Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Kwa sheria za barabarani Dar Mbeya siku 3!

Matoke ya kutozingatia sheria za barabarani tunayaona ambayo ni ajali na vifo. Ni ajali chache sana ambazo husababiwa na hitilafu ya gari siku hizi. Nyingi ni makosa ya madereva wenye hizo akili za taiming.
 
Matoke ya kutozingatia sheria za barabarani tunayaona ambayo ni ajali na vifo. Ni ajali chache sana ambazo husababiwa na hitilafu ya gari siku hizi. Nyingi ni makosa ya madereva wenye hizo akili za taiming.
Wewe unaesema sheria 100% unaweza kwenda Mbeya siku 2. Nilishawahi kusafiri kutoka Dar-Moro masaa 5.30, kwa speed za sheria 50-80kph, watu njia nzima wanalalamika. Kwenye hii assessment, tuweke kila kitu mezani, speed 50-80 ni ndogo sana kwa safari ndefu.
 
Mawazo ya karne ya 14 ndiyo sababu kubwa ya ajali za mara kwa mara. Kwenye nchi zilizoendelea wamepunguza au kumaliza kabisa ajali kwenye barabara kuu kwa kuongeza ufanisi barabarani. Nyie wenzetu huwa mnajifunza kutoka wapi? Speed ya interstate/freeways kwenye majimbo mengi huko Marekani ni 70/Mile per hour. Je hizo ni km ngapi kwa saa??? nyie badala ya kuongeza ufanisi na kuweka kiwango cha spidi ambacho kinawezesha madereva wasafiri kwa haraka na kuondokana na uwezekano wa kulazimika ku-overtake mara kwa mara, mnazidi kupunguza speed na huku mkiruhusu watu kuendelea kujenga karibu na barabara, na nyie kuendelea kukusanya kodi kupitia speed za 50km/hr! Mnaendelea pia kujenga matuta kila mahali ili kudhibiti mwendo... Mnafikiri kinyumenyume kila siku, hivyo ajali zitaendelea kutokea mpaka mtakapo anza kufikiri nje ya hayo mabox yenu.
 
Katika gazeti hili Jumapili iliyopita, tulikuwa na habari iliyosema, ‘Sababu za mwezi Desemba kuwa na mauaji, ajali nyingi.’

Habari hiyo ilielezea kwa kina jinsi ambavyo mwezi huo hugubikwa na matukio ya uhalifu, ujambazi na vifo vitokanavyo na ajali na mauaji na kuelezea kuwa sasa yanaonekana kuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku kiasi kwamba kila msimu wa mwisho wa mwaka ambao huambatana na sikukuu mabalaa haya yanaonekana kama ni wakati wake.

Zimeelezwa sababu kadhaa za matukio hayo yanayogharimu maisha ya watu wengi na wengine kuachwa na ulemavu wa kudumu zikiwamo za ulevi, mwendokasi barabarani na kutafuta fedha kwa njia zisizo halali ili kuzitumia wakati wa sherehe.

Siku moja baada ya habari hiyo, imeripotiwa ajali mbaya iliyosababisha vifo vya watu tisa na wengine 18 kujeruhiwa katika eneo la Ifunda mkoani Iringa wakati lori lilipogonga gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace.

Ilielezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace hiyo iliyokuwa imeegeshwa pembeni mwa barabara.

Licha ya kauli za viongozi wa dini, wanasaikolojia na vyombo vya usalama kueleza sababu za ongezeko la ajali, uhalifu na vifo mwishoni mwa mwaka kwamba chanzo chake ni pilikapilika za sikukuu na harakati za kujiongezea kipato, tunadhani ipo haja kwa wamiliki wa vyombo vya moto, madereva, abiria na wasimamizi wa usalama barabarani kwa maana ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, kila mmoja kutimiza wajibu wake.

Kama alivyosema mwanafalsafa nguli wa Ujerumani, Albert Einstein katika moja ya nukuu zake ajwadi kwamba ni ukichaa kufanya jambo hilohilo tena na tena na kutegemea matokeo tofauti.

Kila mwaka tumekuwa tukisikia matamko mbalimbali ya kututahadharisha na ajali za mwishoni mwa mwaka, lakini inavyoonekana tatizo hilo bado ni kubwa.

Njia mbalimbali zinazochukuliwa na polisi wa usalama barabarani zinaonekana kwamba bado hazijazaa matunda hali hiyo inatuonyesha kwamba tunapaswa kubungua bongo zaidi na kutafuta suluhisho la kuepusha ajali.

