Ajali: Tuambiane ukweli dhahama hili lituepuke

Ajali: Tuambiane ukweli dhahama hili lituepuke

Duhhhhh....
Mkuu umefoka hadi uzi wote umelowa mate..teh🤣
 
Wakati Magufuli anawaambia matrafic wawabane madereva wazembe mkasema ni mshamba!

Mama yenu kupitia kinana akaondoa matrafic barabarani mkashangilia eti anafuta legacy!

Kunyweni damu za wanaofariki sasa!

Mavi matupu nchi hii
 
Waruhusu watu wawekeze kwenye usafiri wa Reli, watu waingize treni za kisasa,nayo itapunguza ajali,wao wawe wajenga miundo mbinu tu, lakini siyo kwa hii selikali ya CCM inayofikiliaga uje uchaguzi ili waibe kura
 
Kwann umesema 80 na sio 70 ama 90 ama 100

Aliekwambia 80 hupati ajali nani
Ninasema 80km/h kwa sababu ndiyo iliyokuwa specified na Tanroads kabla ya Kamanda Muslim kuja na zake za kipolisi.

80km/h zilikuwa zimefikiwa na Tanroads kutokea kwa wajenzi.
 
Shida inaanzia kwenye kuwa na jamii isiyowajibika. Na jamii kukosa uzalendo. Zipo Sheria nyingi sana kulinda ajali zisitokee lakini zinakiukwa kwa sababu ya rushwa mfano gari la abiria linapata ajali Saa Saba za usiku inamaana dereva kavunja Sheria hakupaswa kuendesha gari muda huo, pili Kuna traffic sehemu alipaswa kutoruhusu gari kuendelea na safari. Lakini pia abiria wenyewe wanaona sawa tuuu. Matatizo mengi husababishwa na kutowajibika na kukosa uzalendo

Mabasi yaliruhusiwa kutembea 24 hours sehemu nyingi ikiwamo Dodoma - Dar. Ajali ya usiku jana basi lilikuwa kwenye muda wake. Halikupaswa kuzuiliwa.
 
Wabongo ajali ziwauaaaa kama inziii

Nyie endeleeni na mwendo wenuu huoo

Sisi kazi yetu ni kula ubwabwa na kuzika tu

Ova
 
Tatizo la ajali za Tanzania ni barabara kuwa ndogo,halafu magari ni mengi.Kinachotakiwa kifanyike ni kupanua barabara zote kuu,Dar to Tunduma, Dar to Mwanza, Dar to Arusha, Dar to Mtwara.Hizo njia kuu zikishatanuliwa, tutakuwa tumeokoa vifo vya ajali kwa asilimia 90
Dar to Songea
 
Huna huja za msingi.
Zaidi ya 80% ya ajali ni ama dereva kukosa umakini au barabara mbovu/ nyembamba. Hebu mfikirie dereva ambae hapumzika vizuri halafu anapewa kuendesha gari toka bukoba mpaka Dar. Angalia muda wa ajali. Wanachoka. Bado madereva hawapimwi uwezo wao wa macho kuona mchana na wa usiku. Wengi tunaona vizuri mchana ila usiku taabu. Mamlaka ziamue safari ambazo ni lazima wawepo madereva 2 kila basi. Mfano
Dar to songea
Dar to Bukoba
Dar to Musoma
Dar to sumbawanga
Dar to Mpanda

Na kuwe na ukaguzi wa magari na vehicle inspection itolewe
 
Waruhusu watu wawekeze kwenye usafiri wa Reli, watu waingize treni za kisasa,nayo itapunguza ajali,wao wawe wajenga miundo mbinu tu, lakini siyo kwa hii selikali ya CCM inayofikiliaga uje uchaguzi ili waibe kura

Kulikimbia tatizo hakutatupa ufumbuzi:

Hatuwezi kuwa na madereva wanaoweza kuwajibika kwenye usukani?

1. Wasiendelee kwenda mbele kama mbele hawaoni?
2. Wazingatie mwendo wao kulingana na miundo mbinu.
3. Spidi limit iliyopo ikawa Kwa vyombo vyote?

Inatugharimu nini kufanya hayo?

Hatuwezi kujaribu wenye elimu zaidi?
 
Kuna mabasi yanayokwenda mbio kupitiliza lakini yanaangaliwa tu Hadi litokee Jambo ndio utasikia wenye dhamana wakitoa matamko.
Route ya Mbeya yako kampuni mbili za wachina na moja ya mzawa Tena wa hukohuko Mbeya. Njombe kampuni moja.
Mwanza kampuni kibao. Tanga kampuni moja. Manyara kampuni moja.
 
Nyepesi za muda huu kuna Bus mzinga tena - kutoka Bukoba -Dar; kibuyu kimelia mitaa ya Dodoma. Tutaishaa
 
Udereva Tanzania sio professional job.

Kwanza wanafanya kazi kama vibarua tu hawwezi kuwa na umakini na utulivu sababu ya stress.

