Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ni pamoja na barabara zetu kutokuwa za kiwango cha Kimataifa, ubovu wa magari, madreva kutozijua sheria za barabarani.

 

asante kwa ujuzi huu wa tekenolojia nadhani pia wahusika wamekusoma na wataitumia ili kudhibiti ajali zitokanazo na mwendo kasi ingawa si kila ajali inasababishwa na mwendo kasi
 
Dereva asaini kuwa simu inatrack mwendo? Dereva gani akubali
 
Hayo ndio mambo muhimu ya kupewa kipaumbele kwanza.. Hii habari ya mwendokasi hatutaweza kupambana nayo kwa haraka hivi..

Ni pamoja na barabara zetu kutokuwa za kiwango cha Kimataifa, ubovu wa magari, madreva kutozijua sheria za barabarani.
 
Naunga mkono hoja. Hao wanaotetea ni miononi mwa wanaofikiri ari ni kishada
 

Dah natamani umpokee pr dr kwa miezi michache iliyobaki ili utimize
 
Watanzania inabidi tuwe analytical zaidi ya kuwa na majibu mepesi kama suluhisho la ajali barabarani. Usalama bararani ni idara kama zilivyo idara zingine za serikali kwa hiyo haitatarajiwi iwe bora yenyewe tu kama kisiwa, Kwani idara ipi Tanzania inayofanya vizuri zaidi ya hii? Je ni afya? yawezekana watu wanaokufa mahospitalini kwa uzembe,kukosa dawa au pesa za kulipia matibabu ikawa kubwa kuliko wa ajali za barabara.Vilevile wangapi wanadhulumiwa ardhi?angalia migogoro ya wafugaji na wakulima,wangapi wako magereza au polisi bila makosa?Escrow, EPA na mengine.Wazembe sio madereva tu wako kila sekta tofauti ni impact tu zingine hazionekani kwa haraka ila ni mbaya sana kuliko hata za madereva. Ajali ni matokeo ya corrupt system.
 

Kuwafukuza kazi watu usalama barabarani utakua umetumia nguvu badala ya akili, hata kuwalipisha na kuwafunga jela madereva utawaonea maana vyanzo vya ajari hata serikali inahusika kwa sababu kuna barabara nyingi sana mbovu
 

Hapo kwenye red umeongea mkuu......umesahau na hili la ufinyu wa barabara, na mwendo kasi kwenye kona...
 

Mkuu' hizo ndio simu utakazosikia zinaongoza kwa kuharibika na kuishiwa charge' waanzishe tu hako kamchezo mafundi simu wengi watafahamiana sana na madereva wa mabasi
 
Tufanye sasa tayari sheria ulizoziainisha zimepitishwa halafu mimi ndo kamanda usalama barabarani mathalani Dodoma.

1.Ikibainika dereva wa basi alikuwa speed inayozidi 40km/hr abiria mtaumia aisee mtakula bakora za kutosha na dereva ananyang'anywa leseni.Dar-Mza siku mbili.

2.Dereva akibainika amelewa,anaswekwa lupango miaka mitano(hakuna msamaha wa rais) na kufanyishwa kazi ngumu.

3.Ikitokea ajali na watu wakapoteza maisha,mmiliki wa hicho chombo atapaswa kuwalipa fidia(actually kifuta machozi) 80mil kila marehemu na 200mil kwa majeruhi wenye ulemavu wa kudumu kama kisababishi cha ajali ni ubovu wa chombo au uzembe.

4.Kama chanzo cha ajali ni ubovu wa chombo basi dereva,makenika,mmiliki watakuwa answerable NB hizi kesi haziendi mahakamani ni kitengo kinakuwepo maalumu kwa ajili ya ajali.

5.Mabasi yote na malori ya usafirishaji hayataruhusiwa kuwa barabarani yakitembea 300,000km

6.Madereva wa malori na mabasi wawe na elimu ya kidato cha sita na kuendelea na lazima awe na uzoefu wa 10yrs bila ajali ndo akabidhiwe gari kwengine.

7.Bodaboda akipata ajali kama abiria hajafa basi anapewa yeye hiyo pikipiki na unamlipa fidia na bakora unakula.

8.Basi likifika stendi kabla ya mda uliopangwa abiria mnatoa maelezo na bakora juu.

Nitaendelea.......
 
Ndugu wanaJF, Salam.
Takribani mwezi mmoja sasa, ajali za barabarani zimeongezeka kwa kasi kubwa na zinasababisha vifo na vilema vya kudumu kwa watanzania wenzetu.

Ongezeko hili linaacha maswali mengi kiasi cha kushindwa kuyapatia majawabu stahiki.
Mfano; (a). Ongezeko hili ni kutokana na kuingizwa kwa magari mabovu barabarani?.
(b). Ongezeko hili ni kutokana na kuajiliwa kwa madereva wasio na uzoefu?.
(c). Ongezeko hili ni kutokana na mivutano ya kimasirahi(mikataba & posho) kati yadereva na boss wake?.
(d). Ongezeko hili ni matokeo ya ongezeko la askari wa usalama barabarni?.

Kwa jumla, ni vigumu kupata majawabu stahiki. Kwa sababu hiyo, naombeni michango yenu, nini kifanyike kunusuru maisha ya watanzania?.

Mod, uzi huu ni mhimu kwa maisha ya watanzania. Please, naomba msiufute ama kuunganisha na zingine hapa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…