Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Nakushukuru sana kwa mchango wako mzuri na kwa maono hayo. Madhara ya RUSHWA NA UZEMBE KWA WANANCHI NA VIONGOZI WOTE YATALITAFUNA TAIFA HILI KWA KIWANGO KIKUBWA SANA HASA WAKATI HUU AMBAO HUWEZI KUKOSOA. NAHISI KAMA BADO SANA HATUJA-EXPERIENCE HAYO MADHARA KWA KIWANGO KIKUBWA, NAAMINI YATAKUJA MAKUBWA SANA KULIKO HAYO TUNAYOYAONA LEO.
 
Tunaosafiri kila siku kwenye haya mabasi tunaona mengi! Spidi inayokanyagwa baada ya tochi ni shida,dereva saa kumi yupo macho anakaa kwenye uskani kuanzia Mwanza hadi Dar what next? Unakuta gari chakavu kabisaa hadi nyuzi za matairi zinaonekana gari hiyohiyo inapita kwa matrafki,mizani n.k asee! Mambo ni mengi unaweza jaza lambat!
 
Uzembe kwa kiasi kikubwa unaweza ukadhibitiwa na abiria.. Kwa mfano overtaking kwenye eneo la hatar, michezo ya madereva, mwendokasi, hivi vyote hakuna askari wala mfanyakazi wa sumatra wala mtu wa mamlaka nyingine yeyote ile anaweza kuviona ila ni abiria.. Abiria tupo kimya na tunafumbia macho haya mambo.. Binafsi nawalaumu sana abiria.. Je watu ambao walishawah kuona michezo kama hiyo ya kubadilishana njia walishawahi kutoa taarifa..? Mpaka gar inapigwa tochi speed 122 je humo ndan hakuna abiria??? Ni upuuz wa sisi wasafir ukijumlisha na dereva... Sio suala la kublame serikali.. Serikali itahusika pale tu patakapokua na ubovu wa miundombinu kwa mfano mashimo barabarani.. Huo ndo mtazamo wangu
"Msiba usikie kwa jirani" co JILANI
Kweli kabisa umenena mkuu
 
Tunaosafiri kila siku kwenye haya mabasi tunaona mengi! Spidi inayokanyagwa baada ya tochi ni shida,dereva saa kumi yupo macho anakaa kwenye uskani kuanzia Mwanza hadi Dar what next? Unakuta gari chakavu kabisaa hadi nyuzi za matairi zinaonekana gari hiyohiyo inapita kwa matrafki,mizani n.k asee! Mambo ni mengi unaweza jaza lambat!
Tunachukua hatua gan
 
Nakushukuru sana kwa mchango wako mzuri na kwa maono hayo. Madhara ya RUSHWA NA UZEMBE KWA WANANCHI NA VIONGOZI WOTE YATALITAFUNA TAIFA HILI KWA KIWANGO KIKUBWA SANA HASA WAKATI HUU AMBAO HUWEZI KUKOSOA. NAHISI KAMA BADO SANA HATUJA-EXPERIENCE HAYO MADHARA KWA KIWANGO KIKUBWA, NAAMINI YATAKUJA MAKUBWA SANA KULIKO HAYO TUNAYOYAONA LEO.
Hatar sana
 
Habari za asubuhi wana JF?

Heri ya siku kuu ya Eid kwa waislamu wote na wasio waisilamu..

Wakuu nina wazo,
Naomba tuishauri serikali na ikiwezekana tufanye demonstration kuhamasisha hili;

Kulingana na uzembe wa madereva wetu wengi ambao zaidi ya 95% ni wanaume, kumekuwepo na ajali nyingi sana katika mabasi yetu yanayoenda masafa marefu, yani kms 500-1400, hili linatokana na uzembe wa kutofuata alama za barabarani, mwendokasi above limits, ulevi na uzembe mbalimbali..

Serikali imetoa maonyo, watu wamefutiwa na kufungiwa leseni lakini wapi.. bado ajali zinateketeza roho za watanzania kila kukicha..

Kiini cha thread:
Wakuu, naomba niongee kiufupi hapa ili ninyi muongezee kwa urefu maana mko wengi sana.
Naiomba serikali sasa ione umuhimu wa kuwapa kipaumbele wanawake ambao watakuwa super trained wawe makomandoo wetu watakaotuokolea roho za watanzania.
naamini kabisa hakutakuwa na mwanamke atakaefanya mzaha wa hovyo barabarani, naamini hivyo.