Waajiriwe na kupewa mikataba ya ajira kama fani nyingine hawa wanabeba watu wengi.

Halafu wawe na elimu sio mtu kashindwa huko kakata tamaa ya maisha anakimbilia udereva yaniinakua kama bodaboda ambapo wengi ni wahuni tu au walikuwa vibaka huko sasa ni bodaboda ajali hazitoisha.
 
Ukweli n mchungu lakini tufike mahali tuuseme hata kama unauma.

Mengi yamesemwa kuhusu ajali miaka nenda rudi, lakini ajali ziko pale pale.

Bahati mbaya mzizi wa tatizo umekuwa hausemwi kwa kujua au kutokujua.

"Tatizo letu kuu kimsingi ni ujinga ndugu zangu."

1. Kulikoni dereva kuendesha gari akiwa haoni waziwazi anakokwenda?

2. Kulikoni dereva kuendesha gari bila kujali hali ya miundo mbinu alipo?

Pana haja ya kurekebisha viwango vya elimu angalau kwa kuanzia, madereva wa mabasi na malori.

Kwanini kutokuwatumia wahitimu wa vyuo vikuu kuendesha mabasi?

Kwanini kama ilivyo kwingine kama kiwango cha juu cha mwendo ni 80km/h, isiiwe hivyo kwa vyombo vyote vya moto barabarani?

Kwa kuzingatia haya tu, ajali zitakwisha.

Serikali inao wajibu.
Changamoto kubwa ni miundombinu

Mbona kuna nchi hawana hizi speed limits watu wanapwiyanga tu na hawana ajali nyingi kama sisi

Tutanue barabara zetu angalau tuwe na mbili kwenda mbili kurudi na wajitahidi kuweka taa za solar angalau kima KM 1 taa moja haijalishi ni wapi.

Mfano barabara ya Tanga kuja Msata , Msata Chalinze na hata Morogoro-Dodoma ni majanga tupu. Sasa hivi kapite Mwanza-Shinyanga sijui kuna ujenzi gani pale unaendelea yani hatari hatari hatari

Hizo ninazozijua mimi lakini zipo kibao
 
Huna huja za msingi.
Zaidi ya 80% ya ajali ni ama dereva kukosa umakini au barabara mbovu/ nyembamba. Hebu mfikirie dereva ambae hapumzika vizuri halafu anapewa kuendesha gari toka bukoba mpaka Dar. Angalia muda wa ajali. Wanachoka. Bado madereva hawapimwi uwezo wao wa macho kuona mchana na wa usiku. Wengi tunaona vizuri mchana ila usiku taabu. Mamlaka ziamue safari ambazo ni lazima wawepo madereva 2 kila basi. Mfano
Dar to songea
Dar to Bukoba
Dar to Musoma
Dar to sumbawanga
Dar to Mpanda

Na kuwe na ukaguzi wa magari na vehicle inspection itolewe
Hoja ya msingi ni ipi ndugu?

Dereva kukosa umakini ni nini kama ujinga haumo humo? Mtu aliye responsible hawezi kukosa umakini barabarani na bado ana roho 50 mikononi mwake.

Ukaguzi kwa ujuzi upi kama si suala la ulaji wa polisi tu?

Miundo mbinu mibovu linamuingiaje dereva kichwani na analitafsiri je hilo Kwa vitendo awapo kazini?

Siasa zimeshindwa kumaliza tatizo hili na tunataka kuendelea na hadithi zile zile.

Tusiosoma Tukiambiwa ujinga tunang'aka. Ujinga siyo tusi.

Tujaribu ya wasomi, ya kina msukuma tumeyaona.
 
Changamoto kubwa ni miundombinu

Mbona kuna nchi hawana hizi speed limits watu wanapwiyanga tu na hawana ajali nyingi kama sisi

Tutanue barabara zetu angalau tuwe na mbili kwenda mbili kurudi na wajitahidi kuweka taa za solar angalau kima KM 1 taa moja haijalishi ni wapi.

Mfano barabara ya Tanga kuja Msata , Msata Chalinze na hata Morogoro-Dodoma ni majanga tupu. Sasa hivi kapite Mwanza-Shinyanga sijui kuna ujenzi gani pale unaendelea yani hatari hatari hatari

Hizo ninazozijua mimi lakini zipo kibao

Hakuna nchi isiyo na speed limits. Kwingine ni speed limit kwa lane.

Swali la msingi kwenye changamoto za miundo mbinu dereva anachukua hatua gani?
 
Ukweli n mchungu lakini tufike mahali tuuseme hata kama unauma.

Mengi yamesemwa kuhusu ajali miaka nenda rudi, lakini ajali ziko pale pale.

Bahati mbaya mzizi wa tatizo umekuwa hausemwi kwa kujua au kutokujua.

"Tatizo letu kuu kimsingi ni ujinga ndugu zangu."

1. Kulikoni dereva kuendesha gari akiwa haoni waziwazi anakokwenda?

2. Kulikoni dereva kuendesha gari bila kujali hali ya miundo mbinu alipo?

Pana haja ya kurekebisha viwango vya elimu angalau kwa kuanzia, madereva wa mabasi na malori.

