCM haitaki kutanua barabara maeneo hatarishi mkoani Mbeya?

Ajali isipotokea Inyala, inatokea Mlima Nyoka, isipotokea hapo inatokea mteremko wa Mbalizi, lakini serikali inachukulia poa tu miaka nenda rudi.
Huwa yanafanyika maombi kuombea ajali zisitokee.
 
Wajameni tunatoa comment ambazo haziendani na uhalisia wa ajali, sio sawa! Kama hujui bora ukae kimya au toa tu pole !
 
Kwanini serikali ya CCM haitaki kutanua barabara maeneo hatarishi mkoani Mbeya?

Ajali isipotokea Inyala, inatokea Mlima Nyoka, isipotokea hapo inatokea mteremko wa Mbalizi, lakini serikali inachukulia poa tu miaka nenda rudi.
Makamu wa Rais alikua hapo inyala juzi kukagua/barabara mpya kukwepa huo mlima. Mbalizi tayar wameanza kujenga barabara kukwepa mlima sina uhakika na mlima nyoka
 
Hakuna magari naogopa kuongozana nayo niwapo safarini na private kama malori na mabasi!
Hatari sana mzee wangu hasa mabus, muda wowote wanaforce kuovertake na muda wowote wannaforce kurudi kama mbele kuna kizingiti, na ukisema ukomae wanakugonga kabisa. Malori mengi case zao ni kama hizo wakifeli brake au gari likose muelekeo ni hatari sana
 
Watu wanakufa sana kwa ajali sema wengine hawatangazwi tu.
Jumamosi kuna kijana mdogo tu kagongwa na gari ndogo kwenye barabara ya mwendokasi pale Kinondoni B wakati anavuka akapande Mwendokasi.

Kile kifo kinauma kwa sababu kijana wa watu alikuwa hana kosa ila huyo dereva alikuwa spidi kali sana.
 
Back
Top Bottom