Wakuu, tuwaamini wanawake, watatupunguzia ajali maana wanaume tumezidi uzembe kwa kisingizio cha bosi kutaka gari mapema kumbe ni vice versa.

Karibuni mjadalani,
 
Tatizo ni Mamlaka wangeruhusu angalau gari litembee mwisho speed 120 halafu utengenezwe mfumo wa ku punch kadi kila baada ya vituo lakini hivi sasa wanakagua asubuhi tuu shughuli mchana hivyo ajali hazichangiwi na madereva zinachangiwa na MUDA
 
kuna basi linaitwa ndenjela la dar - mbeya dereva mwanamke.. linasafiri mwendo mzuri sana...

mimi nasapot hoja
Kuna Yule aliyekuwa anaendesha Shabiby sijui bado yupo! Ni wazo jema Ila Mimi naona ratiba ziwe tight tu
 
Tatizo ni Mamlaka wangeruhusu angalau gari litembee mwisho speed 120 halafu utengenezwe mfumo wa ku punch kadi kila baada ya vituo lakini hivi sasa wanakagua asubuhi tuu shughuli mchana hivyo ajali hazichangiwi na madereva zinachangiwa na MUDA
Mkuu basi speed inayoruhusiwa ni mwisho 80/kwa saa,sasa hiyo 120?
 
Unajuaje kama wanawake wakiendesha Mabasi ajali za kizembe zinaweza kupungua?
Si ajabu ajali zinaweza zikaongezeka coz wanawake wengi wana asili ya uoga fulani,anaweza hata akalipindua basi kwa uoga tu kabla ya ajali yenyewe,

Mimi nafikiri udereva wa mabasi ya abiria ungewekewa sheria angalau dereva awe na umri usiopungua miaka 35 coz huo umri akili inakua imekomaa kiasi.

Huo ni mtazamo wangu tu.
 
Suluhisho ni kutengeneza mageti/ vizuizi kila baada ya kilometer chache... hii itasiadia siyo tu mabasi bali na safiri zote kutembea kwa mwendo sahihi... kitakacho wanyosha madereva ni ule usumbufu watakaoupata...
 
Hivi nchi nyingine ajari hazipo?. Hivi watu tanzania wanakufa kwa ajar za magar tuu? Ndo uzembe ulipo tuu,nenda viwandani uone watu wanavyopata ajari...kukatika mikono,miguu;viwanda vya nondo na nabati...nenda viwanda vya cement (silence killer)mahospitalini;wanaokufa kwa kutoa mimba.nk...mbona ndege zinapata ajar..pikikipik. nadhani tatizo la training na nidhamu tu kwa wakufunzi...
 
Hahahaaaa! Naona "Conductor" unatetea kibarua kwa jazba.
 
Kwani wanaume kuwa madereva ilifanyika wapi demonstration ili tupate maana ya kufanya kwa upande wa wanawake nao wawe madereva?
 
Naunga mkono hoja 100%. Najazia kidogo, tuliona speed gavana zilivyopita baada ya watu kupiga pesa zao, tuliona zilivyochokonolewa na Watazania haohao ambao ilikuwa salama yao au ndugu zao, tuliona rushwa ilivyofifisha utendaji wake. Kuna difu ambazo ndio kipimo cha mwendo wa chombo husika, hizi ndio hukontroo mwendo wa chombo, kama kweli Serikali inania ya kweli ktk kuzibiti ajali basi mabasi yote ya mikoani yafungwe difu hizi kwa kuzibiti ajali zitokanazo na mwendo kasi.
 
Mkuu hoja nzuri Ila zingatia haya:
1. Mimba changa (mwezi 1-miezi 3)
2. Tumbo ghafla Yale ya kila mara
3. Kunyonyesha
4. Stress za kupigwa kibuti
5. Kujipodoa kila stand au njiani.

Wengine wataingeza
 
Kwa wanawake wanavyopenda kusifiwa sidhani kama hili ni suluhisho kwani wengi wao hawatakubali kupitwa na wanawake wenzao hovyo hovyo barabarani.
Mimi naona sheria zitiliwe mkazo na adhabu kali zitolewe kwa makampuni na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani!
 
Hahah, umenichekesha.
Nikavuta picha watakavyokua wanashindana
 
Back
Top Bottom