Kwanini kutokuwatumia wahitimu wa vyuo vikuu kuendesha mabasi?

Kwanini kama ilivyo kwingine kama kiwango cha juu cha mwendo ni 80km/h, isiiwe hivyo kwa vyombo vyote vya moto barabarani?

Kwa kuzingatia haya tu, ajali zitakwisha.

Serikali inao wajibu.

Umeanza vizuri sana ila kuna sehemu hazikuwa za lazima

1. Wahitimu wa chuo kikuu still ni binadamu, ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa kibinadamu ambao over the period of time, wote tunao.
2. Kuna maeneo mengi sana hapa nchini penye ruhusa ya kuendesha gari zaidi ya speed 80 kmh, zipo sehemu unaruhusiwa kutembea mpaka 120 kmh i.e. Katikati ya Singida na Shinyanga

Vipo vitu vingi sana kama ulivyosema vya kupunguza ajali, ndio lakini hakuna kitu cha kuondoka kabisa tatizo la ajali.
 
Hii nchi wenye elimu wanabezwa Sana , Ila ujinga ndo tatizo kubwa , umaskini pia , huwez kusafr more than 800 km Kwa basi , dunia za wenzetu hapo ni tren za umeme au aircraft , miundo mbinu mibovu na isiyokidhi , two lanes Kwa highway ni graveyard
Hii ndiyo comment yenye Akili..ufike muda safari ndefu isizidi km 400 inatosha lkn kutembea zaidi ya km 1300 ni majanga Tu hata Ile Sheria ya kuendesha mabus usiku ndiyo risks kubwa na serikali ni Bora wasiruhusu, suluhisho la ajali za barabarani ni kutumia train za umeme Tu kama nchi zilizoendelea
 
Kwamba nchi gani hapa Duniani hakuna ajali? Kiukweli kwa miundo mbinu ya barabara za Tanzania ilivyo mibovu na duni, tuwapongeze madreve wa Tanzania kwamba ajali sio nyingi sana!

Usisome kama kasuku. Soma Kwa kuelewa. Sweden nchi ndogo mno kuliko sisi yenye watu 10m ina takribani magari 5m. Sisi hapa hatuna 1m na nchi kubwa zaidi.

Uendashaji wetu usioakisi miundo mbinu yetu kwa sababu zozote zile ni lazima ubadilike.

Ya mipango ya Mungu hayatusaidii.
 
Vyombo ambavyo havilingani size heavy na light havipaswi tembea speed sawa

Kuweka 80kph kwa Lori,bus gari ndogo mtazika Sana

Gari dogo ukikuta Lori linatembea 80kph lipite kaa nalo mbali kabisa ukishindwa lipita acha iende mbali na wewe
You're right!!!!!
Nakumbuka rafiki zangu Fulani walikuwa hawana uzoefu na kuendesha magari safari ndefu wakawa wanatembea mwendo sawa na mabus kwenye vibao vya speed 50 chakushangaza walikuwa wanakamatwa na traffic lkn mabus yanaenda Tu,kitu ambacho walikuwa hawajui ni kuwa speed 50 ya bus Kwa wewe mwenye gari ndogo unafikisha Hadi speed 80
 
Umeanza vizuri sana ila kuna sehemu hazikuwa za lazima

1. Wahitimu wa chuo kikuu still ni binadamu, ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa kibinadamu ambao over the period of time, wote tunao.
2. Kuna maeneo mengi sana hapa nchini penye ruhusa ya kuendesha gari zaidi ya speed 80 kmh, zipo sehemu unaruhusiwa kutembea mpaka 120 kmh i.e. Katikati ya Singida na Shinyanga

Vipo vitu vingi sana kama ulivyosema vya kupunguza ajali, ndio lakini hakuna kitu cha kuondoka kabisa tatizo la ajali.
Hizi unilateral assessment ndizo tatizo letu kubwa ambapo bila utafiti wowote mtu ana mahitimisho kama yote:

1. Ajali nyingi tatizo liko kwenye common sense kutofautiana baina ya watu.
2. Common sense ni common kulingana na kiwango cha elimu ya mtu. (Labda kama si Kwa Tanzania ambako ni exception).

Chuo kikuu, kwangu umekuwa mfano tu, kwani hawa ni watu ambao wapo hawana kazi na wanaweza kuzifanya kazi hizi kwa ubora zaidi.

"Ni wazi kuwa msomi hata akilima nyanya atalima kwa ubora zaidi."

3. Speed 120km/h barabarani zimeruhusiwa majuzi juzi. Barabara zote kwa Tanroads zilikuwa 80km/h kwa magari yote Kwa mujibu wa wajenzi wa barabara.

Hawa wenye miendo isiyokuwa na ukomo ni kisababishi kingine cha ajali hadi kwa wasiohusika.

Ajali zina kinga katika mazingira yote, na huo ndiyo ulio msingi wa hoja.
 
Back
Top Bottom