Habari za asubuhi wana JF?
Heri ya siku kuu ya Eid kwa waislamu wote na wasio waisilamu..
Wakuu nina wazo,
Naomba tuishauri serikali na ikiwezekana tufanye demonstration kuhamasisha hili;
Kulingana na uzembe wa madereva wetu wengi ambao zaidi ya 95% ni wanaume, kumekuwepo na ajali nyingi sana katika mabasi yetu yanayoenda masafa marefu, yani kms 500-1400, hili linatokana na uzembe wa kutofuata alama za barabarani, mwendokasi above limits, ulevi na uzembe mbalimbali..
Serikali imetoa maonyo, watu wamefutiwa na kufungiwa leseni lakini wapi.. bado ajali zinateketeza roho za watanzania kila kukicha..
Kiini cha thread:
Wakuu, naomba niongee kiufupi hapa ili ninyi muongezee kwa urefu maana mko wengi sana.
Naiomba serikali sasa ione umuhimu wa kuwapa kipaumbele wanawake ambao watakuwa super trained wawe makomandoo wetu watakaotuokolea roho za watanzania.
naamini kabisa hakutakuwa na mwanamke atakaefanya mzaha wa hovyo barabarani, naamini hivyo.
Wakuu, tuwaamini wanawake, watatupunguzia ajali maana wanaume tumezidi uzembe kwa kisingizio cha bosi kutaka gari mapema kumbe ni vice versa.
Karibuni mjadalani,