NDUGU WATANZANIA
Kwanza Kabisa natanguliza POLE yangu kwa wazazi, Ndugu, Jamaa, na Marafiki wa Wafiwa wote na popote pale walipo, ndani na nje ya Tanzania. Huu ni MSIBA wetu sote, na kama ni mapenzi ya Mungu, basi WATANZANIA wote kwa wingi wetu tujumuike na Ndugu zetu Arusha ili Kuiaga miili ya MALAIKA HAWA kwa UPENDO MKUU.
PILI. Tuangalie janga hili kwa jicho la tatu, na tutafakari kwa makini ni nini chanzo cha Ajari hii, na nini kifanyike ili kuepusha vifo vya watoto wengi kiasi hiki.
Ajari ni ajari, lakini imetokea vipi na nini kilifanyika kabla ya ajari kutokea, ama ni jitihada gani zilifanyika ili kuzuia ajali isitokee au kupunguza makali ya ajari kwa abiria ni JAMBO muhimu la kuzingatia na kuliongelea, na kulitolea majibu ili kukomesha,kuzuia, au kupunguza vifo vya watoto wetu.
Kwa hapa Tanzania, MWENDO KASI ni tatizo kubwa sana. Hili ni janga la Kitaifa. Hapa Tanzania hakuna barabara (Highways) ambazo zinafaa ama zinaruhusu magari kwenda kwa mwendo kasi bila kusababisha ajari barabarani. Barabara zetu nyingi ni nyembamba sana zilizo na kona nyingi ambazo ni hatarishi hasa kwa madereva wageni kwenye njia husika.
Uzoefu wa safari ndefu kwa madereva wengi pia ni tatizo. Ajari nyingi hutokea au usababishwa na uzoefu mdogo wa dereva kuendesha gari kwa umbali mrefu. Utakuta dereva wa daladala Dar, anakodishwa apeleke watu msibani Musoma au Bukoba au,Mbeya. Huyu dereva hana uzoefu wa safari ndefu, wala njia yenyewe haijui. Na wakati mwingine hata gari yenyewe haifai kwa safari ndefu, lakini kwasababu ya wakodishaji kutaka usafiri kwa bei chee, na mmiliki wa chombo kutaka kupata pesa ya haraka haraka, utakuta ajari nyingi hutokea kwa sababu ambazo zingeweza kuzuilika.
Kingine ni UZINGATIAJI WA USALAMA WA ABIRIA NDANI YA VYOMBO VYA USAFIRI. Kusema ukweli, kwa hapa Tanzania abiria ni sawa na mzigo tuu kwa mtazamo wa wamiliki wengi wa vyombo vya usafiri. Ebu niulize, je, ni daladala gani ambalo lina mikanda ya usalama kwenye viti vya abiria?
Au, niulize, je, ni abiria wangapi wapo tayari kukataa kupanda bus la kwenda mikoani au daladala eti kwasababu tuu, hakuna "safety seatbelt "?
IT COULD HAVE BEEN AVOIDED.
Kwenye ajari iliotokea Karatu, swali la kujiuliza ni moja tu; JE, WANAFUNZI HAWA (WATOTO WETU) WALIFUNGA MIKANDA YA USALAMA KWENYE VITI VYAO?
Na kama hawakufunga, ni kwanini hawakufanya hivyo, na ni nani aliruhusu watoto wetu wasafiri kwenye bus bila ya kufunga mikanda ya usalama safarini ndani ya bus lao la shule?
Swali lingine la kujiuliza ni, Hiyo SCHOOL BUS ilikidhi vigezo vya kufanya shughuli za kubeba watoto wa shule na kuwasafirisha kwenye safari ndefu?
Je, hiyo school bus ilikuwa na "safety seatbelt" kwaajili ya USALAMA WA WATOTO WETU?
Je, wazazi wa watoto hao walikuwa na taarifa ya safari hiyo na wakakubali kimaandishi kuruhusu watoto wao washiriki safari hiyo?
IKIWA TUTAPATA MAJIBU YA MASWALI HAYA, BASI TUTAWEZA KUZUIA AMA KUPUNGUZA AJARI, AU VIFO VINGI VYA WATOTO WETU.
NAOMBA WAZIRI HUSIKA NA WATAALAMU WA VYOMBO VYA USAFIRI WATUSAIDIE KUCHUNGUZA,NA KUTOA MAJIBU YA MASWALI HAYA, NA KUTUNGA AMA KUSIMAMIA SHERIA ZA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI KWA WATOTO WA SHULE ZOTE TANZANIA.
MUNGU WAPE NGUVU WAZAZI WA WATOTO HAWA NA UTUSAMEHE SISI WATANZANIA KWA KURUHUSU VIFO HIVI VITOKEE KWA KUTOKUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI, NA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI VYA WATOTO WETU MASHULENI.
AMINA.