Tunadhani kwamba moja ya njia zinazoweza kutuondoa katika janga hili ni kuwekeza katika utoaji wa elimu hasa kwa madereva wanaoendesha magari ya abiria na mengine makubwa. Wakielimishwa inavyostahili juu ya matumizi sahihi ya vyombo vya moto na barabara, tuna imani kwamba ajali hizi zitapungua kwa kiwango kikubwa.

Lakini pia tunadhani kwamba ipo haja kwa wamiliki wa magari hasa ya masafa marefu kuhakikisha kwamba kunakuwa na madereva zaidi ya mmoja kwani imeripotiwa mara nyinyi kwamba chanzo cha baadhi ya ajali ni madereva kusinzia kutokana na uchovu.

Ifike mahali kila mmoja wetu ajione kwamba ni mhusika katika kuhakikisha kwamba vyombo vya moto vinakuwa salama wakati wote lakini kikubwa zaidi kama tulivyosema, elimu ndiyo jambo muhimu zaidi kabla hata ya kufikiria adhabu ya faini kwani inavyoonekana matunda yake hayajaonekana.

Inawezekana kabisa kupunguza ajali hizi kama kila mmoja wetu atachukua tahadhari.


Chanzo: Mwananchi
 
NDUGU WATANZANIA

Kwanza Kabisa natanguliza POLE yangu kwa wazazi, Ndugu, Jamaa, na Marafiki wa Wafiwa wote na popote pale walipo, ndani na nje ya Tanzania. Huu ni MSIBA wetu sote, na kama ni mapenzi ya Mungu, basi WATANZANIA wote kwa wingi wetu tujumuike na Ndugu zetu Arusha ili Kuiaga miili ya MALAIKA HAWA kwa UPENDO MKUU.

PILI. Tuangalie janga hili kwa jicho la tatu, na tutafakari kwa makini ni nini chanzo cha Ajari hii, na nini kifanyike ili kuepusha vifo vya watoto wengi kiasi hiki.
Ajari ni ajari, lakini imetokea vipi na nini kilifanyika kabla ya ajari kutokea, ama ni jitihada gani zilifanyika ili kuzuia ajali isitokee au kupunguza makali ya ajari kwa abiria ni JAMBO muhimu la kuzingatia na kuliongelea, na kulitolea majibu ili kukomesha,kuzuia, au kupunguza vifo vya watoto wetu.

Kwa hapa Tanzania, MWENDO KASI ni tatizo kubwa sana. Hili ni janga la Kitaifa. Hapa Tanzania hakuna barabara (Highways) ambazo zinafaa ama zinaruhusu magari kwenda kwa mwendo kasi bila kusababisha ajari barabarani. Barabara zetu nyingi ni nyembamba sana zilizo na kona nyingi ambazo ni hatarishi hasa kwa madereva wageni kwenye njia husika.

Uzoefu wa safari ndefu kwa madereva wengi pia ni tatizo. Ajari nyingi hutokea au usababishwa na uzoefu mdogo wa dereva kuendesha gari kwa umbali mrefu. Utakuta dereva wa daladala Dar, anakodishwa apeleke watu msibani Musoma au Bukoba au,Mbeya. Huyu dereva hana uzoefu wa safari ndefu, wala njia yenyewe haijui. Na wakati mwingine hata gari yenyewe haifai kwa safari ndefu, lakini kwasababu ya wakodishaji kutaka usafiri kwa bei chee, na mmiliki wa chombo kutaka kupata pesa ya haraka haraka, utakuta ajari nyingi hutokea kwa sababu ambazo zingeweza kuzuilika.

Kingine ni UZINGATIAJI WA USALAMA WA ABIRIA NDANI YA VYOMBO VYA USAFIRI. Kusema ukweli, kwa hapa Tanzania abiria ni sawa na mzigo tuu kwa mtazamo wa wamiliki wengi wa vyombo vya usafiri. Ebu niulize, je, ni daladala gani ambalo lina mikanda ya usalama kwenye viti vya abiria?
Au, niulize, je, ni abiria wangapi wapo tayari kukataa kupanda bus la kwenda mikoani au daladala eti kwasababu tuu, hakuna "safety seatbelt "?

IT COULD HAVE BEEN AVOIDED.
Kwenye ajari iliotokea Karatu, swali la kujiuliza ni moja tu; JE, WANAFUNZI HAWA (WATOTO WETU) WALIFUNGA MIKANDA YA USALAMA KWENYE VITI VYAO?
Na kama hawakufunga, ni kwanini hawakufanya hivyo, na ni nani aliruhusu watoto wetu wasafiri kwenye bus bila ya kufunga mikanda ya usalama safarini ndani ya bus lao la shule?

Swali lingine la kujiuliza ni, Hiyo SCHOOL BUS ilikidhi vigezo vya kufanya shughuli za kubeba watoto wa shule na kuwasafirisha kwenye safari ndefu?
Je, hiyo school bus ilikuwa na "safety seatbelt" kwaajili ya USALAMA WA WATOTO WETU?

Je, wazazi wa watoto hao walikuwa na taarifa ya safari hiyo na wakakubali kimaandishi kuruhusu watoto wao washiriki safari hiyo?

IKIWA TUTAPATA MAJIBU YA MASWALI HAYA, BASI TUTAWEZA KUZUIA AMA KUPUNGUZA AJARI, AU VIFO VINGI VYA WATOTO WETU.

NAOMBA WAZIRI HUSIKA NA WATAALAMU WA VYOMBO VYA USAFIRI WATUSAIDIE KUCHUNGUZA,NA KUTOA MAJIBU YA MASWALI HAYA, NA KUTUNGA AMA KUSIMAMIA SHERIA ZA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI KWA WATOTO WA SHULE ZOTE TANZANIA.

MUNGU WAPE NGUVU WAZAZI WA WATOTO HAWA NA UTUSAMEHE SISI WATANZANIA KWA KURUHUSU VIFO HIVI VITOKEE KWA KUTOKUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI, NA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI VYA WATOTO WETU MASHULENI.

AMINA.
 
Tuache kupiga ramli, yaliyo tokea yametokea, maji yakimwagika hayazoleki, tumuombe Mungu atulide, awape wepesi walio umia na kuwapa faraaja waliofiwa. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Bwana ahimidiwe.
 
Je gari lilikuwa na mikanda?, je pre caution measures kabla ya safari inachukuliwa seriously na uongozi wa shule zetu? Madrereva na ubora wa magari ya kubeba watoto, speed nk.
Hili lilikuwa linaepukika, uongozi wa shule usikwepe lawama, kuna watu hawakutimiza wajibu wao.
 
Mkuu kweli umeongea point sana.

Hapo kwenye suala la seat belts hapo watu wengi sana wanapuuziaga, ila wajue kuwa mzungu zio mjinga kubuni hicho kitu. Seat belts ni muhimu sana kwa usalama.

Yaliyotekea hatuwezi kubadili lakini ukweli ni kwamba wangekuwa wamefunga seat belts wasingeteketea wote hao
 
Hizi kauli zinanifanya nisimwamini Mungu wako.. Ati bwana alitoa, Bwana ametwaa, una maana huyo Mungu ndo kaua
 
Tujifunze kutoka hili. Kama nchi zilizoendelea Mfano za Scandnavia (Norway) Maximum speed ni 80 KM/saa na wana super highways na kila section kuna camera kwanini sisi tusiweze. Maisha ya mtu ni ghali yakipotea hayarudi tena!!. Tunakwenda vizuri kwa mabasi makubwa ya mikoani ila sasa ni awamu ya kwa magari yote!! 70KM/saa. No compromise on ones life.
 
Hivi hii ni ajali ya kwanza hapa Tanzania?
safety measures kila siku zinapigiwa kelele. vyombo vya usalama vipo, sisi wenyewe wazazi na walimu na wasimamizi wa abiria na watoto tupo.
na ajali bado zilitokea na zinaendelea kutokea.
 
Kwa muonekano wa ile gar,ni dhahir hawa watoto hawakufunga mkanda,maana haijabondeka saana kwa nyuma..meana walio kaa nyuma wangeweza kusalimika kwa asilimia kubwa
 
Ukishasikia ni ajali basi ukumbuke kuwa AJALI HAINA KINGA!
 
ubovu wa barabara plus matuta/Rasta/Mashimo huchangia kwa 100% ajali za barabarani hapa Tanzania ... Kwanini Highway wanaweka Rasta?
 
Kama ajali haina kinga mbona unavaa condom?
Unavaa condom na bado inaweza kupasuka. Ikipasuka ndipo ajali inapotokea.. ..matokeo yake ni magonjwa au mimba zisizotarajiwa..
Ajali ipo sehemu zote!
 
75% ya ajali zote chanzo chake ni binadamu (human error)
 
Back
Top Bottom